Pilipili kali
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za pilipili kali
Pilipili kali.
Watu wengi wamekuwa wakiacha kutumia pilipili etu kwa sababu ya ukali wake. Ila itambulike kuwa ijapokuwa ni kali lakini ila faida nyingi sana kwa afya ya mtu. Pilipili pia ina vitamini c ndani yake kwa kiasi. Vitamini hivi ni muhimu sana katika mfumo mzima wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na wadudu shambulizi.
Pilipili zote zina vitamin A, C na K lakini pilipili nyekundu zimezidi wenzie. Wataalamu wa afya wanazungumza kuwa antioxidant, vitamin A na C vilivyomo kwenye pilipili husaidia katika kuzuia maradhi ya saratani na baadhi ya maradhi yanayohusiana na kuzeheka, na pia husaidia katka kuboresha mfumo wa kinga. Pia vitamin K husaidia katika kuganda kwa damu, kuimarisha mifupa pia husaidia katika kulinda seli.
Pilipili nyekundu ni chanzo kizuri cha carotenoid ambayo hutambulika kama lycopene, hii ni mujarabu sana katika kuzuia mwili kupata maradhi ya saratani ya kibofu, njia ya uzazi kwa kinamama na saratani ya kongosho.pia kuna carotenoid inayotambulika kama cryptoxanthin hii nayo hujulikana kwa uwezo wake wa kupambana na kuzuia mwili kupata saratani ya mapafu inayohusiana na uvutaji wa sigara.
Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa pilipili husaidia katika kurekebisha mapigo ya moyo na kuongeza joto la mwili kwa muda wa dakika 20 baada ya kuila. Hii inaonesha kuwa mwili utakuwa na uwezo wa kuunguza mafuta na cholesteral za ziada kwa muda huo. Pia tafiti nyingine zinaonesha kuwa pilipili husaidia katka kupunguza athari za vidonda vya tumbo kwani husaidia katika kuuwa bakteria ndani ya tumbo.
Ndani ya pilipili kuna antioxidant iitwayo piperine. Wataalamu wa afya wanadai kuwa ulaji wa antioxidant husaidia katika kuimarisha afya ya mtu. Piperine inatambulika kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kudhibiti na kulinda uharibifu wa seli. Pia ulaji wa pilipili husaidia katika kuimarisha afya ya ubongo.
Kwa ufupi pilipili husaidia sana kwa afya ya mlaji. Pia pilipili husaidia katika kuulinda mwili dhidi ya maradhi ya kisukari, saratani na maradhi ya moyo. Afya ya ubongo, kuimarisha mapigo ya moyo pamoja na kupunguza mgando wa mafuta kwenye mirija ya damu. Pilipili husaidia katika kuufanya mwili uweze kunyonya virutubisho muhimu kutoka kwenye chakula.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 web hosting 👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Faida za kula Faida za kula Boga
Makala hii inakwenda kukueleza faida za kula maboga, na mbegu zake kwa afya yako
Soma Zaidi...Faida za kungumanga/nutmeg
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula kungumanga
Soma Zaidi...Zijue Faida ya kula tunda la tango.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Faida za kula tango japokuwa watu wengi hulipuuzia Ila Lina Faida kubwa Sana mwilini.
Soma Zaidi...Kitunguu saumu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kitunguu saumu
Soma Zaidi...Orodha ya madini, chanzo chake na faida zake
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu orodha ya madini chanzo chake na faida zake
Soma Zaidi...