Katita somo hili sasa tutaenda kujifunza namna ya kuunda table kwenye database ya SQLITE kwa kutumia Python
Somo la 3 python sqlite: Jinsi ya kuunda table kwenye database ya SQLITE na Python
Baada ya kujua jinsi ya kuunda database, hatua inayofuata ni kuunda meza (table) ndani yake. Fikiria database kama faili la kuhifadhia (file cabinet), na meza ndiyo droo unayoweka data yako. Kila droo ina sehemu zake maalum za kuandikia vitu, ambazo tunaziita safu (columns).
CREATE TABLE IF NOT EXISTS products: Hii ndio amri inayoanzisha uundaji wa meza.
CREATE TABLE inaiambia database "tengeneza meza".
IF NOT EXISTS inahakikisha kwamba kama meza ya products tayari ipo, amri hii itapuuzwa na hakuna kosa (error) litatokea. Hii ni njia nzuri ya kuzuia makosa unaporun msimbo mara nyingi.
products ni jina la meza yetu.
Ndani ya mabano (...), unaeleza muundo wa meza yako, ukiorodhesha kila safu (column) na aina ya data (data type) itakayoifadhiwa.
id INTEGER PRIMARY KEY AUTOINCREMENT: Hii ndio safu ya kwanza, ya id.
INTEGER ni aina ya data inayohifadhi namba kamili.
PRIMARY KEY inamaanisha id ni kitambulisho cha kipekee kwa kila mstari (row) katika meza. Hakuna mistari miwili inayoweza kuwa na id sawa.
AUTOINCREMENT inamaanisha id itajiongeza yenyewe kwa namba moja kila unapoongeza bidhaa mpya. Huwezi kuiandika mwenyewe.
name TEXT: Hii ni safu ya kuhifadhi jina la bidhaa. TEXT inaashiria kuwa data itakuwa maandishi (k.m., "Simu," "Laptop").
taken_by TEXT: Safu ya kuhifadhi jina la mtu aliyechukua bidhaa. Aina ya data ni TEXT.
quantity REAL: Hii inahifadhi idadi ya bidhaa kama namba kamili au desimali mfano (0.5). Aina ya data ni REAL Kwani inapokea flot points.
location TEXT: Safu ya kuhifadhi eneo la bidhaa kama maandishi. Aina ya data ni TEXT.
price INTEGER: Hii inahifadhi bei ya bidhaa kama namba kamili. Aina ya data ni INTEGER.
SQLite inasaidia aina tano za data, ambazo zinatumika kufafanua ni aina gani ya habari itakayohifadhiwa kwenye kila safu.
NULL: Hii inaashiria kwamba thamani ya safu ni haipo au ni batili.
REAL: Hii inahifadhi namba za desimali (decimal numbers). Kwa mfano, 3.14, 25.5. Ungeitumia kwa bei au hesabu zinazohitaji desimali.
BLOB: Hii inasimama kwa "Binary Large Object." Inatumika kuhifadhi data ya binary kama vile picha, sauti, au faili zingine. Data hii haisomeki kama maandishi.
VIDEO TUTORIAL: 👇
MWISHO:
Katita somo linalofuata tutaenda kujifunza jinsi ya kuweka data kwenye table ndani ya database
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili tutaenda kujifunza jinsi ya kusoma (Read) data kutoka kwenye database yetu
Soma Zaidi...Katika somo hili tutajifunza utangulizi wa SQLITE na jinsi ya kuitumia katika python
Soma Zaidi...Katika Somo hili la nane utaenda kujifunza namna ya kuchambua data kwenye database yetu kwa kupata jumla ya kiasi cha fedha kilichokopwa
Soma Zaidi...Karibu kwenye somo la sita! Leo tunajifunza UPDATE, amri ambayo inaruhusu kubadili au kusasisha data iliyopo tayari kwenye meza (table) yetu.Â
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuingiza data kwenye table na database tuliyoiunda katika somo lililopita
Soma Zaidi...Katika somo hili utaenda kujifunza namna ya kuunganisha mafaili mengi ya project na kuyaweka kwenye faili moja tu na kuweza kufikia faili zote kwa kupitia faili moja pekee
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza namna bora ya kufuta data kutoka kwenye database
Soma Zaidi...Karibu ujifunze Python Sqlite na muunganiko wa Database (Database Connection)
Soma Zaidi...