Navigation Menu



image

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 7: Mjakazi wa sultani

Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili .....

HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MJAKAZI WA SULTANI

Mtukufu sultani, nakwenda kukusimulia tukio lililotokea leo hii wakati tulipokuwa tunaburudika. Tulikuwa tupo kwenye tafrija moja hivi jana wakati wa jioni kabla ya juwa kuzama. Katik tafrija hiyo tulipata kusikiliza usomaji wa quran kwa sauti nzuri sana hata machozi yakatutoka. Baada ya hapo tukabahatika kusikiliza mashiri. Mshairi maarufu kutokea India alikuwepo, na alighani kwa sauti njema sana.

 

 

 

Baada ya burudani kuisha ndipo tukaletewa chakula kizuri sana. Vyakula vya kuoka, na nyama iliyo kaushwa vizuri ililetwa bele ya hadhara. Vinywaji vilivyo vizuri vikahudhurishwa mbele yetu. Basi tulikaa vikundi vikundi kuzunguruka sahani za vyakula. Katika kundi nililokaa nilikuwa na aliyekuwa na shughuli yake siku ile. Na hapa kitu cha kushangaza ndipo kikatokea.

 

 

 

Katika vyakula vilivyoletwa kulikuwepo na zerbajeh. Hiki ni chakula zilichotengenezwa kwa mchanganyiko wa vyakula kadhaa na matunda. Chakula hiki unapokila harufu yake inaweza kukaa kwa muda wa siku nzima kwenye mikono. Ni chakula kitamu na kipendwacho na watu wa Baghadad. Basi ghafla mwenzetu mmoja alipoona chakula kile akaanza kutetemeka na kutokwa na majasho kana kwamba ameona kitu cha kutisha sana.

 

 

 

Yule bwana hakutaka hata kula chakula kile. Sikuwa na wasiwasi sana nikajuwa lamda hali chakula kile, ama lamda kuna mtu anamdai ndio maana akapata woga. Wakati tunakula nikamuona yule bwana kidolechake gumba kimekatwa. Alipokuwa nakata nyama, nikagundua vidole vyake gumba vya mikono vyote vimekatwa. Hapo nilishindwa kujizuia kuwa na shauku, nikataka kumuuliza kulikoni. Lakini ikabidi nimsubiri amalize kula.

 

 

 

Kumbe wakati ule hata yule mwenye shughuli yake alikuwa anashuhudia yanayotokea. Alikuwa akinisubiri nianza kuuliza. Kwa kuwa yeye ndiye mwenye shughuli isingekuwa vyeka kumkera mgebi wake. Ndipo naye akasubiri amalize kula ili amuulize. Yule bwana alipomaliza kula nikamuuliza “ndugu yangu nimeona hata huugusa chakula hiki “zerbajeh” ama hukupendi” naye akajibu “ninakipenda ila baada ya kula ni lazima nioshe mikono yangu mara 40 kwa maji, mara 40 kwa alita na mara 40 kwa sabuni. Sasa vitu hivi hapa havipo na si vyema kusumbuwa watu kwenye shughuli hii”

 

 

 

Kwa shauku zaidi nikamuuliza ana nini hasa. Ndipo akanieeza kuwa chakula hiki ndio sababu ya yeye kukatwa vidole gumba vya mkono wake. Kisha akatuonyesha na vidole kumba vya miguu yake, pia vimekatwa. Hapo nikapata shauku zaidi kujuwa hasa kwa nini amekatwa vidole gumba vyake vyote vinne kwa sababu ya chakula tu.

 

 

 

Wakati mazungumzo yetu haya yanaendelea yule bwana Mansur mwenye shughuli yake alikuwa anasikiliza. Basi akaagizwa kuletwe ndoo mbili za maji, sabuni na alita. Hapo kopo la kunawia na alita zikaandaliwa kwa ajili ya kutoa povu vyema. Kisha ikaletwa tena sahani yenye zerbajeh. Akaambiwa ale kisha atanawa kama anavyotaka. Basi akala vyema akanywa maji na kumshukuru Mungu. Kisha akaanza kunawa na alita mara 40 kisha sabuni mara 40 kisha maji mara 40. alipomaliza tukamtaka atusimulie hadithi yake ndipo akasimulia hadithi ifuatayo:-

 

 






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Mankaa Tarehe 2024-09-10 14:03:34 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 138


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 11: Kisa cha Kalid na Jalid
Tuendelee kusikiliza na kusoma visa, hadithi, na simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza tuwe pamoja mpka mwisho...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 15: Hadithi ya safari ya Sinbad
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 3 Part 2:  Simulizi ya tabibu wa mfalme
Simulizi ni nzuri sana maana zinafundisha na hazibagui mkubwa wala mdogo... tusikilize na kusoma kisa cha tabibu wa mfalme....kutoka katika kitabu cha kwanza cha HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 1: Hadithi ya safari saba za Sinbad
Hadithi hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 16: Kitabu cha ajabu
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 7: Upendo uliotafsiriwa
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 6: Hadithi ya mwenye kutabiriwa mtoto wa tajiri
Tunapfatilia simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza simulizi hii imetoka ndani ya kitabu cha kwanza karibuni tuendelea kupata skmulizi nyingi za kusisimua ..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 10 Part 1: Carmaralzamani prince pekee
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 2 Part 3: Hadithi ya mzee wa pili na mbwa wawili weusi.
Simulizi za HALIF LELA U LELA ni nziri sana tuwe pamoja kusikiliza kisa cha mzee wa pili na mbwa wawili weusi... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 1: Hadithi ya chongo watatu, watoto wa mfalme na wanawake wa Baghdad.
Skmulizii hii pia imetoka kitabu cha kwanza cha HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 2: Kisa cha kinyozi msiri..
Karibuni tuendelee kusimuliana stori za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza, stori nzuri sana na za kuvutia zimeandaliwa kwaajili ya kujifunza na kujiburudisha pia..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 8 Part 1: Hadithi ya tunda
Simulizi hii pia inapatikana kwenye kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...