image

swala ya witri na namna ya kuiswali

3.

swala ya witri na namna ya kuiswali

3. Swala ya Witri
Witri maana yake ni namba isiyogawanyika kwa mbili kama vile 1, 3, 5, 7, 9, 11 n.k. Sunnah ya witri huswaliwa katika kipindi cha usiku baada ya swala ya Al-Isha na kabla ya kuingia swala ya Al-Fajiri. Lakini ni bora kuichelewesha Witri na kuiswali katika theluthi ya mwisho ya usiku, baada ya swala ya kisimamo (tahajjud).



Mtume (s.a.w) alikuwa akiswali Witri pamoja na swala ya Tahajjud (Swala ya Usiku) na wakati mwingine alikuwa akiswali Witri mara tu baada ya Al-Ishaai. Ni vema kuswali witri baada ya al-Isha kama hakuna uhakika wa kuamka Usiku. Mtume (s.a.w) ameikokoteza sana swala ya Witri kama tunavyojifunza katika hadithi ifuatayo:



Buraydah (r.a) amesimulia, Nimemsikia Mtume (s.a.w) akisema; Witri ni haq (wajibu). Asiyeswali si miongoni mwetu. Witri ni wajibu”. (Abu Da udi)



Witri ina swaliwa kwa rakaa tatu. Huswaliwa kwa rakaa mbili na kutoa Salaam, kisha hukamilishwa na rakaa moja.



Namna ya Kuswali Swala ya Witri
1. Katika rakaa ya kwanza utasoma Sura ya Al-A’alaa (Sabbihisma) baada ya Suratul-Faatiha.


Katika rakaa ya pill utasoma Suratul-Kaafiruuna baada ya suratul-faatiha..



Katika rakaa moja ya mwisho. baada ya kusoma Suratul-Faatiha, utasoma Suratul- lkhlas, AI-Falaq na An-naas. Kuleta Qunut (dua) katika rakaa ya mwisho katika ltidali.


Dua tunayoileta katika Qunut ni hii ifuatayo:


Allahumma ihdidaa fii man hadaita "Ewe Mola n[ongoze kama wale uliouxiongoza"



Wa `aafinaa fiiman `aafaita "Na unininusuru kama hao uliowarursuru"



Watawallanii fiiman tawaffaita "Na unitawalishe pamoja na wale ulio watawalisha



wabaarik lii fii maa a'atwaitanii "Na unitilie pataka katika vile ulivyonipa



Waqinii sharra maa gadhwaita "Unikinge na shari ulizonikadiria"


Tabaarakta rabbanaa wata’aalaita "Ni nyingi kabisa juu yetu baraka zako na umetukuka kweli kweli"


Ni muafaka kuleta dua nyinginezo vile vile kulingana na haja ya mwenye kuswali.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1712


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-