Ana za vyaula somo la 10: Vyaula vya vitamini E
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu vitamini E, kazi zake mwilini, vyakula vyenye vitamini E pamoja na madhara ya kutokuwa na vitamini E vya kutosha mwilini
Vitamini E na Faida Zake Mwilini
Vitamini E ni moja ya vitamini muhimu vinavyopatikana kwenye vyakula, matunda, na mboga. Pia unaweza kuipata kwa njia ya vidonge kutoka kwenye maduka ya madawa. Kama ilivyo kwa vitamini A, B, C, D na K, upungufu wa vitamini E mwilini unaweza kusababisha madhara ya kiafya, ijapokuwa upungufu wa vitamini huu ni nadra sana kutokea. Katika makala hii, nitakupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake, na madhara ya upungufu wake.
Yaliyomo:
- Maana ya Vitamini E
- Kazi za Vitamini E
- Vyakula vya Vitamini E
- Upungufu wa Vitamini E
- Tafiti Kuhusu Vitamini E
Maana ya Vitamini E
Mnamo mwaka 1922, wanasayansi wawili kwa majina ya Herbert Mclean Evans na Katharine Scott Bishop waligundua vitamini E. Baada ya ugunduzi wa vitamini E, tafiti mbalimbali zilifanywa ili kuonyesha kazi zake mwilini. Kwa mfano, mwaka 1946, wanasayansi walikuwa wakifanya tafiti juu ya nadharia inayodai kuwa vitamini E husaidia dhidi ya maradhi ya moyo na mishipa ya damu (coronary heart diseases). Mwaka 1949, tafiti zilifanywa kuhusu nadharia ya kuwa vitamini E huweza kusaidia watoto njiti kuwakinga na maradhi kadhaa.
Kazi za Vitamini E Mwilini
Vitamini E katika miili yetu ina kazi kuu zifuatazo:
- Antioxidant: Vitamini E ni antioxidant, ambayo husaidia kuzuia athari za kemikali mbaya ambazo zinaweza kuharibu miili yetu.
- Utando wa Seli: Husaidia katika utengenezwaji wa utando wa seli na kulinda seli dhidi ya uharibifu wa kemikali.
- Ukuaji wa Misuli: Husaidia katika ukuaji mzuri wa misuli.
- Utando wa Neva na Mapafu: Husaidia katika utengenezwaji wa utando katika maeneo mbalimbali ya mwili kama neva, mapafu, na maeneo mengine.
Upungufu wa Vitamini E
Upungufu wa vitamini E hutokea nadra sana, lakini tafiti zinaonyesha kuwa upungufu huu unaweza kusababisha matatizo kwenye mfumo wa fahamu, ukuaji mzuri wa misuli, na udhaifu wa misuli. Pia, upungufu wa vitamini E unaweza kuathiri macho na hivyo kupelekea mtu kutoona vizuri.
Vyakula vya Vitamini E
- Nyama ya kuku na ng'ombe
- Maini
- Mayai
- Alizeti
- Karanga
- Spinach
- Korosho
- Mchele
- Viazi vitamu
- Siagi
- Samaki
- Maziwa
- Palachichi
Tafiti Kuhusu Vitamini E
Tafiti mbalimbali zimefanywa kuhusu vitamini E, lakini zinahitaji kuendelea zaidi maana bado majibu ya uhakika hayajapatikana juu ya matokeo ya tafiti hizo. Ijapokuwa maneno ni kama hivyo, ukweli ni kuwa vitamini E vina faida katika afya zetu. Miongoni mwa tafiti hizo ni:
- Mwaka 2017: Tafiti zilionyesha kuwa vitamini E husaidia kupunguza udhaifu wa misuli wakati wa kuzeeka.
- Maradhi ya Ubongo: Tafiti zinaonyesha kuwa vitamini E husaidia kulinda dhidi ya maradhi ya ubongo kama kusahausahau na kuchanganyikiwa.
- Saratani: Tafiti zinaonyesha kuwa vitamini E husaidia kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya figo, kibofu, mapafu, na korodani.
- Maradhi ya Moyo na Mishipa ya Damu: Vitamini E husaidia kulinda mwili dhidi ya maradhi ya moyo na mishipa ya damu.
- Wajawazito: Vitamini E ni muhimu kwa wajawazito kwani husaidia katika ukuaji wa fetasi na kulinda afya ya mama.
Hitimisho
Vitamini E ni muhimu sana kwa afya ya binadamu. Ni muhimu kuhakikisha unapata vitamini E ya kutosha kupitia lishe sahihi na, inapohitajika, kupitia vidonge vya vitamini E. Kwa kufanya hivyo, utakuwa unadumisha afya yako na kuepuka athari zinazoweza kusababishwa na upungufu wa vitamini E. Endelea kuwa makini katika lishe yako na ufuatilie tafiti mpya kuhusu vitamini E ili kujua faida zaidi zinazoweza kutolewa na vitamini hii muhimu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 web hosting 👉6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Faida za kiafya za kula majani ya kunde
Leo tutajifunza kuhusu majani ya kunde — mboga za kijani zinazotokana na mmea wa kunde (beans). Wengi hula mbegu za kunde pekee, wakisahau kuwa hata majani yake yana virutubisho vya thamani kubwa kwa mwili. Tutazungumzia vitamini, madini, na faida mbalimbali za kiafya zinazopatikana katika majani haya.
Soma Zaidi...Faida za kiafya za kula mbegu za matikiti
Katika post hii utajifunza faida za kula mbegu za tikiti. Baada ya post hii utajifunza kuwa mbegu za tikiti hazitupwi.
Soma Zaidi...Faida za kiafya za mbegu za papai
Mbegu za papai zina faida nyingi za kiafya ambazo zinaweza kuboresha afya yako kwa njia nyingi. Kutoka kuboresha mmeng'enyo wa chakula hadi kupambana na saratani, mbegu hizi ni chanzo kikubwa cha virutubisho na viambata vya asili
Soma Zaidi...Aina za vyakula somo la 72: Faida za kiafya za kula matembele
Katika somo hili utakwenda kujifunza namna ambavyo matembele yanaweza kuboresha afya ya mwili wako.
Soma Zaidi...Aina za vyakula somo la 32: Faida za kula magimbi
Katika somo hili utakwenda kujifunza faida za kiafya za kula magimbi. Magimbi ni vyakula aina ya mihogo na viazi.
Soma Zaidi...Aina za vyakula somo la 5: vyakula vyenye maji mengi, faida zake na kazi zake
Katika makala hii utakwenda kujifunza kuhusu maji, faida zake na upungufu wake. Pia utajifunza vyakula vyenye maji kwa wingi
Soma Zaidi...