Navigation Menu



image

HADITHI YA BINTI WA KWANZA NA MBWA

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA BINTI WA KWANZA NA MBWA.

HADITHI YA BINTI WA KWANZA NA MBWA

pic
Download kitabu Hiki Bofya hapa

HADITHI YA BINTI WA KWANZA NA MBWA.

Kwanza jua ewe mtukufu mfalme kuwa wale mbwa wawili uliowaona ninawapiga ni ndugu zangu wa baba na mama mmoja. Tuliishi pamoja kwa zaidi ya miaka 10 toka kufariki kwa baba kabla ya kutokea yale ambayo umeyashuhudia usiku wa jana. Basi tambua ewe mtukufu mfalme kuwa dada zangu hawa walinifanyia ubaya ambao ndio chanzo cha haya yote. Basi wakati Zubeida anazungumza maneno haya mbwa walikuwa wakitingisha vichwa na kutowa machozi.

Tambua ewe mtukufu mfalme kuwa yote niliyokuwa nikiyafanya ni kwa ajili ya uhai wa mbwa hawa yaani dada zangu. Laiti kama sitawachapa fimbo zili wangelikufa papo hapo. Juwa ewe mfalme wa nchi hii kuwa yote niliyokuwa nikiyafanya sikuyafanya kwa hiari yangu ila nimeshinikizwa. Nini kulitutokea na nini ninachotakiwa kufanya. Nitaomba ushauri wako ewe mfalme baada ya kusikiliza hadithi yetu.

Basi pale kwenye ukumbi wa mfalme kukaingiwa na utulivu wa hali ya juu. Machongo watatu walikuwepo wakitaka kujua zaidi kilichowakuta wenzao. Wakati mfalme na waziri wake wananshauku ya kutaka kujuwa hasa nini kilimtokea Zubeida. Basi mfalme akaagiza hadithi hii iandikwe kwa wino wa dhahabu na iwekwe kwenye nyaraka maalumu. Basi Zubeida akaanza kuhadithia zaidi kama ifuatavyo;-

Tuliishi na baba yetu kwa furaha zaidi kwa muda wa miaka mingi. Mama yetu alifariki tukiwa wadogo, hivyo baba yetu akalazimika kuwa na majukumu ya umama. Baba yetu alikuwa ni mfanya biashara maarufu na alikuwa amefaniukiwa kwa kiasi kikubwa sana. Baba yetu alifariki kwa ghafla hata bila ya kuumwa. Baada ya mazishi tuligawana mirathi kwa mujibu wa sheria ya kuuslamu. Na kwa kuwa hatukuwa na ndugu wa kiume sote tulipewa mali ya mirathi kwa usawa kila moja.

Mimi na dada zangu wote tukawa tunafanya biashara. Wote tulinunua nyumba na kuendelea na biashara zetu. Kwa upande wangu nilifanikiwa sana na biashara zangu zilikuwa kwa haraka zaidi. kwa muda mfupi niliweza kurudisha mtaji wangu na kuanza kukusanya faida. Halikadhalika na dada zangu nao waliweza kutengeneza faida kwa muda mchache. Unaweza kusema lkuwa tulibarikiwa kibiashara.

Dada zangu waliolewa lakini mimi sikubahatika kupata mchumba. Siku szote nilikuwa namuomba Mwenyezi Mungu anipatie mchumba aliyekuwa ni mwema. Dada wa kwanza alipoolewa alihamishwa na mumu wake na kwenda mji wa jirani. Huko aliendelea na biashara zake pia, lakini kwa vituko vya mume wake hakuchukuwa muda akafilisika. Bila ya kuelewa chochote kumbe dada yangu aliposwa na mume yule si kwa sababu alimpenda ila ni kwa sababu ya mali zake.

Dada alipofiliskisa hakuweza kumuona mumewe tena kwake. Na alipokuja humpiga na kumtukana sana. Hakuwa hata anamletea cha kukila wala cha kuvaa. Nikiwa sina habari ya hili wala lile kwa yanayompata dada yangu. Hali iliendelea kuwa ngumu kwa dada yangu hata mambo yakamshinda. Kwa mujibu wa sheria za kadhi aliweza kudai talaka na kuachwa. Siku ile aloachwa yule mume wake alimvizia na kumpiga na kumchania nguo zake na kumnyang’anya kila alichokibeba.

Dada yangu alijikongoja hata akafika nyumbani kwangu. Kwa hakika sikumtambua kwa hali alonayo maana alikuwa ni nusu uchi. “Ashakumu si matusi” dada yangu akaniambia nisitiri ndugu yangu kwa hakika nimekumbwa na msiba ambao sitausahau. Basi nilimpatia pesa ambayo nimeiweka akiba na kumpatia aanze na biashara. Dada aliweza kuanza biashara tena na kuanza kukuza mtaji. Alipotaka kunirudishia pesa nilompa nilikataa na kumwambia kuwa ilikuwa ni sadaka.

Kwa upande wa dada yangu wa pili yeye alipotaka kuolewa katu sikumilia kipingamizi. Na aliolewa na mfanyabiashara mwenzie wa nchi ya jirani.. Hawa walikuwa wakifanya biashara za majini kutoka kisiwa mpaka kisiwa. Basi dada na mume wake walifanya hivyo kwa juda wa miezi 6. kwa muonekano walionesha kupendana sana na kuishi kwa amani na furaha katika ndoa yao. Kwa ndani mambo hayakuwa hivyo. Kwa kuwa dada alibarikiwa kibiashara pia alikuwa na mali nyingi hata akamzidi mume wake zaidi ya mara tatu. Sasa bila ya yeye kutambua kumbe mume wake aliuwa napanga njama ya kumuibia mali zake na kumtelekeza. Siku moja walipokuwa kwenye dau mume wake alipanga njama na nahodha ili alizamishe dau kimaksudi. Kwa kuwa dada hakujuwa kuogelea waliamini atakufa tu. Basi walifanya kama hivyo na jahazi lilipozama dada alitumbukia majini.

Kwa kuwa ilikuwa ni njama nahodha na wenzake waliweza kuokoa mali na watu wengine na kumuacha dada yangu kuangamia majini. Mume wa dada waliendelea na safari zao wakiamini kwa kuwa dada ameshakufa kinachofata ni kugawana mali. Na mambo yakawa kama hivyo walivyopanga. Lakini kitu kimoja hakikuwa kama walivyotaka, ni kuwa dada yangu katu hakufia majini na aliokoka kwenye ajali hii. Kwa kweli Mwenyezi Mungu ni mkubwa.

Wakati dada alipotumbukizwa kwenye maji wanyama wa majini walikuwa wakicheza na samaki mkubwa alimbeba na kuja kumtupia ufukweni. Na kwa hali hii dada yangu aliweza kuokoka. Kwa bahati nzuri dada alipookolewa alitupwa kwenye ufukwe wa nchi yetu hii na kutegemea nguo alizoziokota ufukweni aliweza kuja nyumbani. Kwa hakika nilishindwa kumtambua isingelikuwa kidani chake alichokuwa anakipenda.

Sasa mimi na dada zangu tumekusanyika tena nyumbani baada ya utengano wa muda. Nilimpatia dada yangu huyu nae pesa kama nilompa dada yangu wa kwanza. Ana alianza kufanya biashara zake. Dada zangu hawa waliungana pamoja na kuanza kufanya biashara za majini. Hivyo wakawa wanatembea kwenye visiwa mbalimbali kufanya biashara. Kwakweli biashara zao zilikuwa vizuri sana na walipata umaarufu na mali nyingi pia. Walifanya hivi kwa muda mrefu takribani kwa miaka miwili. Sikujuwa kumbe waliweza kuwa na hisia za ubaya juu yangu.

Wakati fulani wakaniomba niungane nao kwenye biashara zao lakini nilikataa. Walirudia kuniomba kwa zaidi ya mara 4 kwa nyakati tofauti. Basi mara ya tano nikakubali na kwa haraka wakaanza kuandaa safari na kuniandalia pia kwa upendo walionesha kunijali sana.basi nikagawa pes zangu mafungu mawili, fungu moja nikalifukia kama akiba na fungu la piali nikalitumia kuandaa bidhaa. Basi maandalisi yalipokamilika sote tulitoka na kuelekea ufukweni na kupanda jahazi letu lililojaa bidhaa. Safari ilikuwa njema sana, na nilifurahia pia maana ilikuwa ni mara yangu ya kwanza japo nilitapika sana.

Tulikwenda kisiwa mpaka kisi tukifanya biashara. Kwa hakkika nilipata faida sana kuliko pale nyumbani. Kwa safri yote nilikuwa naomba tufike salama maana sikupenda mazingira ya majini. Basi tulipokuwa tukirudi nyumbani kwa ghafla upepo ulubadilika na mawimbi yakawa makubwa. Nahodha hakuweza kutia nanga hinyo akaliwachia jahazi lielekee kokote kule na hii ndio njia salama kwa manahodha. Basi jahazi lilikwenda mpaka upepo ulipotulia asubuhi ya siku ilofata.

Tulishangaa tupo karibu na kisiwa ambacho kinaonekana ni mawe tu. Basi nahodha alipoulizwa hakuwa na ujuzi wa eneo hili, ila akashauri watu waingie kisiwani ili wakapate maji ya kunywa na kupata hewa safi. Kitu cha kushangaza ni kuwa kisiwa kizima kilikuwa ni mawe. Yaani majimba, miti, wanyama, watu na mikokoteni ni mawe matupu. Hata walinzi wa magetini walionekana kuwa mawe matupu. Kwa hakika huu mji ulikuwa ni wa ajabu sana. Kila mtu alitaka kujuwa habari za mji ule lakini ni nani wa kuwaambia.

Jambo linhine la kushangaza ni kuwa pesa na dhahabu zilikuwa zikizagaa masokoni ambapo watu wake wamegeuka mawe. Watu wa kwenye jahazi walikuwa wakistaajabu na kuanza kukusanya pesa na dhahabu. Kwa upande wangu niliendelea ndani zaidiya mji ule kujuwa zaidi habari. Nilipokwenda nikaingia kwenye ukumbi wa mfalme na nikamkuta amekaa kwenye kiti chke akiwa ni jiwe. Dahabu alizovaa zilikuwa zikining’inia tuu. Nikasogea zaidi na kukuta baraza la malkia likiwa na wanawake wengi nao wakiwa ni jiwe na mapambo yao ya dhahabu yakining’inia tuu.

Kwa hakika nilistaajabu sana na niliendelea pia. Niliona mambo mengi na ya kushangaza. Nilipokuwa kwenye eneo la kulia chakula watu nikuta wamegeuka mawe na vyakula vikiwa vizima hata kuharibika bado. Nikiwa katika hali ya mshangao nikasikia sauti ya mtu anasoma Qurani. Sikuamini hivyo nikasikiliza vizuri sauti ile na kupata uhakika wa kuwa nimesikia vyema. Hivyo nikaanza kuifata sauti ile hata nikaingia kwenye kijichumba kimoja na kumkuta kijana wa kiume mzuri sana. Nilibakia nikistaajabu kwa uzuri wake hata nikasahau yaliyonistaajabisha hapo mwanzo.

Nilimsogelea kijana yule na kumsaalimia kwa salamu ya kiislamu na akaniitikia kwa upole zaidi. Sikuamini kama ni mtu au ni jini hivyo ikabidi nimuulize vizuri. Bila ya wasi akanijibu kuwa yeye ni mtu wa kawaida tu na ni mtu pekee aliyeokoka na janga liliowapata watu wa eneo lile. Kwa shauku nikamuuliza ni kipi basi kilichowapata watu wa eneo lile. Aliniangalia kwa huzuni kisha akaanza kufuta machozi yake na kunza kunisimulia hadithi ya yaliyotokea eneo lile kama ifuatavyo;-


                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela1 Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 653


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MLEVI MBELE YA SULTANI
Soma Zaidi...

SAFARI YA TATU YA SINBAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA TATU YA SINBAD Siku ile ya pili Sinbad mbeba mizigo alivaa ngup zake safi alizonunua na kijipamba vyema na kuelekea kwenye kikao chao. Soma Zaidi...

Hadithi ya binti wa pili mwimba mashairi mwenye makovu
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi ya chongo watatu wa mfalme na wanawake wa Baghdad
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

HADITHI YA MWEN YEKUTABIRIWA MTOTO WA TAJIRI
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITI YA MWENYE KUTABIRIWA MTOTO WA TAJIRI Kwanza tambua ewe ndugu yangu kuwa mimi ni mtoto wa tajiri mkubwa sana katika nchi yetu hii. Soma Zaidi...

Hadithi za Sinbad
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Binti wa ndotoni
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Safari ya kwanza ya sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Hadithi ya mvuvi na jini
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

HADITHI ZA SINBAD
Soma Zaidi...

Hadithi ya mzee wa tatu na mbwa wake mwekundu
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Kitabu Cha hadithi ya wanawake watatu
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...