Kuanzishwa Ufalme.
Kuanzishwa Ufalme.
Muawiyah kwa kumrithisha mtoto wake, Yazid, uongozi wa Dola, bila kuzingatia utaratibu wa kuchangua viongozi kutokana na sifa stahiki, alivunja maongozi ya Kiislamu na kuasisi utawala wa kifalme au utawala wa kiukoo ambao mpaka leo unaendelezwa katika nchi nyingi za Arabia(Bara Arab), Saud Arabia ikiwa miongoni.
Dola ya kifalme aliyoiasisi Muawiya ilitafautiana na Dola ya Kiislamu aliyoiasisi Mtume(s.a.w) na kuendelezwa na Makhalifa wanne waongofu, Abubakar, βUmar, Uthman na Ali, kwa sababu:
(i) Taasisi ya shura ilivyunjwa na raia walipokonywa uhuru wao wa kutoa maoni na kukosoa viongozi
(ii) Hazina ya Dola β Baitul-Mali, ilifanywa mali ya nyumba ya mfalme ambapo mfalme aliitumia atakavyo kwa maslahi yake binafsi na familia ya kifalme.
(iii)Tabia za kijahili za majivuno ya kikabila na nasaba ziliibuka na kustawishwa na ufalme.
(iv)Watawala (viongozi mbali mbali wa dola) walianza kuishi kwenye mahekalu na nyumba za kifahari za Kifalme.
(v) Suala la kutenganisha maongozi ya Serikali na Dini liliibuka.Masheikh wazuri waliokuwa waadilifu walitengwa na kundi la watawala. Wao wakawa wanajitahidi kuirekebisha jamii lakini wakiwa ndani ya kuta nne za msikiti na nje ya vyombo vya dola.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
(i) Tujitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuondoa maovu katika jamii kwa mikono yetu na ikiwa hatuwezi tuyakemee kama alivyofanya Nabii Lut(a.
Soma Zaidi...KUANGAMIZWA KWA JESHI LA TEMBOTukio la pili ni lile tukio la tembo, na ilikuwa hivi:- Kiongozi mmoja wa kiyemeni aliyetambulika kwa jina la Abrah aliona waarabu kutoka maeneo mbalimbali wanafunga misafara kuelekea Makkah kwa lengo la kwenda kuhiji.
Soma Zaidi...KUKUTANA NA BAHIRA (MTAWA) WA KIYAHUDIMzee Abu talib alikuwa ni mfanya biashara, hivyoslikuwa akimchukuwa kijana wake kwenda kwenye biashara.
Soma Zaidi...Baada ya kupigwa kura juu ya nani awe mlezi wa Maryam, Nabii Zakaria akachaguliwa kuwa mlezi wa Maryam.
Soma Zaidi...Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mtume Ilyasa ni mmoja wa Mitume waliotumwa kupitia kizazi cha Bani Israil.
Soma Zaidi...