Bonoclass ni muunganiko wa maneno mawili, kutoka katika lugha mbili yaani lugha ya kiingereza na lugha ya kiswahili.
Bonoclass ni muunganiko wa maneno mawili, kutoka katika lugha mbili yaani lugha ya kiingereza na lugha ya kiswahili. Maneno hayo ni “bongo” kutoka katika lugha ya kiswahili na “class” kutoka katika lugha ya kiingereza. Neno “bongo” maana yake kwa lugha ya kiswahili ni ubongo, akili au maarifa. Na neno class katika lugha ya kiingereza ni darasa. Muunganiko wa maneno haya mawili ndipo tunapata bongoclass.
Kilugha kama tulivyoona hapo juu bongoclass ni darasa la kutumia akili na maarifa. Kulingana na malengo ya tovuti hii neno bongoclass lina maana kuu zifuatazo:
1.Bongoclass ni darasa la kutumia akili na maarifa
2.Ni darasa linaloshirikisha akili na maarifa kutoka watu mbalimbali
3.Bongoclass ni darasa la kutumia akili na maarifa katuka kutatua matatizo na changamoto
4.Bongoclass ni darasa la kutumia maarifa katika kuingiza kipato
5.Bongoclass ni darasa la kutumia akili na maarifa katika kutumia fursa zilizopo.
Kama utachanganya maana zilizopo hapo juu kwa pamoja unaweza kupata maana halisi ya bongoclass kwa mujibu wa tovuti hii. Kwa hivyo tunasema kuwa:-
Bongoclass ni darasa la kushiriika akili na maarifa kutoka kwa watu mbalimbali katika kutumia fursa zilizopo ili kuzalisha kipato na kuleta maendeleo katika jamii.
Hiyo ndiyo maana halisi ya bongoclass kwa mujibu wa tovuti hii. Maana hii itaendelea kutumika kwenye blog zetu nyingine na kwenye huduma zetu nyingine. Bongoclass tunashirikiana na wadau mblimbali na lengo letu kuu ni kuleta maendeleo katika jamii kwa kiasi tutakachoweza.
Tunatumia jina hili katika social media kama bongoclass kwenye facebook, instagram, twitter na youtube. Tutaendelea kutumia jina hili katika maeneo yeyote ambayo huduma zetu zitaweza kupatikana. Ukiwa na maoni ama mapendekezo na maswali wasiliana nasi kwa mawasiliano yetu. Bofya hapa kupata mawasiliano
Kama maelezo ya hapo juu yanavyojieleza yenyewe kuwa tunatowa huduma ya kielimu katika jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Na huduma hii inatolewa bure bila hata ya malipo yeyote. Kwa ufupi wa maneno zifuatazo ndizo huduma ambazo bongoclass inatoa:-
Kutoa elimu katika jamii kuhusu maswala yote ya afya, afya ya uzazi na mlo kamili, elimu ya dini, elimu kuhusu matumizi ya sayansi na teknolojia, elimu kuhusu sayansi ya viumbe na kilimo, pia tunatoa msaada kwa wanafunzi wa mashuleni. Mwisho tunatoa elimu inayochangamsha akili kama game, maswali na nahau, methali na vitendawili bila kusahau chemshabongo.
Tunatoa burudani kwa watu wa rika zote. Burudani tunayotoa ni utunzi wa hadithi tamu na murua zinazoweza kusomwa na watu wa rika zote. Bila kusahau chemshabongo ambazo huburudisha na kuchangamsha akili. Tunakupatia game rahisi kuzicheza.
Tunaunga, kutengeneza na kusambaza vitabu kupitia tovuti yetu na blog yetu. Vitabu hivi ni vya bure. Ni vijijarida vidogo vilivyokusanya mada zihusuzo afya, dini na burudni. Unaweza kudownload moja kwa moja ndani ya tovuti hii bila hata malipo.
Tunatengeneza tovuti na kuboresha, tunafungua blog na kuziporesha. Hapa tunalenga kuwasaidia mablogger walio wachanga katika ujuzi huu. Lengo letu ni kusaidia maendeleo ya sayansi na teknolojia yaweze kufika mbali kwa kutumia lugha ya kiswahili.
Tunatengeneza App za android. Hii ni kwa ajili ya bishara. Hapa tunakwenda kuwasaidia wafanyabiashara kuweza kufikia malengo yao ya kukuza majina yao, kampuni na kuwafikia walengwa kwa urahisi kabisa kupitia simu za mkononi.
Tunatangaza matangazo mbalimbali katika blog na tovuti yetu. Ukiwa wewe ni mfanyabishara na unataka biashara yako ifikie mamia maelfu ya watu. Bongoclass ndio sehemu sahihi kwako. Tutakutangazia biashara yak na utaweza kufikia walengwa wako kwa urahisi zaidi.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Unaweza kuwasiliana nasi kwenye mitandao ya kijamii, kwa kutumia jina la Bongclass.
Soma Zaidi...Hapa utakwenda kujifunza namna ambavyo ukoloni uliingia Tanzania na vipindi vyake. Utajifunza hatuwa ambazo ukoloni uliweza kupiti na hatimay kuitawala Tanzania
Soma Zaidi...MAAJABU YA VIUMBE Dunia ina maajabu sana lakini viumbe wana maajabu pia.
Soma Zaidi...Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.
Soma Zaidi...Bila shaka umekuwa ukijiuliza sana kuhusu wiki bongo hasa ni kitu gani. Hapa upo mahala sahihi. nitakwenda kukueleza hasa ni nini maana ya hili neno "wikibongo".
Soma Zaidi...VITABU: Karibu kwenye Maktaba yetu ya vitabu, hapa utaweza kusoma na kudownload vitabu vyetu bure.
Soma Zaidi...