Katika somo hili tutajifunza utangulizi wa SQLITE na jinsi ya kuitumia katika python
Somo la 1: Utangulizi wa SQLITE na jinsi ya kuitumia katika python
SQLite ni database engine ambayo inapatikana kama library moja tu. Huwezi kuhitaji ku-install database server yoyote tofauti. Badala yake, database nzima inahifadhiwa kwenye faili moja kwenye kompyuta yako. Hii inafanya iwe rahisi sana kuanza nayo kwa sababu hakuna setup ya ziada inayohitajika.
Faida: Ni ndogo, inafanya kazi haraka, na ni rahisi kutumia. Inakuja pamoja na Python, hivyo huna haja ya kui-download tena.
Matumizi: Inafaa sana kwa ajili ya programu ndogo ndogo za desktop, mobile apps, na kwa kujifunzia.
Lengo: Amri ya import sqlite3 inaiambia Python iandae moduli (module) ya sqlite3 ili tuweze kuitumia kuwasiliana na database yetu ya SQLite. Fikiria kama unafungua sanduku la vifaa ambalo lina zana zote za kufanya kazi na database.
Moduli hii ina kazi mbili kuu utakazozitumia mara kwa mara:
sqlite3.connect('jina_la_db.db'): Hii ndio kazi ya kwanza kabisa utakayotumia. Inafanya muunganiko (connection) na database.
Ikiwa faili ya jina_la_db.db haipo, Python inaiunda moja kwa moja.
Ikiwa faili ipo, Python inaifungua na kuungana nayo.
Kutoka hapa, unaunda object inayoitwa conn (mfano wa connection) ambayo ndiyo utatumia kufanya kazi nyingine zote.
conn.cursor(): Cursor ni kama pointer au mshale unaotumika kutekeleza amri za SQL kwenye database. Baada ya kuunda connection, unatumia amri hii kupata cursor na kuanza kufanya shughuli kama vile kuunda meza (tables), kuongeza data (INSERT), au kusoma data (SELECT).
Muhimu:
Katika subtopic hii ya PYTHON na SQLITE tutajifunza kwa vitendo zaidi ili kuimarisha ujuzi wetu. Vitendo vya kujifunza tutajikita kwenye kuunda CRUD rahisi (CREATE, READ, UPDATE and DELETE) Kwani ndio msingi wa programming yoyote katika ulimwengu wa coding.
Mwisho:
Somo litakalofuata tutasoma kwa undani zaidi ni kwa namna gani tunaweza kuanza kuitumia Sqlite kwenye python.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Karibu kwenye somo la sita! Leo tunajifunza UPDATE, amri ambayo inaruhusu kubadili au kusasisha data iliyopo tayari kwenye meza (table) yetu.Â
Soma Zaidi...Katika somo hili tutaenda kujifunza jinsi ya kusoma (Read) data kutoka kwenye database yetu
Soma Zaidi...Katita somo hili sasa tutaenda kujifunza namna ya kuunda table kwenye database ya SQLITE kwa kutumia Python
Soma Zaidi...Katika somo hili utaenda kujifunza namna ya kuunganisha mafaili mengi ya project na kuyaweka kwenye faili moja tu na kuweza kufikia faili zote kwa kupitia faili moja pekee
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuingiza data kwenye table na database tuliyoiunda katika somo lililopita
Soma Zaidi...Katika Somo hili la nane utaenda kujifunza namna ya kuchambua data kwenye database yetu kwa kupata jumla ya kiasi cha fedha kilichokopwa
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza namna bora ya kufuta data kutoka kwenye database
Soma Zaidi...Karibu ujifunze Python Sqlite na muunganiko wa Database (Database Connection)
Soma Zaidi...