image

Sababu za maumivu ya tumbo kitovuni na dalili zake

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo kitovuni na dalili zake

SABABU ZA MAUMIVU YA TUMBO KITOMVUNI NA DALILI ZAKE

 

1.Kuwepo na uvimbe kwenye njia ya chakula (digestive track) kitaalamu hufahamika kama gastroenteritis. Hali hii inaweza kusababishwa na virusi, bakteria ama parasite. Mgonjwa anaweza kusikia maumivu na yanaweza kuwa ni makali sana. Mara nyingi maumivu haya yanapoa yenyyewe bila hata kuhitaji matibabau ha huondoka ndani ya siku chache. Ila ni vyema kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.

 

Dalili zakeTofauti na kuwa mgonjwa atakuwa anaumwa na tumbo kwenye kitomvu, lakini tumbo hili litafungamana na dalili zifuatazo:-1.Kuharisha2.Kichefuchefu3.Kutapika4.Homa5.Kutokwa na jasho sana

 

2.Kuvimba kwa appendix. Maumivu ya tumbo kwenye kitomfu yanaweza kuashiria ugonjwa wa appendix, kitaalamu hufahamika kama appendicitis. Kama utahisi maumivu makali ya tumo kitomvuni kisha ghafla yanahamia upande wa kulia wa tumbo kwa chini, huashiria tatizo hili. Tofauti na kuwepo kwa maumivu haya pia mgonjwa ataona dalili flani.

 

Dalili za ugonjwa wa appendix1.Kujaa kwa tumbo na kukaza kama mtu aliye vimbiwa2.Kichefuchefu3.Kutapika4.Kuhisi maumivu ambayo huwa yakiongezeka kila unapokohoa ama unapojongea.5.Mvurugiko wa tumbo kama kukosa choo au kuharisha6.Homa7.Kukosa hamu ya kula.

 

Ugonjwa huu ni katika magonjwa ambayo yanahitajika kutibiwa mapema na haraka sana. Endapo mgo jwa atachelewa kutibiwa appendix inaweza kupasuka, na endapo itapasuka inaweza kuhatarisha maisha.

 

3.Vidonda vya tumboYes maumivu ya tumbo kitomvuni yanaweza kuwa yamesababishwa na vidonda vya tumbo, huwenda vipo kwenye tumbo la chakula ama sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayotambulika kama duodenum. Tofauti na maumivu ya tumbo kwenye kitomvu pia mgonjwa ataona dalili zifuatazo

 

Dalili za vidonda vya tumbo:1.mvurugiko wa tumbo2.Kuhisi tumbo kujaa na kucheua3.Kichefuchefu4.Kutapika5.Kukosa hamu ya kula6.Kutoa hewa kwa mdomoni kwa sauti

 

4.Matatizo kwenye kongoshoHuu ni ugonjwa unaosababisha kuvimba kwa kongosho kitaalamu huitwa Pancreatitis. Maradhi haya yanaweza kuja ghafla sana bila ya kuonyesha ishara za awali. Pia zinapoonyesha dalili zake huwa ni kama:-

 

Dalili za maradhi ya kongosho1.Kichefuchefu2.Kutapika3.Homa4.Mapigo ya moyo kuongezeka

 

5.Kuwa na ngriri ya heniaUgonjwa huu huwapata wanaume, na hutokea pale ambapo baadhi ya tishu za tumboni zinapoingia kwenye misuli ya tumboni karibu na kitomvu. Kwa watu wazima upasuaji hufanyika ili kutibu tatizo.

 

6.Kama kuna kizuizi katika utumbo kinachozuia chakula kutembea. Tatizo hili likichelewa kutibiwalinaweza kuwa hatari zaidi. Tatizo hili huweza kusababishwa na:-1.Mashambulizi ya bakteria2.Henia3.Uvimbe4.Kama kulitokea shida wakati wa kufanyiwa upasuaji.

 

Dalili1.Kichefuchefu2.Kutapika3.Tumbo kujaa4.Kupunguwa maji5.Kukosa hamu ya kula6.Kukoa choo7.Homa8.Kuongezeka kwa mapigo ya moyo

 

7.Matatizo katika mishipa mikuu ya damu kwenye tumbo (aortic aneurysm). hili ni tatizo la kiafya linalosababishwa na kudhoofu na kutanuka kwa kuta za mishipa mikuu ya damu. Hali hii inaweza kuhatarisha maisha ya mtu kama mishipa ya damu itapasuka na kupelekea damu kuingia tumboni, hii inaweza kupelekea maumivu makli. Maumivu haya yanaweza kuathiri na viungo vingine.

 

Dalili nyingine:-1.Kupata pumzi kwa tabu2.Kushuka kwa presha ya damu3.Kuongezeka kwa mapigo ya moyo4.Kuzimia5.Udhoifu wa ghafla upande mmoja wa mwili

 

8.Kama kutakuwa na shida wakati wa mzunguko wa damu katika tumbo (mesenteric ischemia). hii hutokea endapodamu inayotembea kwenye utumbo mdogo itapata usumbufu, kwa mfano ikiganda. Mgonjwa anaweza kusikia maumivu makali ya tumbo. Maumivu haya huandamana na dalili kama:-1.Kuongezeka kwa mapigo ya moyo2.Kuona damu kwenye choo





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1188


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Dalili za malaria
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya dalili za maralia Soma Zaidi...

Dalili za maumivu ya jino
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za maumivu ya jino Soma Zaidi...

Dalili za tezi dume ambayo hazijashuka (cryptorchidism)
Tezi dume ambayo haijashuka si ya kawaida kwa ujumla, lakini ni ya kawaida kwa wavulana waliozaliwa kabla ya wakati.na muda mwingine zikipanda tumboni huwa hazishuki kabisa kwenye korodani. Soma Zaidi...

VIPIMO VYA MINYOO (UTAJUAJE KAMA UNA MINYOO)? fecal test, blood test, colonoscopy tape test X-ray, MRI na CT scan.
VIPIMO VYA MINYOO Haitoshelezi kuwa na dalili pekee ukathibitisha kuwa una minyoo. Soma Zaidi...

Kivimba kwa utando wa pua
post hii inazungumzia kuhusiana na kuvimba kwa utando wa pua unaoonyeshwa na mchanganyiko wa dalili zifuatazo: Kupiga chafya Msongamano wa pua Muwasho wa kiwambo cha sikio Kuwasha kwa pua na koromeo Uvimbe huu hutokea ikiwa mashambulizi ya kupiga chafya, Soma Zaidi...

Maradhi ya Ini na dalili zake, na vipi utajikinga nayo
MAGONJWA YA INI NA DALILIZAKE, NA KUKABILIANA NAYO Ini ni katika viungo vikuu katika mwili wa binadamu. Soma Zaidi...

Ninashida Kuna mtu anaumwa pressure Kila anap pima Iko juu il mwil aumuumi at kidg n dawa anatumia unawez kunisaidiaj
Kama unasumbuliwa na presha post hii ni kwa ajili yako. Hapa tutakuoatia ushauri kutokana na swali alilouliza mdau wetu. Soma Zaidi...

Dalili za maambukizi ya sikio kwa watoto
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za maambukizi ya sikio kwa watoto. Soma Zaidi...

Namna ya kuishi na vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ya kuishi na vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

Ujuwe ugonjwa wa ebola, dalili zake na jinsi unavyoweza kusambazwa.
Posti hii inahusu sana kuhusu ugonjwa wa ebora. Ugonjwa huu usababishwa na virusi.Virusi hivyo husababisha kutokwa na damu nyingi mwilini kutokana na kupasuka kwa mishipa ya damu Soma Zaidi...

Walio hatarini kupata gonorrhea (gonoria)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu watu walio hatarini kupata gonorrhea gonoria Soma Zaidi...

Saratani ya Matiti ya wanaume.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Saratani ya matiti ya Mwanaume ni Saratani nadra ambayo hutokea katika tishu za matiti za wanaume. Ingawa saratani ya matiti hufikiriwa zaidi kuwa ugonjwa wa wanawake, saratani ya matiti ya mwanaume hutokea. Saratani y Soma Zaidi...