NDEGE WAFIKISHE
Hebu paa ndege paa, ufise habari hizi, Ufike wanako kaa, imi kufika siwezi, Paa bila kuzubaa, upae anga iwazi Naujumbe huu twaa, tekeleza hiikazi, Kawa pe utawafaa, wata po fa nyia kazi Kwa watakaokataa, usifanye lazimizi, Wambie lamanufaa, niwasihilo mtunzi, Elimu iso chakaa, ni ifanyiwayo kazi, Ili wawe mashujaa, waepuke upuuzi, Waache kata tamaa, katikalao amuzi Subira ikiwajaa, lilofichwa huja wazi, Shidani wakikomaa, lazima lije tatuzi, Wasivunje ujamaa, sababu yamachukizi, Wasiishi kwahadaa, nichukizo kwa mwenyezi, Nawaache kuzubaa, wafanyapo andalizi, Wambie elimu taa, kuikosa niajizi, Mwenye elimu hun'gaa, sioleo tangu juzi, Ujinga kizaazaa, mfano kama uchizi, Yasaba beti nakaa, sitaki uendelezi, Shikeni hayo kadhaa, yalainishe ulezi, Tungo hii nibidhaa, nawaipe mapokezi, Mtu nzi:H D.Hassa n Tanga pangani 0655832944