Sababu za mdomo kuwa mchungu

Hapa utajifunza sababu zinzopelekea mdomo kubadilika ladha na kuwa mchungu, ama mchachu.

Sababu za mdomo kuwa mchungu

KWA NINI MDOMO UNAKUWA MCHUNGU?
Umeshawahi kuamka asubuhi ukiwa na ladha chungu sana ya mdomo, na je hali hii ulishawahi kudumu nayo kwa muda wa masaa kadhaa?. bila shaka ungependa kujuwa sababu inayopelekea kutkea hali hii. Makala hii ni kwa ajili yako. Hapa nitakujuza sababu kuu za kuwa na ladha chungu ya mdomo, na nini kifanyike. Endelea kusoma makala hii hadi mwisho. Ila ningependa utambuwe kuwa mdomo kuwa mchungu mara nyingi sio shida sana ya kiafya kiasi cha kuhitaji dawa ama kumuona daktari. Endapo shida itaendelea hapo fanya maamuzi ya kuonana na daktari



Mdomo kuwa mchungu mara nyingi sio maradhi. Hali hii hutokea na kuondoka yenyewe ndani ya masaa machache. Mara nyingi hutokea wakati wa asubuhi ama unapotoka kulala. Hali hii pia huwapata wagonjwa. Hali hii wakati mwingine inakuwa ni dalili ya maradhi. Kama utaona mdomo wako unaendelea kuwa mchungu kwa muda mrefu onana na daktari kwa uchunguzi zaidi.



Ni nini husababisha mdomo kuwa mchungu?
1.Mdomo kutokuwa msafi. Hii ni kawaida wakati umelala mdomo bakteria waliokuwa wapo mdomoni wanaendelea kufanya kazi yao, kula mabaki ya chakula na kuendelea kuzaliana. Kumbuka mate yana kazi ya kusafisha mdomo,lakini wakati umelala mate hayawezi kufanya kazi hii kwani huwezi kuyatoa. Hivyo uchafu huendelea kujizalisha bila ya kutolewa. Hali hii inaweza kusababisha mdomo kuwa mchungu unapoamka.



Vyema usile kitu muda huu, kabla ya kupiga msaki. Safisha kinywa vyema ladha ya mdomo itarudi sawa ndani ya muda mchache. Pia kama ulitoka kulala baada ya kutema mate kwa muda mchache yaani baada ya mdomo kujisafisha hali hii inaweza kuondoka bila ya wasi wala hakuna ulazima wa kupiga mswaki, kwani mdomo una sifa ya kujisafish awenyewe kwa kutumia mate.




2.Matumizi ya madawa ya antibiotics au antidepressants. Dawa hizi pindi mdu anapozitumia hufyonzwa ndani ya mwili na kutolewa kwa kupitia mate na kusababisha mate kuwa machungu. Mfano wa dawa hizi ni:-
A. Tetracycline
B.Gout medication kama allopurinol na lithium
C.Madawa yanayotumika kutibu maradhi ya moyo.

Baada ya kuacha kutumia dawa hizi ladha ya mdomo itarudi sawa ndani ya siku chache. Pia unaweza kunywa juisi ya vitu vichachu kama hali itaendelea kukusumbuwa.



3.Ujauzito, hali ya mdomo kuwa mchungu ama kuwa na ladha ya chuma kwa wajawazito ni kawaida na hali hii kutaalamu hufahamika kama dysgeusia ama metallic taste. Hutokea kwa uda wa siku kadhaa kisha huondoka. Baadhi ya wajawazito wanapata ladha ya pesa, yaani kama ulishawahi kuweka mdomon hela ya sarafu, ile ladha unayoipata ndio ambayo huwapata baadhi ya wajawazito.



4.Kama unatumia dawa za kuongeza vitamini, unaweza kupata ladha hii. Kuna baadhi ya dawa za vitamini zina madini mengi ya metali. Madini hayokama zinc, shaba, chuma na chromium. Kama dawa hiyo ina madini haya inaweza kubadili ladha ya mdomo na kuwa chungu



5.Ni dalili ya maradhi ya ini. Kama ini lako halifanyi kazi vyema ama lina matatzo, mwili utakuwa na kiasikikubwa cha ammonia ambayo ni sumu. Hatimaye kubadili ladha ya mdomo.



6.Mashambulizi ya kwenye mfumo wa upumuaji. Wakati mfumo wa upumuaji unapokuwa katika mashambulizi ya bakteria ama virusi au fangasi, inaweza kuathiri ladha ya mdomo.



7.Kama umecheuwa, hali hii inaweza kupelekea kubadilika kwa ladha ya mdomo



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2062

Post zifazofanana:-

Kuwa mwenye Kumtegemea Allah
35. Soma Zaidi...

Dalili za UKIMWI huonekana baada ya muda gani
Hapa utajifunza muda mabao dalili za VVU na UKIMWI huonekana, na kwa muda gani mgonjwa ataishi na UKIMWI bila ya kutumia ARV Soma Zaidi...

dondoo za afya
Basi tambua haya;- 1. Soma Zaidi...

Nguzo 6 za iman ya dini ya kiislamu kwa mafundisho ya quran na sunnah
Nguzo za Imani. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Nanasi
Soma Zaidi...

Sifa za wanafiki katika quran
Soma Zaidi...

Historia ya Dhulqarnain
Dhulqarnain sio jina la mtu bali cheo, maana yake ikiwa: 'Mwenye Pembe Mbili'. Soma Zaidi...

TEKNOLOJIA NA MAWASILIANO
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula papai
Soma Zaidi...

Historia na asili ya kuzibiti uzazi na uzazi wa mpango
Soma Zaidi...

Hadhi na Haki za Mwanamke Katika Jamii
Soma Zaidi...

NUHU(A.S) NA WATU WAKE NA UOVU WALIOKUWA WAKIUFANYA WATU WAKE
Mtume aliyemfuatia Nabii Idrisa(a. Soma Zaidi...