KUTOA NI USHUJAA
KUTOA NI USHUJAA
Salamu kwanza awali, wasikizi tikieni, Mwambaje nazenu hali, kheri nawatakieni, Mungu awape sahali, muifuzu mitihani, Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa, Kila alie akili, hutunza yake thamani, Hilo sote twakubali, sitaraji upinzani, Zingata yangu kauli, ikufae maishani, Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa, Mja ulie na mali, mtazame masikini, Kwani wake udhalili, niqadari ya manani, Kumtenga niajali, tena mbaya hukumuni, Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa, Natena usikubali, aingie dhilalani, Maliyo siibakhili, nikuipa kisirani, Mungu kwayake ajili, mlinde huyojirani, Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa, Kumwacha niukatili, tena usio kifani, Fikiria mara mbili, mali kwakomtihani, Hakutatosha kuswali, namisaada toweni, Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa, Ukitaka afadhali, nauishi kwa amani, Mafunzo haya nakili, uyatie matendoni, Kiombwa siwe mkali, toa kwadhati moyoni, Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa, Maisha nipande mbili, kuna nyuma na usoni, Ukatae ukubali, lambeleni hulioni, Kesho hashindwi jalali, nawe kukushusha chini, Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa, Mtu nzi:H D.Hassa n @SUKARI YA [email protected] Pangani Tanaga 0655832944