picha

Nani muuaji?

Posti hii inakwenda kukusimulia kuhusu muuaji wa mtoa burudani wa sultan

NANI MUUWAJI?

Mfalme alipoamka alitaka kumuona kijana wake lakini asimuone. Akauliza habari za kijana yule na akaelezwa kuwa amefariki lakini muuwaji hajulikani, mpaka sasa kuna wauwaji wanne na kila mmoja anadai yeye ndio muuwaji halisi. Mfalme akaamrisha wote waitwe na waje mbele yake na amtafute muuwaji halisi wa kijana wake yeye mwenyewe.

 

Mfalme aliogopa sana asije fanya kosa kama lile alolifanya kwenye kesi ya kifo cha mtoto kwenye ndoo ya maji ambapo mtu asiye na hatia aliuliwa. Walinzi wa mfalme wakamuuliza kwani ni kitu gani kilitokea kuhusu kesi ya mtoto huyu. Akawasimulia kwa ufupi habari hii kuwa alikiwepo mama mmoja aliyekuwa na mtoto anayeanza kusimama dede. Pale ndani palikuwepo na mfanya kazi wao. Mtoto yule alizoeshwa kuogeshwa kwenye ndoo ya maji na mama yake a alikuwa akifurahia sana anapotiwa kwenye ndoo ya maji.

 

Siku moja mama yule alipata safari ya ghafla na kumuacha mtoto wake kwa jirani maana mfanyakazi hakuwepo alikwenda kuchota maji mbali kidogo. Mtoto yule akiwa kwa jirani alitoroka na kyurudi kwao. Na kwa kuwa milango ilikuwa wazi aliingia ndani na kukuta ndoo za maji zipo wazi. Mtoto yule akaingia kwenye ndoo zile na kupitiwa na usingizi. Dada mchota maji alipokuja hakuangalia vizuri kwenye ndoo akajaza maji na kuondoka kwa haraka ili akawahi foleni ya maji.

 

Mtoto mule kwenye ndoo alipiga kelele na kayanywa maji zaidi na hatimaye akapoteza maisha. Akaja dada wa kazi na kujaza ndoo ile kisha akaifung bila ya kuangalia nddani. Akazipandanisha ndoo kama tatu. Mama aliporudi alimtafuta mtoto kwa jirani bila ya mafanikio. Juhudi za kumtafuta ziliendelea ndani ya siku tatu bila hata kufanikiwa. Majirani wakamuonea huruma mwenzao na wakaamua kumpikia apate kula, wengine wakaanza kufua nguo zake na kudeki nyumba maana ndani ya siku tatu hakukuwa kukipikwa wala kufagiliwa wala kudekiwa.

 

Maji yalipobakia ndoo moja wakamkuta mtoto amshakufa kwenye maji. Mama yule kwa hasira alimpeleka mfanyakazi wa hakimu na hatimaye mfanyakazi akauliwa kwa kosa la kumuuwa mtoto kwenye maji na kumficha na ndoo. Kumbe mfanya kazi hana hatia maana ni mama aliyemzoesha mwanae kuingia kwenye ndoo na nikosa la jirani kutomuangalia vizuri mtoto. Kosa la mfanyakazi kuweka maji bila ya uangalifu. Hivyo nahofia kesi hii isijekuwa na mfanano na hii. Basi kwa haraka akaagiza waletwe wat wote wanaohusika mbele yake.

 

Watu wote wakapelekwa kwa mfalme pamoja na maiti wao. Falme akaanza kuuliza mmoja mmoja ataje amemuuwa vipi. Hapo mlevi akasema namna ambavyo tukio limetokea, kisha muuza nyama akaeleza tukio lilivyotokea kwa upande wake kisha tabibu kisha mshona nguo. Baada ya kiusikia maelezo ya kushangaza mfalme akaamuru habari hii iandikwe kwa wino wa dhahabu na iwekwe kwenye kumbukumbu za kifalme. Kisaha mfalme akauliza je kuna mwenye hadithi inayoshangaza zaidi ya hii ya kijana wangu huyu? Hapo mlevi akasema yeye ana hadithi ya kushangaza zaidi ya hii. Na akaanza kusimulia kama ifuatavyo;-

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2021-11-07 Topic: Aliflela2 Main: Burudani File: Download PDF Views 2455

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 web hosting    👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina   

Post zinazofanana:

Ndoa ya siri

NDOA YA SIRI YAFANYIKA Hatimaye siku ya ijumaa ikafika na mimi nikaoga nyema na kuchukuwa kanzu iliyo nadhifu zaidi.

Soma Zaidi...
Siku ya sita ya wageni

SIKU YA SITA YA WAGENI Siku ya sita walianza mapema kama siku ya nne kisha wakamueleza baba awapeleke msituni.

Soma Zaidi...
Hadithi ya tunda la tufaha (epo)

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
ALIF LELA U LELA KITABU CHA PILI

Download kitabu Hiki Bofya hapa KITABU CHA PILI HADITHI ZA ALIF LELA U LELA UFUPISHO WA ALIF LELA U LELA KITABU CHA KWANZA.

Soma Zaidi...
Deni la mapenzi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

Soma Zaidi...