Navigation Menu



image

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 1: Hadithi ya chongo watatu, watoto wa mfalme na wanawake wa Baghdad.

Skmulizii hii pia imetoka kitabu cha kwanza cha HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza

CHONGO WATATU WATOTO WA WAFALME NA WANAWAKE WA BAGHDAD

 

Hapo zamani katika nchi ya Baghdad kulikuwepo na mbeba mizigo maarufu sana. Alikuwa ni kijana asiyepunguwa miaka 40, na alisifika kwa nguvu na akili sana na uwezo wa kufikiri alio nao. Alipendwa sana na watu na aliheshimika pia. Siku moja laikuwa amekaa eneo lake la kila siku kusubiri wateja, ghafla akatokea binti mmoja mrefu wa kiarabu. Binti huyu alimfanya mbeba mizigo amtazame sana kwa muda mrefu kwa uzuri alonao binti huyu. Binti akamwambia yule kijana nifate. Kwa haraka zaidi kijana akanyanyuka na kuanza kufata.

 

Wakafika kwenye nyumba moja yule binti akagonga mlango kwa madaha, mzee mmoja akatoka, binti akatia mkono kwenye mkoba wake na kutoa pesa nyingi na akampa yule mzee. Bila ya kuzungumza mzee alijiwa kinachotakiwa aliingia ndani na akaja na chupa kubwa lililojaa pombe. Kijana akabeba mzigo ule na kuuweka kwenye kapu lake kubwa la kubebea mizigo. Wakaelekea kwenye duka la matunda, hapa wakanunua matunda ya aina nyingi sana. Kisha wakafika duka lingine wakanunua vitu vingi sana vya harufu nzuri. Kwa urembo alonao huyu binti unaweza kufikiri ni vitu gani vya harufu nzuri angechukuwa. Kijana akamwambia “binti bora ungenambia toka mapema kama una mizigo mingi ili nichukuwe punda ama ngamia”. Binti akaheka sana na akamwambia “sijamaliza bado”.

 

Mambo yakawa hivyo waliendelea kununua vitu vingi katika matunda na vyakula na vinywaji. Vitu vya kunukia maua, mafuta pafyumu nna vinginevyo viingi. Wakafika kwenye nyumba mija mzuri sana, yule binti akaenda kuginja kwa madaha na upole zaidi kwenye malngo wa geti la nyumba hivyo. Muda wote kijana alikuwa akifurahia uwepo wa binti huyu na kila analofanya. Basi akatoka binti mwingine wa makamo aliyeonekana mzuri zaidi kuliko huyu na akafungua mlango.

 

Muda wote kijana alikuwa akishangaa na macho yake yaliganda kwa hutu mfungua mlango. Baada ya muda yule binti akamwambia “tafadhali ingia ndani”. Hapa kijana fahamu zikamrejea kwa shauku akaingia ndani. Alishangaa sana uzuri ulioje wa ndani pale. Nyumba yenye kila kizuri anachokijuwa na ambavyo ndo alianza kuviona. Kuna vinyago vya dhahabu na chemchem za maji. Meza yz almasi na sakafu yenye marumaru za kuvutia zaidi.

 

Kila kilichopo ndani hapa kilimflaisha kijana, ila zaidi ya hapo kilichomshangaza zaidi pale ndani kuna kiti kikubwa na zizuri. Aliyekaa kwenye kiti kile alikuwa ni dada mmoja mzuri sana huenda aliwashinda wote pale ndani. Kijana alifikiri yule ndo mkubwa wao, na huu ndo ukweli. Yule aliitwa Zubeida na yule alokuja nae kutoka kwenye bidhaa ni Sadie na yule alofungua mlango aliitwa Amina. Basi amina aliingiza mizigo ndani na sadie alitowa kiasi chapesa na kumpatia kijana.

 

Kijana aliendelea kushangaa pale ndani kwa muda mpaka zubeida akauliza “vipi kaka mbona hauondoki? Au unataka pesa zaidi?”. Kijana akaanza kujitetea kuwa angependa kukaa kidogo na akaleta hadithi nyingi na baadae wakamruhusu aendelee kukaa kidogo. Zubeida akamwabia “basi nitakuruhusu kukaa kwa sharti uwe mpole na usitowe siri ya maisha yetu hapa”. Kiana akakubaliana na sharti na akawajibu “nitatunza siri za humu ndani kuliko alivyotunza siri kinyozi wa mfalme”. Kwa shauku Amina akauliza “alifanya nini kinyozi wa mfalme?”. Kijana akamjibu amina “ni hadithi ndefu kidogo”. Akadakia Sadie “tusimulie basi hiyo hadithi ya kinyozi”. Kijana akamuangalia Zubeida aliyekuwa akimuashiria awaridhishe ndugu yake. Basi kijana akaanza kusimulia hadithi kama ifuatavyo;-






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Mankaa Tarehe 2024-09-09 13:38:51 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 86


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 9: Hadithi ya binti wa ndotoni.
Simulizi hii pia inapatikana kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 2: Sehemu ya safari ya kwanza ya sinbad
Muendelezo wa stori ya safari ya Sinbad ambayo ipo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 3 Part 4: Kisa cha waziri aliyeadhibiwa
Simulizii hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 15: Mji uliogeuzwa mawe
Hadithi hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part24 : Kaka wa tatu wa kinyozi
Muendelezo Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 10 Part 4: Ndoa ya kwanza
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 3 Part 6: Simulizi ya samaki wa rangi nne
Simulizi za HALIF LELA U LELA zipo nyingi na zinasisimua.. kisa hiki cha samaku wa rangi nne kipo katika kitabu cha kwanza Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 2: Kisa cha kinyozi msiri..
Karibuni tuendelee kusimuliana stori za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza, stori nzuri sana na za kuvutia zimeandaliwa kwaajili ya kujifunza na kujiburudisha pia..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 8: Simulizi ya chongo wa tatu mtoto wa mfalme
Muendelezo wa hadithi ya mtoto wa mfalme mwenye chongo katika hadithi ya HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 7: Upendo uliotafsiriwa
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 10 Part 6: Ndoa ya pili
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 10 Part 7: Taharuki
Muendelezo..... Soma Zaidi...