Namna ya kujitwaharisha Najisi ndogo
Kujitwaharisha Kutokana na Najisi
Kutokana na uzito wa kujitwaharisha tutazigawanya najisi katika makundi matatu
(a)Najisi ndogo.
(b)Najisi kubwa na
(c)Najisi hafifu
(a)Najisi Ndogo.
Najisi Ndogo
Inahusu najisi zote isipokuwa najisi ya mbwa na nguruwe. Namna ya kujitwaharisha kutokana na najisi ndogo ni kuosha paliponajisika kwa maji safi mpaka iondoke rangi na harufu ya najisi.
Kama tunatumia maji machache ambayo huharibika mara tu yatakapoingiwa na japo najisi ndogo, hatuna budi kutumia kata au chombo kingine cha kuchotea maji na kujitwaharisha pembeni kwa kujimiminia maji kupitia sehemu ile yenye najisi mpaka najisi hiyo iondoke.
Katika hali ya kawaida, maji safi hutumika kwa kustanjia. Tunazitwaharisha sehemu zetu za siri kwa mkono wa kushoto mpaka tuhakikishe kuwa najisi imeondoka. Katika hali ya dharura ya kukosa maji au ugonjwa usioruhusu kutumia maji, tunaruhusiwa kustanji kwa kutumia vitu vikavu kama vile karatasi laini (toilet paper), mawe, n.k. Tukistanji kwa vitu vikavu, kama vile mawe makavu tutapangusa sehemu zetu za siri kwa mawe matatu. Kama najisi ingalipo, tutaongeza mawe mawili mawili mpaka turidhike kuwa najisi imeondoka.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 ai web app 👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Zijuwe nguzo 17 za swala.
Ili swala itimie utahitajika kutimiza nguzo zake na masharti yake. Hapa utajifunza nguzo 17 za swala.
Soma Zaidi...Yaliyoharamishwa kwa mwenye kuwa katika ihram
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Aina za twahara na aina za najisi
Katika post hii utakwenda kuzijuwa aina za twahara katika uislamu. Utaviona vigawanyo vya twahara kulingana na maulamaa wa Fiqh
Soma Zaidi...Njia za kudhibiti riba
Ufumbuzi wa tatizo la ribaRiba imeenea na kuzoeleka duniani kwa kiasi ambacho watu wengi wanadhani kuwa bila riba hakuna shughuli yoyote ya uchumi inayowezekana.
Soma Zaidi...