Epuka kuwa muoga na yajue madhara ya uwoga

36.

Epuka kuwa muoga na yajue madhara ya uwoga

36. Kuepukana na Woga



Kinapokosekana kipengele hiki cha 'kumtegemea Mwenyezi Mungu katika kila hali' katika tabia au mwendo wa mja nafasi yake inajazwa na kipengele cha 'woga'. Woga na khofu juu ya matukio mbali mbali ya maisha ya hapa ulimwenguni husababishwa na uhaba wa imani


juu ya Allah (s.w) na sifa zake. Mtu asiyemtegemea Mwenyezi Mungu hudhania kuwa mafanikio yote ya maisha hupatikana kwa uwezo wa mwanaadamu na kuwa ni mwanaadamu pekee mwenye uwezo wa kujikinga na shari zote zinazomkabili.Dhana hii humtia mtu katika wasi wasi na woga atakapohisi kuwa tatizo au dhara fulani linalomkabili litamshinda nguvu kwa kuwa hana uwezo au msaada wa mwanaadamu wa kumuwezesha kupambana nalo.



Muislamu wa kweli hapaswi kuwa mwoga wa chochote kwa sababu hapana chochote kinachoweza kumdhuru, ila awe amekadiria hivyo Mwenyezi Mungu (s.w) na hapana mja awezaye kuepa ajali yake aliyoandikiwa na Mwenyezi Mungu. Muislamu anatakiwa awe imara katika kusimamisha Dini ya Allah katika kila kipengele cha maisha yake, bila ya kuhofu chochote kwani yeye daima yuko chini ya ulinzi na uangalizi wa Mwenyezi Mungu (s.w), na halitamsibu ila lile alilomuandikia Mwenyezi Mungu (s.w).


'Sema; halitatusibu ila alilotuandikia Mwenyezi Mungu, yeye ni Mola wetu. Basi Wa is lamu na wamtegemee Mwenyezi Mungu tu '(9:51).
Pia Allah (s.w) ametukataza kuwaogopa makafiri:


' Leo makafiri wamekata tamaa na dini yenu basi msiwaogope, bali
n iogop en i mimi '(5:3).




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 135

Post zifazofanana:-

KUMUAMINI MWENYEZI MUNGU
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Tikiti
Soma Zaidi...

Sababu kuu za maumivu ya tumbo chini ya kitomvu, Tumbo la ngiri na chango
Makala hii inakwenda kukuletea somo linalozungumzia maumivu ya tumbo chini ya kitomvu, na tumbo la ngiri kwa wanaume, na tumbo la chango kwa wanawake Soma Zaidi...

Sababu za Kushuka Surat Al-Masad (tabat yadaa) na fadhila zake
4. Soma Zaidi...

NJIA ZA KUJIKINGA NA MALARIA (zijue njia za kupambana na mbu wa malaria)
Soma Zaidi...

Faida za kula Palachichi
Palachichi lina virutubisho vingi na vitamini, kula palachichi uiokoe afya yako Soma Zaidi...

Kumuandaa Maiti kabla ya kufa ama kukata roho
Soma Zaidi...

ENGLISH STATARD FOUR TEST
Soma Zaidi...

Standard Seven Geography Review
Soma Zaidi...

IJUE MALARIA; DALILI ZAKE, TIBA YAKE, ATHARI ZAKE NA KINGA YAKE
MALARIA NI NINI HASA? Soma Zaidi...

DARSA ZA QURAN
Soma Zaidi...

Tofauti ya uchumi wa kiislamu na usio wa kiisalmu
Tofauti kati ya mfumo wa uchumi wa Kiislamu na ile ya Kitwaghuti (i) Dhana ya mafanikioKatika mtazamo wa uchumi wa Kiislamu mafanikio yanatazamwa kwa kuzingatia hatima ya ama mtu kupata radhi za Mwenyezi Mungu au kubeba laana ya Mwenyezi Mungu. Soma Zaidi...