Katika somo hili tutaenda kujifunza jinsi ya kusoma (Read) data kutoka kwenye database yetu
Somo la 5 Python Sqlite: Jinsi ya kusoma (Read) data kutoka kwenye database
Kusoma (Read) data kutoka kwenye database ni hatua muhimu sana. Hapa ndipo tunapata faida halisi ya kuhifadhi taarifa zetu. Leo, tutajifunza jinsi ya kuunda faili la read.py na kuelewa kila mstari wa msimbo wake.
Fungua Text Editor (kama vile VS Code au Sublime Text), kisha uunde faili jipya na uli save kama read.py kwenye eneo lile lile ambalo faili za db_conn.py na insert.py zilipo. Kisha,uingize code zifuatazo.
Mfano:
read.py
Sasa hebu tuchambue code zetu ili kuelewa kila mstari unamaanisha nini.
import db_conn as dbConn: Hii ni amri ya kuingiza moduli (module) yetu ya db_conn ambayo ina kazi ya kuunganisha na database. Tunaifupisha iwe dbConn ili iwe rahisi kuitumia.
def ReadData():: Hii inaanza kazi (function) inayoitwa ReadData. Kazi yake ni kusoma taarifa zote kutoka kwenye database.
connection = dbConn.get_connection(): Hapa, tunaita kazi ya get_connection() kutoka kwenye faili la db_conn.py ili kupata muunganiko na database yetu.
cursor = connection.cursor(): Tunapata cursor yetu. Kumbuka, cursor ndiye mtendaji au mtaalamu wa kutekeleza amri za SQL.
query = "SELECT * FROM products": Hii ndiyo amri muhimu ya SQL.
SELECT: Hii inaambia database "chagua" au "soma" data.
*: Nyota (*) inamaanisha "safu zote" au "habari zote". Hivyo, tunaiambia "chagua taarifa zote kutoka kwenye safu zote".
FROM products: Hii inaeleza meza gani tunayotaka kuchukua data kutoka. Katika kesi hii, ni meza ya products.
cursor.execute(query): Hapa tunamwambia cursor "tekeleza" amri yetu ya SELECT.
results = cursor.fetchall(): Hii ndiyo sehemu inayochukua matokeo ya amri. fetchall() inaweka taarifa zote zilizopatikana kwenye query yetu na kuzihifadhi kwenye variable inayoitwa results kama orodha (list) ya tuples.
for Endex, result in enumerate(results, 1):: Hii ni kitanzi (loop) ambacho hupitia kila mstari (result) kwenye orodha yetu ya results. enumerate() inatusaidia kuhesabu kila mstari unaopitiwa, kuanzia namba 1 (kwa sababu ya 1 mwishoni).
Id, name, taken, quantity, location, price = result: Hii inachukua data kutoka kwenye kila mstari (tuple) na kuigawa kwenye variable tofauti. Kwa mfano, thamani ya kwanza inaenda kwenye Id, ya pili kwenye name, na kadhalika.
print(...): Hapa ndipo matokeo yanavyoonyeshwa kwa lugha inayoeleweka. Tumetumia f-string (format string) kuweka variable ndani ya maandishi. price:,} husaidia kuweka alama ya mkato (comma) kwenye bei ili iwe rahisi kusoma, mfano 1,000,000.
ReadData(): Mwishowe, tunaiita kazi yetu ya ReadData() ili ianze kufanya kazi.
Baada ya kuiita function yetu ya ReadData() tuta run kwenye terminal yetu na sasa tutaweza kusoma vyema data zetu kutoka kwenye database.
VIDEO TUTORIAL: 👇
MWISHO:
Katika somo litakalofuata tutaenda kujifunza zaidi jinsi ya ku sasisha (Update) taarifa zetu kutoka kwenye database
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Katika Somo hili la nane utaenda kujifunza namna ya kuchambua data kwenye database yetu kwa kupata jumla ya kiasi cha fedha kilichokopwa
Soma Zaidi...Katika somo hili tutajifunza utangulizi wa SQLITE na jinsi ya kuitumia katika python
Soma Zaidi...Katika somo hili utaenda kujifunza namna ya kuunganisha mafaili mengi ya project na kuyaweka kwenye faili moja tu na kuweza kufikia faili zote kwa kupitia faili moja pekee
Soma Zaidi...Karibu ujifunze Python Sqlite na muunganiko wa Database (Database Connection)
Soma Zaidi...Karibu kwenye somo la sita! Leo tunajifunza UPDATE, amri ambayo inaruhusu kubadili au kusasisha data iliyopo tayari kwenye meza (table) yetu.Â
Soma Zaidi...Katita somo hili sasa tutaenda kujifunza namna ya kuunda table kwenye database ya SQLITE kwa kutumia Python
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuingiza data kwenye table na database tuliyoiunda katika somo lililopita
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza namna bora ya kufuta data kutoka kwenye database
Soma Zaidi...