Hadhi na Haki za Mwanamke katika jamii mbalimbali hapo zamani
Utangulizi:Uislamu unamuelekeza mwanaadamu namna nzuri ya kuendesha maisha yake katika kila kipengele cha maisha akiwa binafsi, katika familia na katika jamii.
Utangulizi:
Uislamu unamuelekeza mwanaadamu namna nzuri ya kuendesha maisha yake katika kila kipengele cha maisha akiwa binafsi, katika familia na katika jamii. Mfumo huu wa Uislamu, kwa kuwa umeasisiwa na Allah (s.w), Aliye Mjuzi Mwenye Hekima, ndio pekee uanomuelekeza mwanadamu kujenga familia imara iliyosimamishwa juu ya msingi wa haki na uadilifu. Hivyo utaona katika jamii zote za Ulmwengu, ni jamii ya Kiislamu pekee inayompa mwanamke hadhi na haki zake zote anazostahiki. Kinyume chake jamii nyingine zote zilizobakia, za kale na za sasa, zimemyanyasa na kumdumisha mwanamke kwa kiasi kikubwa.
Sura hii, ili kuonesha kwa uwazi ubora wa mfumo wa Kiislamu katika kumpa mwanamke hadhi na haki zake zote anazostahiki, ukilinganisha na mifumo ya maisha ya kijahili, tumeigawanya katika sehemu mbili:
Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii za kijahili, Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii ya Kiislamu.
Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii za Kijahili
Hivi leo duniani kote, suala Ia hadhi na haki za mwanamke katika jamii linaongelewa katika kumbi mbali mbali za kitaifa na kimataifa. Pametokea makundi ya harakati ya kitaifa na kimataifa ya kutetea hadhi na haki za wanawake ziliziporwa na wanaume. Swali Ia kujiuliza ni; Je, jitihada hizi zimefanikiwa au zinaonyesha kuleta mafanikio yoyote hapo baadaye? Jibu Ia swali hili tutalipata baada ya kupitia mifano michache ya kihistoria inayoonesha jinsi mwanamke alivyo nyanyaswa na kudunishwa na jamii mbali mbali za kijahili na hatua zilizochukuliwa na jamii hizo ili kumkomboa. Katika sehemu hii tutazipitia jamii zifuatazo:
1.Jamii za Magharibi.
2.Jamii za Mashariki.
3.Jamii za Kiafrika.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawa mirathi
Haya ni mamno muhimu yanayozingatiwa kabla ya kuanza zoezi la kugawa mirathi ya marehemu.
Soma Zaidi...Maneno mazuri mbele ya mwenyezi Mungu
kuna adhkari nyingi sana ambazo Mtume wa Allah ametutaka tuwe tunadumu nazo. lajkini kuna adhkari ambayo imekusanya maneno matukufu na yanayopendwa sana na Allah.
Soma Zaidi...Jinsi ya kumuandaa maiti baada ya kufa
Haya ni maandalizi ya kumuandaa maiti baada ya kufariki.
Soma Zaidi...