Navigation Menu



HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA SAFARI SABA ZA BAHARIA SINBAD

SAFARI SABA ZA SINBADKatika nchi ya Baghdad kulikuwepo na kijana aliyejulikana kama Sinbad mbeba mizigo.

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA SAFARI SABA ZA BAHARIA SINBAD

Safari 7 za Sinbad

By Rajabu Athuman

SAFARI SABA ZA SINBAD

SAFARI SABA ZA SINBAD
Katika nchi ya Baghdad kulikuwepo na kijana aliyejulikana kama Sinbad mbeba mizigo. Kijana huyu alijaaliwa kuwa na uwezo mkubwa wa nguvu za kuweza kubeba mizgo. Pia alikuwa na uwezo mzuri wa kiakili. Sinbad aliipenda sana kazi yake pia watu walimpenda kwa kuwa alikuwa akifanya kazi zake kwa umakini.


Ilitokea sikumoja alipokuwa katika kituo chake cha kufanyia kazi alikuwa mtu mmoja asiyemfahamu kabisa na kumpa kazi ya kupeleka mzigo wake sehemu husika. Mtu yule alitoweka baada ya kutoa maelekezo na kumpatia pesa yake. Sinbad baada ya kupewa maelekezo aliuchukuwa ule mzigo na kuanza kuukokota kwenye mkokoteni wake kuupeleka alikoelekezwa.


Njiani Sinbad alikutana na geti liliozungukwa na mauwa mazuri yenye kuvutia ndege, wadudu na wanyama kwa harufu na utamu wake. Sinbad alisimama kidogo eneo hili ili apate kushangaa uzuri ulioje wa eneo hili. Akilini alijiambia kuwa bila shaka ndani ya eneo hili kuna nyumba kubwa yenye bosi mkubwa.


Sinbad akiwa katika hali hiyo alituwa mzigo wake chini na kuanza kufuta jasho lake. Alisogea kidogo kwenye geti lile na kuona ndani kuna mambo ya kuvutia. Sinbad alikuwa ni kijana mwenye adabu na heshima lakini leo alisahau mambo yote hayo na akaanza kuchungulia ndani kwa watu. Alipokuwa hatoshelezi macho yake aliamua kuingia kwenye geti lile ili aone zaidi.


Sinbad hakuamini macho yake kama yanamuonesha sahihi, aliona nyumba kubwa yenye kila akijuacho kuwa kinahitajika, na aliona pia ambavyo havijui. Aliona nyumba iliyozungushiwa malumalu na lulu zikiwa zinaningi’inia kama mauwa mazuri yaliyopambwa. Rangi za nyumba utadhani ni dhahabu iliyochovywa. Kawahakika Sinbad alistaajabu sana. Kisha akaanza kuzungumza maneno yaloonesha kumalaumu mwenyezi Mungu kwa kuwapa watu wengine mali nyingi kama anazoziona pale. Pa aliendelea kumlaumu mwenyezi mungu kwa kumfanya yeye apate rizki kwa jasho jingi lakini watu wengine wapo wamekaa na bila jasho wanapata rizk.


Sinbad alilalamika sana hata akasikiwa na mwenye nyumba. Basi akaamrisha aletwe, akiwa natetemeka kwa woga Sinbad alipelekwa mbelel za Mkuu wa nyumba. Kisha akamwambia akae. Sinbad hakuamini kama meambiwa akae maana alifikiri atapewa adhabu kali. Basi mkuu wa nyumba akamuuliza “unaitwa nani kijana” “naitwa Sinbad “ au Sinbad mbeba mizigo. Yule mzee akamwambia jina zuri sana na inaonekana wewe ni wajina wangu. Mimi naitwa Sinbad au ukipenda niite Sinbad wa baharini.


Baada ya kutambulishana majina Sinbad wa baharini akaanza kumwambia Sinbad mbeba mizigo. “kijana nimekusikia maneno yako, ila sio kosa lako kusema maneno yale na wewe pia si wa kwanza. Kwani wapo wengi wamesema kama wewe. Sasa leo nataka nikueleze kuwa mimi sikupata mali zote hizi kwa kukaa hapa bila ya jasho. Kabla sijapata mali hizi nilipata tabu kubwa sana na pengine hakuna anayeweza kunifikia jasho na taabu nilizopata wakati natafuta malihizi”


Huu ni wakatii sasa wa mimi kula na kuulia kwani mchumia juani hula kivulini. Kabla ya hapo mimi nilikuwa ni mfanya biashara wa majini yaani nasafiri visiwa mbalimbali. Utajiri wote kuu umettoka na na taabu na mashaka yalonikuta. Nilisafiri safari SABA ambazo hizo nilipata taabu kubwa sana na sito sahau. Leo nitakueleza wewe na walokuwepo hapa yalonikuta kwenye safari hizo.”


Basi kabla hajaanza kusimulia Sinbad mbeba mizigo akamwambia Mkuu mimi nina mzigo wangu natakiwa niupeleke sehemu hivyo niruhusu niondoke. Palepale Sinbad wa baharini akamwambia nitakupa mtu umuelekeze apeleke yeye hiyo mizigo na nitakulipa pato la siku yako yote ila ukae na mimi leo upate kusikia hadithi saba za safari zangu saba. Basi palepale akamuagiza mtu apeleke mzigo ule na vinywaji na vyakula vialetwa. Watu wakakusanyika na kukaa tayari kusikiliza hadithi za safari saba za sinbad. Badi bila ya kuchelewa akaanza kusimulia hadithi ya safari zake kama ifuatavyo:-


SAFARI YA KWANZA YA SINBAD
Tambua kuwa baba yangu alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana katika nchi ya baghdad wakati wa utawala wa sultan harun Rashid. Baba yangu alifariki miaka 21 iliyopita nilipokuwa kijana kama wewe. Wakati huo nilikuwa na marafiki wengi sana. Na nilianza kutumia mali aloniachia baba na hatimaye akakaribia kuisha na marafiki wakanikimbia. Na hapo ndipo nilipoamua kuanza biashara za majini, yaani kuuza bidhaa sehemu mbalimbali za visiwa.


Nilijiandaa vizuri kwa ajili ya safari yangu ya kwanza. Na maandaliizi yalipokuwa tayari tulianza safari ya kubiashara. Safari ilikuwa salama kabisa kwa muda wa masiku. Tulipita visiwa kadhaa tukiuza na kununua. Kwa upande wangu biashara haikuwa mbaya ijapokuwa ugeni ulinisumbuwa sana. Kwa ujumla nilifurahia safari ile. Baada ya kutembea visiwa kadhaa tuliamua kumalizia katika viziwa vingine ili tuweze kurudi nyumbani. Ilitikea sikumoja ghafla upepo ulianza kubadilika na jahazi likashindika na kudhibitiwa na manahodha.


Upepo ulizidi mpaka nahodha akaamua kukiachia chombo kiende kokote, hali iliendelea kuwa mbaya mpaka bidhaa zikaanza kutumbukizwa majini ilikuokoa ualama wa maisha. Haliiliendelea kuwa mbaya hata chombo kikaanza kunywa maji. Watu wakaanza kuania rohozao, na kuanza kushika mbao zilizovunjika kutoka kwenye jahazi. Mimi nilipata mbao moja na ilinipeleka mbali zaidi ambapo sikuweza kuona hali za wenzangu kilicho endelea.


Kwa upande wangu mawimbi ya maji yalinipeleka mbali sana, nikiwa nimeshikilia tawi lile hata sikusubutu kuliachilia. Nilipofika hali ambapo sijielewi kwa kuchoka ghafla nikaona kunaweupe mbele yangu, kuangalia vizuri kilikuwa ni kijisiwa kidogo. Basi nikajitahidi kujizuia huku nikawa naiba maji ili yanipeleke kule. Kwa bahati njema kaupepo kakanipeleka kwenye kisiwa kile. Kwa msaada wa mizizi ya miti niliweza kutoka kwenye maji yale.


KISIWA CHA UOKOZI
Nikajisogeza vyema hata nikafika kwenye kivuli. Na kwa kuwa miguu yangu haikuwa na nguvu nilibuluzika tu. Nililala bila ya kijitambua niliamshwa na maji yaliyokuwa yakinipiga miguuni kumbe maji yalikuwa yanajaa. Haukupita muda ghafla nikaona kuna kijahazi kinaingia kikiwa kina mifugo kadhaa. Walipofika pale kisiwani wakawafungulia mifugo yao na kuanza kuwaosha na kuwapaka dawa. Mmoja wao akaenda mbali kidogo akaja na majani mengi sana na kuanza kuchagua baadhi ya ng’ombe na kuanza kuwapa majani yale.


Niliwafuata na kuwaomba msaada wa chakula. Wakanipa maziwa na mkate wa nyama. Nilipomaliza kula wakaniuliza habari yangu na eneo lile na nikawaeleza kila kitu. Basi wakaniambia kama ungekuja kesho usingetukuta na pengine ungefia hapa maana hakuna majahazi yanayokuja hapa ila ni sisi tu na huchukuwa miezi 3 ndo tunakuja tena. Na kisiwa hiki hakina chakula, hivyo pengine ungeishia kufariki hapa. Basi wakanipatia na nguo na nikawauliza pia sababa ya wao kuja hapa na ni kinanani wao.


Mkubwa wao akanieleza kuwa wao ni watumishi wa mfalme aliyepo karibu na eneo hili. Mfalme huyo amekiteua kisiwa hiki kama eneo la kutibia mifugo yake na amepanda majani maalumu kama dawa ya mifugo yake. Hivyo eneo hili hawaruhusiwi watu wengine hapa. Basi walipomaliza shuhuli zao walifunganya mizigo yao na kuchukuwa majani mengi na nikaondoka pamoja nao.


Tulipofika kwenye utawala wao wakanipeleka kwa mfalme wao na nikamueleza mimi ni nani na nini kazi yangu na kumueleza kuwa natokea baghdada nchini kwa sultan Harun Rashid. Basi mfalme yule nikamueleza mengi kadir alivyouliza na mimi sikuwacha kuu;liza mambo kadhaa. Kwa haraka zaidi mfalme yule alionekana kunipenda sanan na kunikubali. Basi alinifanya katika watu wa karibu yake na ni kama mshauri pia. Niliishi pale nikawa nafanya biashara chini ya mfalme yaani nilikuwa naendeleza bishara za mtoto wake wa kike.


Siku moja niligundua kuwa kuna kisiwa jirani ambapo kunasikika sauti za furaha kila siku. Nilipouliza nikajibiwa kuwa ni kisiwa jirani huwa wannafanya sherehe kila wanaporudi kutoka kutafuta lulu. Hicho ni kisiwa pekee kinachofahamika kwa kuwa ni wafanyabiashara wa lulu. Basi kwa kuwa sikuijua lulu ilibidi niumuombe ruhusa mfalme ili na mimi nikashuhudie sherehe zao na nipate kuijua lulu. Mfalme alikubali na akanipa msafara wa wafanyakazi wake waende pamoja nami.


Tulipofika kule nilifurahi kuiona lulu kwa mara ya kwanza na nikafurahia pia sherehe zao. Basi katika hali kama zile nilishangaa kuona kuwa watu wanashusha mizigo kutoka bandarini lakini katika ile mizigo kuna ambayo imeandikwa Sinbad, nilipoangalia kwa uzuri nikagundua kuwa nahodha wa lile jahazi alikuwa ni yule nahodha wetu. Hivyo kumbe zile mali zilikuwa ni zakwangu na lile jahazi lilikuwa ni lile letu. Nikamuita kijana mmoja na nikamuuliza habari zao na akanieleza kuwa walibahatika kuliokoa jahazi lao na watu wote walipona isipokuwa Sinbad ndo hakuonekana. Kijana huyu alizungumza bila ya kunijuwa kama ndo mimi


Basi nikamfuata nahonda na kumueleza kuwa mimi ndo Sinbad na zile mali ni za kwangu. Basi nahonda alliponiona akanikumbuka na kutoa machozi kwa furaha maana walifahamu kuwa nimekufa. Nahodha akanikabidhi mali zangu na nikaziuza, nikapata habari kuwa jahazi letu litarudi Baghdad wiki ijayo. Nilichukua bidhaa zangu na kuuza baadhi na kurudi kwa mfalme na baadhi ya bidhaa. Nikamuelezea kilichotokea na alifurahi sana kwa kupata bidhaa zangu. Na hivi ndo Mwenyezi Mungu anavyowafanyia watu wenye subira.


Nikampatia mfalme bidhaa zilizobaki kama zawadi na nikamuomba ruhusa ya mimi kurudi nyumbani kwetu wiki ijayo. Kwa majonzi na kinyongo mfalme aliniruhusu na hata binti yake alikuwa na majonzi sana lakini haina budi “milima haikutani binadamu hukutana” ni maneno nilojisemea moyoni. Basi wiki ilipoisha mfalme alinipatia mali nyingi sana kama zawadi. Nilipata pia lulu kutoka kwenye kisiwa kile. Kwa hakika katika safari hii nilipata taabu na faida kubwasana.


Tulipofuka Baghdadi niliwaelezea ndugu zangu habari ya yalonikuta, kwakweli waliniambia niwachanena habari za biashara hii. Hata mimi nikajiapiza kwa yalonikuta kwa hakika sitarudia tena bishara hii. Basi nikatoa sadaka kutoka katika faida yangu na nikatoa na zaka muda ulipo fika. Nilitumia faida ile kujiendeleza kibiashara hata miezi mingi ikapiata. Nilisahau kabisa yalonikuta kwenye safari ile. Baada ya muda nahodha wetu wa mwanzo nilikutana nae, na katika mazungumzo yetu alinieleza kuwa wanatarajia kuanza safari wiki ijayo.


Kwa hakika nilivutiwa tena na biashara ile. Na kwa kuwa nilisahau machungu yalonikuta katika safari ya kwanza nikaazimia kuanza safari ya pili wiki ijayo. Mpaka kufikia hapa Sinbad kwa baharini akamaliza kusimulia hadithiya safari yake ya kwanza. Na kwa kuwa muda ulukuwa umekwenda hakuweza kuanza hadithi ya safari yake ya pili. Basi akampatia Sinbad mbeba mizigo zawadi nyingi na pesa kadhaa ya kutumia kama fidia ya kuvunja kazi zake. Na akamuahidi kesho awahi kuja maana safari ya pili ina mambo mengi na makubwa zaidi kuliko ya kwanza.


SAFARI YA PILI YA SINBAD
Basi siku ile Sinbad mbeba mizigo aliwahi haraka sana na mapema zaidi, na akamkuta Sinbad wa baharini ameshakaa na watu wake wanamsubiri kuanza hadithi. Walipokusanyika watu wote vikaagizwa vinywaji na vileja na kuanza kula huku wakisikiliza hadithi. Sinbad wa baharini akaanza kusema “basi tambueni kuwa sfari hii ya pili nilikutwa na makubwa zaidi kuliko hii ya kwanza. Ha ilikuwa hivi:-


Basi tulipozungumza na nahodha kuwa wiki ijayo wataanza safari nilirudi nyumbani na kujiandaa kwa safari. Ndugu zangu walijaribu kunizuia lakini sikuwasikia “sikio la kufa halisikii dawa” wengine wakanambia najipeleka nikafe ila sikuwasikiliza. Maandalizi yalikamilika kwa siku mbili na nikawa nasubiria safari tu. Wiki ilipofika tukaanza safari kwa amani lakini siku ya tatu kabla ya kuingia kisiwa cha kwanza kufanya biashara hali ya hewe ikabadiliki ghafla.


Nikiwa na woga sana juu ya roho yangu nikabaki namuomba msamaha mwenyezi Mungu. Jahazi lilikwenda ovyo ovyo kwa muda wa masaa sita. Manahodha walifanya wawezapo hata wakaamua sasa kuachia hatima kwa Mwenyezi Mungu. Abiria tulianza kutapika na mimi nikiwa mmoja wapo. Kwamuda kadhaa nilipotelewa na kumbukumbu na sikufahamu zaidi. Nilikuja kupata fahamu chombo kilianza kutulia mbele yetu kukiwa na weupe kwa mbali. .


Nilikaa vizuri nipate lujua kinachoendelea. Manahodha walituambia kuwa kwa sasa tunaingia kisiwa cha roc. Kisiwa hiki hakuna wakazi na wanyama pia hakuna au ni wachache. Kuna hadithi ya zamani sana walokuwa wakisimulia mababu kuwa kuna roc aliyekuwa akila mali za watu kama mifugo na kujeruhi wakazi. Hivyo watu wamehama kisiwa hiki. Ni miaka mingi sasa na ni mababu tu wanasimulia hadithi hii. Huenda ni ngano tuu au ni kweli. Hivyo tutaingia hapa kwa ajili ya kupumzika kidogo na kuangalia kama tutapata maji maana safari ni ndefu. Basi tukaingia kisiwani pale na kuanza kuranda randa. Kwakuwa nilitapika sana sikuwa na nguvu za kutosha hivyo nikaelekea kwenye kivuli kikubwa na kujilaza. Nililala sana na nilipokuja kuamka sikuona watu wala jahazi. Kumbe nilisha kimbiwa, niliogopa sana na nisijue nitatokaje pale kisiwani ambapo hakuna watu wala chakula. Nilianza kujuta kwa kukubali kuja. Nilijua sasa hapa kisiwani nitakufa pekeangu kwa kukosa chakula.


Nilianza kukizunguka kisiwa chote kujua nini nitafanya. Jua nalo lilikuwa likizama. Katika kuzunguka nikaona kuna kitu cheupe kwa mbali. Nikaanza kukifata taratibu na nikakuta kama limpira kubwa sana na laiiini. Kuangalia vizuri sikufahamu nini kitu kile. Ghafla nikaona anga inafunikwa na kuna kivuli kikubwa kinaingia nilikimbia kwenda kujificha. Kumbe alikuwa ni ndege roc mkubwa sana yaani mguu wake mmoja ni kama shina la mti. Kumbe lile dude kubwa jeupe ni yai lake.


Basi kiza kilipoingia nilikwenda karibu na ndege yule nikavua kanzu yangu na kufifunga vizuri kwenye miguu ya yule ndege. Niliamini kuwa akiruka atanibeba na kunitoa kwenye kisiwa kile. Basi nilifanya hivyo na kuendelea na imani yangu hiyo. Mambo yakawa kama nilivyotaka asubhi ndege yule aliruka na kunibeba, kwa kuwa sikuwa mzito sana hakujua kama amebeba kitu lamda alijua ni guo tu.


KUELEKEA BONDE LA UOKOZI
Alinibeba akapaa angani sana hata sikuona ardhi. Alikwenda kwa muda wa dakika 30-50 na akatua kwenye bonde lenye milima. Alipotua nikajifungua na kwawoga alishituka na kuniacha pale. Nikaondoka kwa haraka na kujificha asijeniona. Muda haukupita roc alikamata nyoka mkubwa sana na kumkata vipande. Alimla na kuondoka na kipande. Alipoondoka na mimi nikatoka mafichoni pale na kuanza kuchunguza eneo lile na kujua vipi nitatoka pale.


Nilipochunguza zaidi eneo lile nikagungua ni bonde lililopochini sana na limezungukwa na milima mirefu yenye mawe. Ni bonde ambalo katu mtu asingeweza kutoka. Mchana mzima nilikuwa nikitafuta pa kutokea lakini bila mafanikio. Japo nilikuwa najishauri kuwa bora hapa kuliko kule kisiwani. Usiku ulipoingia nilijificha kwenye mapango na kulala. Usingizi haukuja kabisa kwa woga. Kwani uksiku nyoka walokuwa wakiogopa mchana kuliwa na roc walikuwa wakitoka kutafuta chakula.


Muda wote nilikuwa nikimuomba Mungu dua aniokoe na wadudu wabaya usiku ule. Mwenyezi Mungu alinilinda na ulipofika asubuhi nikaendelea na uchunguzi wangu wa eneo lile. Kwa ghafla nilishituliwa na kishindo nyuma yangu. Nilipogeuka nikakuta ni kipande kikubwa cha nyama. Nyama. Hapa nikakumbuka hadithi ya zamani sana juu ya bonde la wawinda madini. Wazee wetu walikuwa wakitusimulia kuwa kuna watu wanawinda madini kwa kutumia nyama. Yaani wanatupa nyama kwenye bonde lenye madini, kisha nyama ile inaganda vipande vya madini na pindi ndege wanapokuja kuchukua nyama ile ambayo ina madini yaloganda kutoka bondeni huwakimbiza ndege wale na wanapoidondosha wanachukua madini.


Pale nikawa nawaza huende hii ikawa ndio njia pekee ya mimi kutoka pale. Nikawa naangalia kama nitaona mtu lakini sikuweza kuona kwani juu ni mbali sana. Basi nikaamza kuokota madini mapande makubwa makubwa. Eneo lile lilikuwa na madini mengi na makubwa yalokuwa waziwazi. Niliokota almasi na dhahabu kwa wingi pamoja na madini mengine. Nilipomaliza nikayafunga kwa uzuri sana na kuanza kutengeneza mpango wa kutoroka pale nilipofungwa.


Kwakuwa mapande ya nyama yalokuwa yakitupwa yalikuwa ni makiubwa sana, nikachagua lile kubwa zaisi na kujifunga nali na kujificha kwenye kanzu yangu. Baada ya muda ndege mkubwa sana alikuja ndege aina ya eagle. Ndege yule ana watoto hivyo alichagua pande kubawa na kuondoka nalo. Pande hili ndo lile ambalo nipo. Alinipeleka mpaka kwenye kitundu chake. Na haukupita muda watu wengi wakatokea na kuanza kumtisha ndege yule na kunidondosha mimi na nyama ile.


Kumbe wale wawinda madini kila mmoja alikuwa na kitundu chake, hivyp walishangaa baada ya nyama anatoka na mtu. Niliwasimulia yote yalonopata. Walinipa pole lakini kwa kuwa nilikuwa na madini mengi sana yule mwenye kitundu chake nilimwambia achukue kiasi anachotaka na akachukua pande moja tu. Kisha akaniachia mengie, nikawagawia na wenzie. Tulikaa eneo lile kwa muda wa wiki tukiwinda madini na baada ya hapo tukaanza kurudi baghadadi, kwa kuwa na wale walikuwa wakiishi bafhdad ila hatukuwa tukijuana kwa kuwa ni wa mji mwingine.


Njiani tulipita misitu mikubwa na yakutisha, tulipishana na manyoka wakubwa sana hata tukafika ufukweni na nikauza baadhi ya madini yangu kwenye kisiwa cha Balrora. Nikanunua pale bidhaa kadhaa na zawadi za kupeleka nyambani. Siku tatu baadae tulipanda jahazi la kuelekea baghadad na tulipofika kwanza nikaanza kutoa sadaka na zaka mali zangu na nikawasimulia ndugu zangu yote yaloniptata. Walinipongeza sanana na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunirudisha salama. Nilikusanya watu na kufanya dua na kutoa sadaka zaidi kama ni shukrani yangu kwa msaada alonipa mwenyezi Mungu hata akanirudisha salama. Niliamua sasa kutofanya biashara nyingine za baharini na kuanza biashara ndogo ndogo. Nilifanya hivi kwa muda wa miezi sita, huku nikawa nafatilia habari za wasafiri. Muda wote huo sikusikia ajali yeyote na walikuwa wakinisifia faida walokuwa wakizipata. Nilivutiwa zaidi na nikasahau machungu yote yalonipata. Nikaamua kuanza safari ingine ya tatau.


Baada ya kumaliza hadithi hii Sinbad wa baharini akampatia Sinbad mbeba mizigo kiasi cha pesa kama ni fidia ya kupoteza muda wake wa kazi na kusikiliza hadithi yake. Kisha akamuahidi kesho awahi ili ajepata yalomkuta safari ya tatu. Akawaambia watu wote walokuwa pale kuwa kesho wawahi maana safari hii amekutwa na mengi ya kustaajabu. Basi watu wote wakatawanyika pale na Sinbad wa baharini akaingia ndani kwake.


SAFARI YA TATU YA SINBAD
Siku ile ya pili Sinbad mbeba mizigo alivaa ngup zake safi alizonunua na kijipamba vyema na kuelekea kwenye kikao chao. Alipofika alikuta watu wote wamekusanyika tayari wanamdsubiri yeye. Alipofika vinywaji viliagizwa na vyakula laini. Watu wakaanza kuburudika, na baada ya muda mzee Sinbad akawasili na kuaza kusimulia safari yake ya tatu kama ifuatavyo:-


Basi niliamua nisafiri tena kwa mara ya tatu, nikafuatilia taarifa za kuwa jahazi linaondoka lini na wapi. Nilikusanya bidhaa za kwenda kuanza nazo na maandalizi nilikamilisha kwa muda wa wiki nzima. Siku ya safari ilipofika ndugu zang walinisaidia kupeleka mizigo baharini. Walinisaidia na kupandisha pia huku wakinishawishi nisiende. Bila ya kujuwa kitakachonikuta nilikataa ushauri wao na kujitetea kuwa kwa miezi sita sijasikia ajali yoyote iwe leo kisa mimi nimo?.


Tulisafiri salama katika visiwa kadhaa na safari ilikuwa ni njema kwakweli. Tulifanya biashara visiwa kadhaa na kuona faida na matunda ya biashara. Hapa nikawa najuta kwa nini sikufanya biashara kwa muda wote huo. Tulikubaliana tuendelee kidogo kufanya biashara kisha turudi nyumbani baada ya siku kadhaa. Ijapokuwa nilipenda tuendelee lakini mawazo ya wengi sikuyakatalia. Basi tukaendelea na visiwa kadhaa hata kukaelekea kwenye kisiwa cha mwisho ili tugeuze. Kwa jumla tulikuwa watu 48 wafanya biashara pamoja na manahodha na wasaidizi tulikuwa jumla ya watu 60.


Tulipokuwa tupo kwenye bahari tukielekea kisiwa kile ghafla nahodha alipoteza uelekeo na kutuambia amepotea na yupo kwenye kisiwa cha maharamia vibushuti. Hatukuelewa nini anazungumzia lakini alifafanua zaidi ni watu wafupi wanaotembea kwa makundi. Kazi yao ni kupora majahazi. Basi haukupita muda tukawaona wanakuja, nahodha aliongeza kuwa kupambana nao kwenye maji hatuwezi ila tukienda nchi kavu hawatakuja.


Nahodha alijitahidi awezavyo awahi kufika nchi kavu kwenye kisiwa kinachoonekana jirani. Hakuwahi kufanya hivyo tukavamiwa na jahazi letu likachanywa na kukatwa katwa na nanga ikakatwa. Walipora mali zetu zote na tukakimbilia kwenye kisiwa kile. Tukiwa tukihangaika nini tufanye kuondoka pale tukaona kuna jumba kubwa sana mbele yetu. Bila ya kujuwa kama ule ni mtego mwingine tukaingia kwenye jumba lile na kuanza kufanya mipango.


Usiku ulipofika tukaamua kujisitiri mule. Kumbe jumba lile ni mtego wa majidude yanayokula watu. Wanavizia wasafiri wanapopata matatizo na kuporwa wakiingia mule wananafungua na kuwala. Basi usiku ule likaja jitu moja kubwa sana na refu pia. Kwa urefu alonao nilimfikia magotini na upana wake lamda tujipange saba kama mimi. Ukiangalia ukubwa wa jumba lile utaamini ukubwa wa alolijenga.


Basi limtu lile lilipoingia likafunga mlango na kukoka moto. Tukiwa tumetulia sana hatujui tufanye nini, lile limtu likaamza kumshikamshika kila mmoja. Likamkamata nahodha mkuu na kuanza kumbanika. Kumbe lilikuwa likiangalia mtu alionenepa amle. Alimbanika nahdha wetu na kuanza kumla. Alimla wote kisha akalala fofofoi. Kila mmoja alikuwa akitetemeka na kuanza kulia na kuogopa.


Lile limtu likalala pale mpaka ilipofika karibu na alfajiri likatoka na kuacha mlango wazi. Tulikaa pale ndani na baada ya muda tukatoka. Tulipofika nje tukaanza kupiga mipango ya kuondoka. Tulizunguka kisiwa kile kutafuta pa kulala lakini tulikosa. Tukiwa katika hali ilie nikapata wazo la kuwa tutengeneze mitumbwi midogomidogo. Tukaanza kufanya kazi ile hata usiku ukakaribia kuingia. Nikawashauri wenzangu kuwa tumuuwe yule mtu au tumtoboe jicho lake. Maana alikuwa najicho moja tu. Nikasisitiza kuwaambia kama tutamuuwa ndo tutaweza kuondoka hapa bila hivyo atatufuata na wenzie.


Tukapanga mpango wa kumuuwa na mimi nikiongoza mtego. Usiku ule tukaingia mule ndani na tukajifanya tumelala. Lile limtu likaingia na kuanza kumpapasa kila mmoja ili achukuwe alonona amle. Alimchukua nahodha mwengine alokuwa amenenepa zaidi katika sisi. Basi akambanika pale tukiwa tunamuona. Uchungu ulinishika lakini niliendelea kusubiri alale. Alipolala tu nikaweka msumari wa moto kwenye mato na ukaiva vizuri hata ukawa mwekundu sana. Baada ya muda nikawdokoa wenzangu kuwa mambo tayari


Nilimfata yule limtu na kumchoma na msumari ule kwenye jicho lake. Alilia sana na kuguta makelele. Alikwenda kukaa mlangoni ili atukamate. Kwakuwa alikuwa ni mrefu sana tuliweza kupita kwenye magoti yake hata bila kutupata. Tukaenda kwneye mitumbwi yetu na kuanza kuimalizia kwa msaada wa mbalamwezi. Lile limtu likaelekea sehemu huku linalia. Muda le kwa haraka zaidi tukamaliza mitumbwi yetu na tukagawana waiwi wawili kila mtumbwi.


Baada ya kugawana tukaanza kuingia maji kila mmoja anajitahidi kuenda kwa haraka kiasi awezavyo ili kuweza kuondoka kisiwa hiki. Basi baada ya jua kuchomoza tulikuwa mbali kidogo lakini tukashangaa tunaona weupe unakuja. Kumbe lile limtu lilikwenda kuwatafuta wenzie wengi wakiwa wamebeba mawe. Kwa urefu wao walianza kuyaingia maji na kuanza kuturushia mawe. Wenzetu walokuwa nyuma walizama kwa mawimbi ya maji baada ya kurushiwa majimawe makubwa. Mwshowe mitumbwi miwili tu iliokoka wakwetu na wawenzetu, hivyo tukawa wanne tulookoka.


Tulikwenda bila ya kujua wapi tutaishia, kwa bahati tukaona kisiwa kwa mbele zaidi. Tukaingia kwenye kisiwa kile na kunanza kutafuta chakula. Tukapata matunda na maji. Tuliandalanda pale na ilipofika jioni tulilala chini ya mti. Kwa ghafla usiku alikuja nyoka mbubwa sana na akamchukuwa mwenzetu aliyekuwa pembeni amelala. Tukaogopa sana maana tumeokoka kule kwenye mawatu na sasa ni nyoka. Kwa hakika usingizi haukuja tena.


Ilipofika asubuhi tulitafuta njia ya kurudi bila mafanikio basi nikawashauri wenzangu tutengeneze kitundu cha miiba tulale. Basi tukakusanya miiba mingi na kutengeneza kitundu.yule nyoka alipokuja usiku ule alizunguka kwenye miiba bila ya mafanikio. Baada ya muda alipata kaupenyo ka kuingia na akamchukuwa mwenetu mwingine. Pale tukabaki wawili tu. Asubuhi tukawatunajishauri la kufanya, bila mafanikio tukabahatisha kupata matunda machache ya kula tu.


Tukaamua kutengeneza kitundu juu ya mti na chini tuzungushe miba ili ashindewe kupanda. Tukafanya vile na ulipofika usiku alizunguka sana nyoka yule na aipate pa kuingia. Aliruka na kuivunja miba ile na kupanda juu na kumchukiwa mwenzangu pale nikabaki peke angu. Asubuhi ilipofika nikazunguka sana kisiwani pale na nikakuta sehemu kuna kimfereji cha mguu mmoja. Nikakivuka na kukutana an kisiwa kingine. Yule nyoka alishindwa kuja kule kwa sababu ya maji ya chumvi ambayo yangemuuwa kama angejaribu kuyavuka. Nilitembea huku na kule na kufika sehemu kuna kijibostani kizuuri. Nikawa nakula matunda. Kwa mbali nikaona kuna kibibi kizee kinaniita kwa ishara.


Nikaenda pale nikakikuta kibibi kinataka kuvushwa kwenye mfereji. Nikakibeba, ila mara tu baada ya kukibeba kikatia makucha yake kwenye mbavu zangu na kuganda. Kikawa kinaninyonya damu. Nikikaa pia habanduki, nilijitahidi kadiri niwezanyo lakini hakutoka. Nilichoka sana na nikaanza kupoteza nguvu na kukonda zaidi. Siku ya tatu nikatengeneza pombe kwa kutumia mizabibu na ilipokkuwa tayari nilimreburebu hata akakubali kunywa. Alipolewa aliachia na kuanguaka na hapo nikamkimbia.


Nilizunguka sana na mida ya mchana nikaona jahazi kwa mbali, hapo nikavua shati langu na kuashiria wajeniokoa. Walipokuja nikawasimulia habari yangu. Wengi walinipa pole na wengine wakanambia bahati yangu ila ningekufilia mbali. Wakanichukuwa na kuenda nao na safari yao. Tukafika sehemu kuna kisiwa, yule nahodha akanambia shuka ukafanye kama watu wanavyofanya. Nikaendanao watu wa jahazi lile mpaka kwenye kisiwa kile. Basi wakaokota mawe mengi sana wakawa wanawapiga nyani waliopo kwenye minanzi.


Nikaokota mawe na kupiga na mimi, basi kila nikimpiga nyani kwa jiwe ananirudishia kwa kunipiga na nazi. Basi nachukuwa nazi ile na kuiweka kwenye mizigo yangu. Niliweza kupata nazi mia sita. Mizigo ya watu ilipoenea tukaondoka na kwenda kisiwa kingine na kuuza bidhaa zile. Nilipata faida kubwa kuliko ile ilopotea kwenye maji. Baada ya hapo nikanunua bidhaa na tukaendelea kufanya biashara visiwa kadhaa na tulipofika karibia na baghadadi nikashuka na kurudi kwetu kwa majahazi yanayokwenda Baghadadi


Safari hii nilipata faida kubwa lakini nilipatwa na makubwa zaidi. Nilikuta ndugu zangu wakilia pindi nilipowaelezea kilichonikuta. Nilitowa sadaka mali yangu na kuendeleza biashara zangu. Niliogopa tena kufanya biashara za majini. Ijapokuwa uwoga huu unanipata kwa muda ila huenda nikasahau. Na hivi ndivyo huwa sikio la kufa halisikii dawa. Miezi kadhaa ilipita na niliposikia msafaa wa biashara unatoka baada ya siku 12 nilijifunganya na mimi niweze kutoka safari ya nne. Mpaka kufika hapa Sinbad wa baharini akamaliza msafara wake wa tatu na kumpatia Sinbad mbeba mizigo pesa kiasi kwa kufidia kazi zke. Akamuahidi awahi kesho maana safari ya nne alikutwa na hatari na mambo makubwa zaidi na alipata faida pia.


SAFARI YA NNE YA SINBAD
Basi ikafikia siku ya kuanza safari yangu ya nne ya kibiashara. Tulianza safari ile usiku hata ikafika asubuhi tukiwa katikati ya maji. Njia ya safari hii sikuwa na uzoefu nayo na niliona mambo mapy. Niliweza kuona majabali yalofanana na watu, wanyama na vitu mbalimbali. Pia tuliweza kuona mawe ya ajabu ambayo huwa hayapati maji sikuzote. Tukiwa karibu ya kuingia kwenye kisiwa chetu cha kwanza kwa ghafla tulivamiwa na majiwatu makubwa na yenye nguvu sana.


Watu hawa walifanikiwa kututeka sote tuliokuwa mule ndani ya jahazi lile. Walitukamata wote na kutufunga kamba na kutuziba macho yetu kwa vitambaa hata tusione wapi tunakwenda. Walitupeleka tusikokujuwa na kwa kuelewa tu niliona kama tunarudinyuma. Waliturudisha nyuma kwa muda wa takribani masaa matatu kisha tukaelekea upande wa kushoto na kukiwacha kile kisiwa tulokuwa tukikiona kuliani. Tulikwenda kwamuda wa takribani masaa sita. Nikiwa nachukuwa hisia juu ya safari ili niligunduwa kumbe wanatuzungusha tuu lakini tunatupeleka pale kwenye kisiwa kile tulichokiona.


Hatimaye tukawasili na wakatufungua machoyetu na hapo nikapata tena kuona ardhi nzuri yenye udongo mweupe wa kupendeza. Wale watu wakawa wanagawana kila mmoja kucukuwa watu kadhaa katika sisi. Waligombaniana watu wote na kubakia mimi. Walichelea kunichagua kwa sababu nilikuwa nimekonda sana. Basi akatokea mzee mmoja wa heshima katika wao akanichukuwa. Basi wote tuliingizwa kwenye jumba moja na kuletewa chakula kilichofanana na machicha ya nasi. Bila ya kuchelewa wenzangu wakaanza kula chakula kile ila mimi nikachelea kukila hata kikaisha.


Baada ya muda tukaletewa majani mithili ya majani ya miwa lakini haya yana maji mengi na ni matamu sana. Mimi sikuyala kwa kuhofia usalama wangu. Niliweza kugunduwa ladha yake kwa kuhadithiwa na wenzangu. Nilikaa na njaa kwa muda wa siku mbili hata nikakosa nguvu. Yule mzee akamiletea samaki wa kuchoma pamoja na mayai ya kasa. Nilikula sana hata nikashiba. Nilipopata nduvu ziku ya tatu nikaona mabadiliko kwa wenzangu. Walikuwa wakinenepa sana kwa ghafla kila walipokula vyakula vile. Kitu cha kushangaza wakawa wanapoteza kumbukumbu na kuwa na akili ya kinyama kinyama.


Hali iliendelea hivi kwa muda wa wiki tatu hata akawa mmoja kati ya wenzangu hawezi kupita kwenye mlago kwa unene. Basi wale watu wakawa wanamchukuwa mtu mmojammoja kila wiki na kuondoka nae na asirudi. Nikawa nafatilia nini kinaendelea hata nikagunduwa kuwa wanakwenda kumchinja na kumuuza nyama kwenye kisiwa kingine. Niolijaribu kuwaeleza wenzangu lakini wamekuwa wanyama hakuna walijualo zaidi ya kula tu. Mimi niliendelea kula vyakula kwa kuiba na hali yangu ikazidi kudhoofu.


Yule mzee akaamuwa kunitoa bandani mule kwa kuamini nikiwa huru naweza kunenepa. Hali iliendelea hivyo hata nikapewa funguo ya kuwalinda wenzangu. Waliendelea kuchinjwa hata wakabakia watu kumi na mbili. Kuna siku kulikuwa na sherehe na watu wakaondoka na kuniacha mimi na yule mzee. Basi nilitoroka pale peke angu kwani ningemhukuwa yeyote asingekubali na kwa unene na uzito alonao asingeweza kukimbia hata kidogo. Basi nilitoroka kwenda mbali zaidi. KISIWA CHA UOKOZI
Nilikwenda mpaka nikakuta misitu minene na nisijuwe pa kuenda. Kwa ghafla nikasikia sauti za watu wanaowinda na kwa uchovu nilonao nilianguka chini na kwa njaa nilonayo nilipootelewa na fahamu. Hapo sikujuwa kilichoendelea hata nikashituka nipo kwenye kitanda safi na pembeni kuna binti mzuri ananiwekea chakula tayari kwa kuniamsha ili nipate kula chakula. Bila hata kujaribu kuniamsha niliamka kwa upole na kumuuliza swali “eti unaitwa nani, na nimefikaje hapa?”. “naitwa ‘Aisha ni mtoto wa mfalme, umeokotwa porini na baba alipokuwa akiwinda”. Ni maneno aliyoyasema bint Aisha mtoto mfalme.


Nikanawa maji tayari kwa kuanza kula, baada ya muda wa dakika takriban 10 aliingia mfalme, na nilimtambua kwa mavazi yake. Baada ya utambulisho nikawaelezea kila kilichonikuta. Na akazungumza kuwa kwa uda wa miaka 10 wamekuwa wakikitafuta kijiji hiko bila mafanikio. Inadaiwa kuwa wakazi wa kijiji hiko sio watu wa kawaida hivyo walishangaa kuniona mimi nimeweza kutoroka kwenye kijiji kile kisichofikika. Basi mfalme aliniuliza mengi kuhusu Baghadad na bila kusita nikawa namjibu kwa uwazi kabisa. Kwa hakika alivutiwa sana na majibu yangu.


Mfalme alinitambulisha kwenye baraza lake na kunifanya mimi mmoja ya washauri wake na watu wa karibu. Niliishi pale kwa muda wa wiki moja hata siku hiyo baada ya swala ya magharibi nikasikia mlango unagongwa. Nikaenda kufunguwa nikamkuta mfalme na mkewake. Kwa heshima kubwa nikawakaribisha na walionesha uso wa furaha hata nisiijue sababu ya ujio wao. Baada ya kuwapatia maji ya kunywa mfalme akaanza kuzungumza.


“mwanangu, ujio wetu hapa mimi na mama yako ni kutaka ushauri wako. Kama ujuavyo sisi tuna mtoto mmoja tu naye ni wa kike. Pia binti yetu ameonesha kuvutiwa sana na wewe. Hivyo tumekuja kukuomba uwe mkwe wetu na mrithi wa utawala huu baada ya kufa kwangu”. Kimoyoni nilifurahi sana japo nikamwambia mfalme “nashukuru sana kwa maneno yako baba yangu mtukufu mfalme. Naomba muda nifikirie na nitakujibu baada ya mshuko wa swala ya ijumaa keshokutwa in shaa Allah” Basi mfalme akakubali kunipa muda ule na kuondoka.


Nilitafakari sana nini nifanye na nikikubali kuoa pale nitaondoaje kwenda Baghadad. Nitakuwa mkwe na mtoto wa kiume wa mfalme, na nitatakiwa kuurithi ufalme ule, hivyo ndoto zangu za akurudi nyumbani zitakuwa zimekwisha. Siku ilofata asubuhi nikaenda kwa rafiki yangu ambaye mkewe alikuwa akiumwa na tumbo. Nikaenda kumuomba ushauri lakini nikamkuta analia sana. Sikuweza kumuomba tena ushauri badala yake nikamuuliza kinachomliza zaidi. “rafiki yangu, tambuwa kuwa katika nchi yetu hii, akifa mke mume atazikwa pamoja na mkewe akiwa hai, na akifa mume mke atazikwa na mkewe akiwa hai. Hivyo nalia kama mke wangu akifa na mimi ndo mwisho wangu.


Niliposikia maneno yale pale moyo wnagu ulipasuka na kudunda haraka. Nikaanza kutetemeka miguu na meno. Jasho jingi lilinitoka japo kulikuwa na baridi wakati ule. Yote hayo yalitokea nilipokuwa nawaza nni nitamjibu mfalme. Maana nikikubali kuoa nikifa mimi wa kwanza sio taabu ana ila akitangulia kufa mtoto wa mfalme nitazikwa pamoja naye nikiwa hai. Mawazo haya yaliniumiza sana hata nikakosa hamu ya kula kabisa. Jioni ile mmnikapita nyumbani kwa mfalme na kumkuta binti yake akiumwa eti amekataa kula mpaka asikie jibu langu kwanza.


Hali ile ikazidi kuniogopesha zaidi pale niliposikia kuwa binti mafalme ameahidi kujiuwa kama nitamkataa. Nikaogopa zaidi niliposikia hivi. Nilijihisi uchovu na nikaelekea nyumbani kulala. Siku ilofata ilikuwa ndio siku ya ijumaa ambapo mfalme nimemuahidi kumpatia jibu juu ya kumuoa mwanae. Niliamka mapema sana siku ile na kuoga kisha nikaenda msikitini na kuwahi mstari wa mbele. Niliswali rakaa mbili na kufanya istikhara yaani kumuomba Mungu anipe majibu ya maswali yangu.


BINTI WA NDOTONI.
Baada ya kufikiri kwa kina na kumuomba mungu nilipitiwa na usingizi. Niliwa usingizini nikaota ndoto ya ajabu sana. Nilipokuja kuamka niliona watu ndo wanaanza kujaa msikitini lakini mfalme bado hajafika. Nikaanza kujiuliza maana na tafasiri ya ndoto ile ya ajabu. Nikiwa katika hali ya mawazo nilikuwa nikikumbuka machache kuhusu tafasiri za ndoto. Nikaanza kuichambua ndoto yangu nilioora. Nikiwa kwenye mawazo hayo nikaona kama kuna mtu amekuja na kuniuliza kuhusu ndoto yangu ili anitafasirie.


Nimeota nipo safarini na binti mfalme akiwa kwenye safari ile. Tukiwa tupo kwenye jahazi kwa ghafla tulipatwa na ajali. Mule kwenye jahazi lile hakuna mtu ninayemjua asipokuwa ni binti mfalme tu. Katika ajali ile jino lanhu moja liling’oka na nikatumbukia ndani ya maji. Binti mfalme akaja na kamba na kunirushia nikaikamata kamba ile na kufika kwenye mbao kubwa ambayo binti mfalme alikuwemo. Kwa bahati mbaya bint mfalme aliteleza kwenye mbao ile na kuingia kwenye maji, niliwa sijui uogelea nilijitahidi kumuokoa bila mafanikio na akaniashiria kuwa niondoke niendezangu. Baada ya hapo nikashituka


Katika hali kama hiyo yule mtu akanieleza kuwa ndoto ile ni ya ukweli na kunajambo ninaelezwa kwenye ndoto ile. Yule mtu akaanza kunieleza maana ya ndoto ile. “kuhusu kuwa safarini wewe na bint mfalme ni ishara ya kushirikiana. Na kuhusu kupata ajali inamaanisha kuwa katika kushirikiana kwenu mtapatwa na matatizo lakini yeye ndiye atakayekuokoa.


Na kwakuwa kwenye ndoto ni wewe ndiye uliyeokolewa inamaana wewe katika matatizo yako utapata njia kupitia kushirikiana nae. Na kuhusu yeye kushindwa kuokolewa na wewe na hatimaye akaishia majini inaonesha atapatwa na matatizo na atafariki bila ya wewe kufanikiwa kumuokoa. Ama jino linamaanisha kituchako cha karibi kama mke na ndugu. Hivyo jino lako lile linaonesha ni bint mfale atakuwa mkeo na kung’oka kwa jino ni ishara ya kufariki kwa mkeo. Hii ndiyo tafariri ya ndoto yako”


Baada ya hpo yule mtu akatoweka, nilipokuja kupaa fahamu kutoka kwenye mawazo yale sikumuona yeyote. Nikutaka kutafuta zaidi nikaweka imani kuwa huenda ni malaika ametumwa kunisaidia kufasiri ndoto yangu. Basi nikaamuwa kumuoa bint mfalme kutokana na ndoto ile inaonesha yeye ataanza kufa na mimi nitaokoka. Hivyo nikaamini hii ni mipango ya mungu. Basi baada ya swala nikaende kwa mfalme na kumueleza kuwa nimekubai ombi lake.


Nilipokuwa nazungumza na mfalme kumbe yele binti alikuwa akisikiliza mazungumzo yale na aliposikia nimekubali alipata furaha kubwa iliyopelekea akazimia. Tulishangaa kusikia kishindo nyuma ya mlango na kuenda kuangalia alikuwa ni binti mfalme aliyezimia pale chini. Moyowangu uliruka sana nikawa najiuliza ndo qadar zimeanza yaani atakufa kweli hapahapa na kuniacha mimi. Aliitwa muuguzi na kuanza kumpa tiba. Nilirudi nyumbani nikiwa nasikilizia kama atakufa au atapona maana akifa nitazikwa hatakama shererhe ya ndoa haijafanyika.


Nikiwa na wasiwasi siku ilofata nilielekea kwa mfalme kwenda kujulia hali ya binti yake. Nilishangaa kuona mfalme akiwa na bashasha punde tu aliponiona “mwanangu, mwenzio amepata fahamu tayari na mama yenu anaandaa maandalizi ili wiki ijayo iwe ni sherehe ya ndoa yenu. Nilifurahi sana kuona kuwa binti yupo hai maana alikuwa amebeba dhamana ya uhai wangu. Nikawa najiambia moyoni kuwa wiki ijayo naingia maisha mapya na nitakuwa mfalme mtarajiwa. Sinbad mimi ndo utakuwa mwisho wa kuiona familia yangu.


NDOA YA SINBAD NA BINT MFALME.
Siku hazikuenda kipolepole hatimaye wiki ikafika na harusi ikafanyika. Sherehe kubwa isiyo na kifani ilifanyika na hata wafalme wa jirani walihudhuria. Niliozeshwa binti yule na kukabidhiwa nyumba ndani ya ikulu. Nilipata kukabidhiwa na mali na mambo mengine kadhaa. Sherehe za kimila pia zikafanyika kwa ajili ya kukabidhiwa cheo cha mfalme ajae yaani baada ya kufa mfalme huyu nitakuwa mfalme mpya. Yote haya yalifanyika japo sikuwa na furaha nayo.


Ni miezi miwili sasa imefika na mishaanza kuzoea mazingira ya kulinda muda wote na kuzungukwa na watu. Nilitembelea uwanja wa kujifunzia farasi nikakuta watu wanaendesha farasi bila ya kuweka kiti chha farasi. Basi nikatumia taaluma nilonayo na kuwatengezea viti vya farasi. Jambo hili lilifanya nipendwe sana na watu na mawaziri kwa kuleta kitu kipya zaidi. Mapenzi ya mfalme na mimi yalizidi kuongezeka siku hadi siku. Watu walikuwa wakinikubali sana hasa ninapokuwa nawasimulia hadithi za kuhusu baghadad na safari za majini na mikasa iliyowahi kunikuta.


Ni miezi mitano sasa toka kumuoa binti mfalme. Binti mfalme alinipa habari za furaha kuwa ana ujauzito. Nilizipeleka habari zile kwa babamkwe na mama mkwe. Kwa hakika siwezi kusimulia namna ambavyo furahayao ilivyokuwa. Habari ziliwafikia mawaziri na watu wengine. Wote walikuwa wakiniupongeza. Binti mfalme alizidi kuniona mimi ni mtu muhimu sana kwenye maisha yake kwa kumfanya awe mama mtarajiwa wa familia ya mifalme.


Hatimaye miezi ya kujifunguwa ya binti mfalme imefikia na sasa amepelekwa kwa wakunga. Nikiwa nipo mlangoni kusubiria habari za furaha nilishitushwa na kilio kikubwa sana kilichotoka ndani. “Innaa lillahi wa innaa ilaihi rajiun” niliposikia maneno haya yakisemwa nikajua mtoto wangu amefariki dunia. Nilianza kulia sana, na muda si mrefu mkunga mmoja akatokea nje na kuniambia kuwa binti mfalme amefariki dunia na mtoto wake amepona. Nililia zaidi na kutamani ardhi inifukie.


Furaha za kupata mtoto sikuweza kuzipata kamwe nikikumbuka kuwa nakwenda kuzikwa na me wangu. Mila haikuwacha kufuata mkonowake sasa mwili wa marehemu ukawa unaanza kuandaliwa na nikamuona baba mkwe akija kwa unyonge na kunipa maelekezo na kunipatia nguo mpya na kuniambia hizi zitakuwa ndio sanda yako. Sina la kukusaidia lamba nitakuongezea mkate wa nane. Maana huwa aliye hai anapozikwa na mwenza anapewa kichupa cha maji na mkate mikate 7 hivyo nitakupendelea kukupa mikate nane.


Maneno haya yaliendelea kuniumiza hasa pale watu walipokuja kunihani na kuniaga kwa mara ya mwisho. Sasa ndipo nikaanza kujuta kukubali kutembea majini safari hii. Nilitamani hata ningekuwa kama wale wenzangu nilowaaza kule wanachinjwa maana taabu nitakayoiona na kuzikwa nikiwa hai ni kubwa. Basi likaandaliwa jeneza moja kubwa sana na mimi na mke wangu tukaingizwa na kubebwa kuelekea mazikoni. Walikwenda kwa muda wa masaa 2 na nusu kisha wakaanza kupandisha juu kwa mwendo wa nusu saa. Nikawasikia wanazungumza kuwa wamefika tayari.


NDANI YA PANGO LA MAKABURI
Mmoja wapo akatowa kamba na kulifunga jeneza vizuri na kuanza kulishusha chini ya mapango kwa kamba ile.hatimaye n ikahisi jeneza limefika chini kutokana na kugonga chini. Nikalifungua jeneza lile na kutowa mikate yangu nane na maji yangu. Nikaangalia huku na huku hakuna pa kutokea. Nikaangalia juu ni mbali sana na tundu ni dogo na hata sauti haifiki. Nilizunguka mchana mzima sikupata pa kutokea. Sikuya kwanza, pili, tatu mpaka siku ya nne sikupata pa kutokea. Nilikata tamaa nikajua sasa huu ndio mwisho wa Sinbad.


Nikaanza kula mikate yangu kwa kuilinda ili isiishe kwa araka. Sasa imefika siku ya sita nikiwa na mikate miwili mkononi. Ilipofika siku ya saba mida ya mchana nikasikia migongano. Nikasogea karibu kwenye lile tundu loo!! ni jeneza linakuja. Nilikuwa nikihisabu siku kwa kuangalia mwanga kwenye tundu lile dogo la kuingizia majeneza. Jeneza lile lilipofika chini nikaona mwanamke aliye hai amezikwa na mumewe. Mwanamke yule nikamsaidia kutoka pale nikiwa na imani kuwa ana mikate yake saba ambapo huenda akanisaidia pindi ya kwangu ikiisha. Nikamsaidia kutoka pale na kujanae pembeni kabisa ya lile pango ambapo harufu za wafu hazifiki kwa kasi.


Siku ile usiku nilipolala ghafla nikasikia sauti ya mnyama

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela1 Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 2994


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

NDOTO YA MGONJWA MTOTO WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa NDOTO YA MGONJWA BINTI WA MFALME. Soma Zaidi...

Kisiwa cha uokozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Safari ya sita ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari za Sinbad Soma Zaidi...

HADITHI YA TABIBU NA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA TABIBU WA MFALME Katika nchi ya Zouman iliyopo maeneo ya uajemi alikuwepo mfalme mkubwa sana. Soma Zaidi...

Hadithi ya tabibu wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Safari ya saba ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Kuingia kwa wageni
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Kitabu Cha hadithi ya Chongo
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI. Soma Zaidi...

Hadithi ya chongo wa pili mtoto wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...