Kumuandaa maiti punde baada ya kufariki dunia

Kumuandaa maiti punde baada ya kufariki dunia

Mambo Anayofanyiwa Mtu mara tu baada ya Kufa



Baada ya kushuhudia kuwa ndugu yetu ameshakata roho vyema tuseme na kuzingatia maneno yafuatayo kama alivyotufahamisha Allah (s.w)
'... Hakika sisi ni wa Allah na kwake tutarejea ...' (2:156).



Maneno haya ni ya msingi sana katika hali hii ya kufiwa, kwani yanawaliwaza wafiwa na kuwaepusha na fadhaa zinazoweza kutokea juu ya kifo cha marehemu. Ukizingatia maneno ya aya hii utaona kuwa kwa vyovyote iwavyo, kurejea kwa Allah ni jambo lisilozuilika. Hivyo, chochote kile kitakachokuwa ndio sababu ya kifo cha marehemu kitakuwa ni sababu tu ya kifo hicho aliyoiweka Allah (s.w)



Baada ya maliwazo haya maiti ile yapasa kufanyiwa yafuatayo:


1. Kwa taratibu rudishia mdomo usibakie wazi kwa kufunga kidevu kwa kitambaa na kukizungushia kichwani.



2. Funga macho ya marehemu kwa taratibu na huku ukisoma:



'Kwa jina la Allah na kwa kufuata mila ya Mjumbe wa Allah. Ewe Mola wetu mrahisishie mambo yake ya sasa na msahilishie mambo yake baadaye. Na jaalia atakayokutana nayo yawe bora kuliko aliyoachana nayo'.



3. Lainisha viungo vya maiti kwa kukunja na kukunjua pole pole sehemu zote zenye viungo katika mikono na miguu. Kama patakuwa na ugumu wowote katika kumnyoosha viungo hivyo, maji ya moto au mafuta yanaweza kutumika ili kulainisha. Baada ya kulainisha viungo, miguu na mikono inyooshwe na alazwe huku uso ukielekea Qibla kwenye kitanda kisichokuwa na godoro.



4. Maiti avuliwe nguo zote alizokufa nazo kisha kumgubikwa kwa shuka kubwa, pia ni vyema afungwe kitambaa tumboni au kuwekewa kitu chenye uzito kidogo juu ya tumbo ili lisifutuke sana.



5. Marashi na ubani vitumike sana mahali alipo maiti ili kuzima harufu ya uvundo itokayo kwa maiti.Mwanaadamu ni msafi sana anapokuwa hai. Lakini muda mfupi tu baada ya kufa huanza kutoa harufu kali ya uozo.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 160


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

ENYI WAJA WANGU NIMEIKATAZA NAFSI YANGU DHULMA
Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII MUSA(A.S) NA HARUN(A.S)
Nabii Musa(a. Soma Zaidi...

Imam Malik Ibn Anas
Soma Zaidi...

Darsa za Sira historia ya Mtume (s.a.w) Jaribio la 02
Soma Zaidi...

Ni zipi siku ambazo ni haramu kufunga? na ni kwa nini hairuhusiwi kufunga katika siku hizo
Soma Zaidi...

'Allah (s.w) humwingiza katika rahma zake amtakaye na kumwacha kupotea amtakaye'
Soma Zaidi...

Waliomuamini Nabii Nuhu(a.s)
Waliomuamini Nuhu(a. Soma Zaidi...

kuwa muaminifu na kuchunga Amana
Uaminifu ni uchungaji wa amana. Soma Zaidi...

SHUGHULI ZA KILA SIKU
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Kubisha hodi katika nyakati za faragha katika familia
'Enyi mlioamini! Soma Zaidi...

Adam(a.s) na Mkewe Katika Pepo
Adam(a. Soma Zaidi...

SHARTI ZA KUWAJIBIKA KWA ZAKA
Soma Zaidi...