Simulizi za Hadithi EP 4 Part 9: Hadithi ya binti wa mfalme kufichwa.
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza......
BINTI MWENYE KUFICHWA, MTOTO WA MFALME.
Juwa ewe mwenye kuja kwa jina la Habili kwa cheo cha mchanja kuni kuwa mimi ni mtoto wa mfalme niliyetambulika kwa uzuri na hta mawaziri na watoto wa wafalme wakawa wanagombana kwa kutaka kunipata kuwa mke wao. Ugovi huu ulikuwa mkali hata ukaingiliwa na viumbe visivyo onekana navyo vikataka kunioa nao ni maini waliombali na rehema za Mwenyezi mungu.
Nyumbani kwetu kulikuwana kisima kilichoaminika kuwa ni cha muda mrefu kisichopungua umri wa miaka 150. katika kisima hiki kijana wa kijini alichikuwa madaraka ya kutawala majini waliopo kwenye kisima kile. Siku ile nilikwenda kuchota maji kisimani pale nikiwa kichwa changu kipo wazi kinyume na maamrisho ya dini yetu. Bila ya kutambua unywele wangu mmoja uliangukia kwenyekisima kile na kumganda kiongozi mpya a majini alipokuwa akipewa majukumu.
Nilirudi nikiwa na mabadiliko katika kichwa changu hata ndoo ya maji niliiona n nzito sana kuibeba hivyo nikatumia mikono yangu kubeba maji yale. Siku ile sikupata usingizi kwa maumivu ya kichwa na nilipopata usingizi nilshituka kwa ndoto za kutisha nilizokuwa ninazipata. Sikujuwa chanzo cha matatizo haya yote. Ilipofika asubuhi nilimueleza baba yangu ju ya maumivu ya kichwa changu. Baba alimwita daktari wetu na kuanza kunitibia. Kwa muda wa siku 5 sikupata nafuu zaidi ya maradhi yaliyokuwa yakinizidia.
Kwa muda wa miezi waganga na madaktari wote walishindwa kutibu ugonjwa wangu. Ilifikia hali kuwa mbaya hata nikawa sinafahamu juu ya niayofanya, unaweza kusema nilikuwa mkichaa ambaye akili zinaingia na kutoka. Hali hii ilimpa baba yangu wakati mgumu hata akafikiri ni maradhi yaliyosababishwa na wale wachumba wliokuwa wakinigombania. Habari za ugonjwa wangu zilienea nchi nzima na kila mtaalamu wa tiba alikuja kujaribu bahati yake kwani donge nono liliahidiwa kwa atakayenitibu.
Miezi sita ilifika na habari za ugonjwa wangu zikaenea nchi za majirani. Baba alifikia hatua akatangaza kwa yeyote aatakayenitibu ataniozesha nae. Jambo hili lilisababisha hata wataalamu wa ta kutoka nchi za jirani wa lengo la kunioa pindi wakifanikiwa kunitibu. Bila ya mafanikio yeyote juu ya ugonjwa wangu ijapokuwa wapo walofaniukiwa kunipa nafuu lakini haichukui muda kabla ya ugonjwa kunizidia.
Siku niliota ndoto ya kushangaza. Ndoto hii nilipomwambia baba alijaribu kuwauliza wataalamu wenye kujuwa tafsiri za ndoto. Basi akaja mtaalamu na akaniambia nimueleze ndoto ile bila hata ya kuacha hata sehemu ndogo. Basi nilikaa kimya kwa muda kisha nikakusanya mawazo yangu na kuanza kumuelezea ndoto yangu kama ifuatavyo;-
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 ai web app 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 6: Hadithi ya Ndoa ya siri
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili muendelezo....
Soma Zaidi...Simulizi za Hadithi EP 5 Part 16: Hadithi ya safari ya saba ya Sinbad
Muendelezo wa safari ya Sinbad.......
Soma Zaidi...Simulizi za Hadithi EP 4 Part 12: Hadithi ya mfalme alikuwa kwenye kisima
Wapendwa tuendelee kuoata stori nzuri na za kusisimua kutoka katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.....
Soma Zaidi...Simulizi za Hadithi EP 5 Part 4: Sehemu ya pili ya safari ya Sinbad
Muendelezo wa hadithi ya safari ya Sinbad iliyopo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.....
Soma Zaidi...