CHUKI
Kwako lifike darasa, lisilo lamembarini, Lisilo hitajipesa, adakama yashuleni, Litambue hili kosa, silitie matendoni, Mvaach u ki moyoni, mwenyewe h uja mtesa, Kisikie hikikisa, utafakari kichwani, Sichakale nicha sasa, sikiliza kwamakini, Upate kiini hasa, nakipi utabaini, Mvaa chuki moyoni, mwenyewe huja mtesa, Bwana mmoja afisa, wacheo serikalini, Alie akitikisa, kwa mbwembwe zote mjini, Mkewe ekuwa tasa, ndio wake mtihani, Mvaa chuki moyoni, mwenyewe huja mtesa, Nduguye damu kabisa, kwake hali masikini, Ekuwa na wana tisa, na wakumi e tumboni, Ikatokea furusa, kuitwa kibaruani, Mvaachuki moyoni, mwenyewe huja mtesa, Bwana akaanza visa, vya kuvunja tumaini, Ila ndugu hakususa, akatazama usoni, Kumbe kilichomtesa!, apate vyote kwanini? Mvaa chuki moyoni, mwenyewe huja mtesa, Lilo likimtonesa, atarithiwa nanani, Nahakutaka kabisa, wale wana wafulani, Donda hilo halebesa, lemuweka taabani, Mvaa chuki moyoni, huja mtesa mwenyewe, Kufumbua na kupwesa, aondolewa cheoni, Bila kosa bila kisa, karudi uriyani, Machungu akaalisa, kwahuzuni na nun'guni, Mvaa chuki moyoni, hujamtesa mwenyewe, Shida kuanza mnusa, msaada hauoni, Hana nduru hana hisa, akangia majutoni, maisha yakibubusa, ikawa kwake ngani, Mvaa chuki moyoni, mwenyewe huja mtesa,