Navigation Menu



HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA MVUVI NA JINI

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA MVUVI NA JINI

mvuvi na jini

by R
Rajabu Athuman

MVUVI NA JINI

HADITHI YA MVUVI NA JINI
Hapao zamani kulikuwepo na mvuvi aliyekuwa masikini wenye watoto watatu na mke mmoja. Alikuwa anavuwa kwa kutumia nyavu ya kutupa. Alijiwekea sheria ya kutupa nyavu mara nne kwa siku.


Alitoka sikumoja asubuhi, akatupa nyavu yake mara ya kwanza na asiambulie kitu. Akarudi nyumbani na kurudi baada ya muda, akatupa nyavu yake na akaambulia mauchavu. Akatupa mara ya tatau akaambulia mauchafu bila ya samaki. Na hapo nyavu yake alikuwa imeharibiwa hivyo akaishona na kuiweka tayari kutupa mara ya mwisho. Mara hii alipotupa aliambukia kuvua lichiupa la shaba lenye mfuniko wa silva.


Kwa kutaka kujuwa kilichomo mule akaamua kuofunguwa chupa ile. Akaanza kuitowa kifuniko. Ghafta akaona moshi mkubwa unatoka kwenye ile chupa. Moshi ukajikusanya angani kama kiwingu na punde tu kukatokea jini kubwa sana. “chaguwa mwenyewe kifo cha kukuuwa” ni sauti ya kushangaza ya jini lile. Mvuvi akashngaa kusikia anaambiwa achaguwe kifo.


“nimefanya nini mkuu? Na wewe ni nani? Na umetoka wapi?”. Ni fgurushi la maswali ya mvuvi kuliuliza lile jini.


“Mimi ni jini nilikuwa nimefungiwa kwenye chupa hii na mkuu wangu, na wewe ndo umenifungulia”. Ni maneno ya jini Mkuvu akamuuliza “sasa kama nimekufungulia ulipokuwa umefungu ina maana nimekutendea wema , haya mbona unataka kuniuwa”?


“nilifanya kosa na mkuu wangu akanifungia humu, miaka mia moja kwa kwanza niliahidi atakaye nifungulia nitampa utajiri mkubwa. Mika ile ikapita na sikupata wa kunifungulia. Miaka nia ya pili nikaahidi atakaye nifungulia nitampa thamani kubwa ya duniani, pia hakutokea wa kunifungulia. Miaka mia ta tatun nikaahidi atakaye nifungulia nitamfanya mfalme na nimpa anachotaka kwa kila siku. Pia miaka hii ikapita bila ya kufunguliwa. Baada ya hapo nikaahidi kuwa atakaye nifungulia nitamuuwa ila nitampa nafasi ya kuchagywa kifo atakachotaka. Hivyo wewe ndo umekuja kunifungulia, chaguwa kifo gani unataka ufe”.


Mvuvi akamwambia hule jini, “mimi siamini kama umetoka humu kwe nye chupa. Umeingiaje humu wewe mkubwa hivyo kwenye kichupa kidogo hiki?. Hebu ingia nikuone ndo nitaamini”.


Yule jini akajirudisha kwenye jhali ya moshi na akaingia kwenye ile chupa. “umeona sasa nilivyoingia?, nipo kwenye chupa sasa, umeamini?” ni maneno ya jini kumwambia mvuvi. Mvuvi baada ya pale kwa haraka zaidi akachukuwa kifuniko na akaifunga chupa. “sasa nitakurudisha kulekule baharini ulikokuwa.” ni maneno ya mvuvi akimwambia jini.


Jini akajitahidi atoke lakini akashindwa ikabidi amwambie mvuvi “ naomba nifungulie, nitakupa utajiri ukunifungulia” mvuvi kwa sauti kubwa akamjibu “hapana siwezi kukutowa usije ukawa umenidanganya. Nitakutupa baharini na nitaweka tangazo hapa ili atakaye ivua chupa ajuwe kuna jini airudishe”.


Jini likaanza kujitetea kwa saiti ya kinyonge “nakuomba, nakuahidi pia unifungulie, nitakupa utajiri”. Mvuvi kwa sauti ya busara akamjibu “naogopa yasije yakanikuta yaliyompata tabibu wa mfalme.” “ni yapi hayo yaliyompata tabibu?” ni swali la jini kumuuliza mvuvu. Mvuvi akaanza kusimulia hadithi ya tabibu kama ifuatavyo;-


HADITHI YA TABIBU WA MFALME
Katika nchi ya Zouman iliyopo maeneo ya uajemi alikuwepo mfalme mkubwa sana. Mfalme huya alipenda kusoma na kucheza mpira wa farasi, alimwamini sana waziri wake. Mfalme huyu alikuwa na ugonjwa ambao matatibu wengi walijitahidi lakini walishindwa. Kila tabibu mzuri katika nchi yake alijaribu bila ya mafanikio. Mfalme alikata tamaa ya kupon augonjwa wake.


Ilitokea katika nchi ile kuna tabibu ambaye ni mjuzi sana lakini hakutambuwa kama mfalme ana tatizo hilo. Tabibu huyu aliitwa Douban. Alipo[ata taarifa za ugnjwa wa mfalme alikusanya mavitabu yote na utabibu na kuanza kustadili kuhusu ugonjwa wa mfalme wake. Na hatimaye akafanikiwa kugunduwa dawa itakayomtibu mafalme. Dawa ambayo ingemtibu mfalme hata bila ya kumgusa. Siku ilofata alivaa nguo zake safi za kitabibu na akaenda ikulu kuomba kumuona mfalme. Kwa kuwa alijitambulisha kama tabibuilikuwa ni rahisi kwake kumuona mfalme. Alipiga magoti na kumueleza mfalme kilicho mleta. “nina dawa ya kutibu maradhi yako hata bila ya kukugusa kwa uwezo wa Allah” ni tabibu akimwambia mfalme. “ukitibu maradhi nilonayo nitakufanya tajiri na utakuwa ni katika watu wangu wa karibu” kwa furaha mfalme akimwambia tabibu Douban. “Ndio mkuu tutaanza tiba yetu kesho IN shaa Allah” ni maneno aliyoyasema tabibu.


Siku hiyo tabibu alivaa safi mavari yake na kuiweka dawa yake tayari kwa ajili ya kumtibu mfalme. Aliiweka dawa yake kwenye fimbo ya kuchezea mpira wa farasi. Kisha akamwambia mfalme atumie fimbo ile kuchezea mpira wa farasi na apige kwa nguvu mpaka jasho limtoke. Mambo yaka wa kama hivyo na mechi ikaanza. Mfalme alicheza kwa uwezo wake wote na akawa anapiga mpira kwa fimbo yenyedawa. Kila anapopiga ndio dawa inavyiongia kutoka kwenye fimbo kuingia mwilini mwake. Mechi ilipoisha akamwambia mfalme akifika nyumbani kwake aoge kisha alale. Mfalme alifanya vivyohivyo na alipoamka ailikuwa ni asubuhi. Alistaajabu kuona ampona kabisa maradhi yake.


Aliagiza tabibu Douban aletwe mbele yake ili amlippe alichomwahidi. Mambo yakawa vivyo hivyo aliletwa tabibu na kutoa heshima kwa mfalme. Mfalme alifurahi na kumpa utajiri yeye na familia yake. Tabibu Douban akawa ni katika watu wa karibu na mfalme. Baadhi ya viongozi wa nchi walimonelea wivi tabibu. Waziri mkuu alikuwa ni muhanga wa jambo hili. Alikuwa akikasirika sana kumuona tabibu na mfalme. Hakupenda ukaribu wao na alitafura mbinu na njama mbalimbali kuweza kuwatenganisha.


Sikumoja kaamuwa kutekeleza mpango wake, alimfata mfalme na akamweleza kuwa amegunduwa kuwa huyu tabibu anataka kukuuwa. “kama angetaka kuniuwa kwa nini amenitibu” ni swali la mfalme kwa waziri. “huenda ange kuuwa muda ule angejulikana, lakin sasa umemwamini muda si mrefu atatekeleza madhambi yake” waziri akimjibu mfalme. Mabishano haya yalichukuwa muda mfalme akimtetea tabibu na waziri akimkandamiza tabibu. Mwisho mfalme akamwambia tabibu “nakumbuka vizuri maneno ya waziri mfani alipomwambia mfalme Sinbad alipotaka kumkinga mwanae asiuliwe” . “ni maneno ganihayo ewe mfalme wangu” waziri akimuuliza mfalme kwa shauku. Mfalme akamjibu “alimwambia usiamini maneno ya mtu yeyote hata akiwa mkweo kisha akamsimulia hadithi hii”;-


HADITHI YA MKE NA KASUKU.
Hapo zamani kulikuwa na mfanya biashara, ambaye alikuwa na familia yake na mkewe ambaye alimpenda san. Hakuamini kama atakuja kuachana naye. Kwakuwa yeye ni mfanya biashara alikuwa akisafiri mara kwa mara. Ijapokuwa kuanwatu walikuwa wakimpa maneno kuhusu mkewe alikuwa ahawaamini. Ilifikia wakati sasa aliingiwa na mawazo ya kutaka kuwaamini japo hakufanya hivyo,


Sikumoja alipopata safasi alikwenda kwenye maduka yanayouzwa ndege wa kufuga. Alinunuwa kasuku mmoja laiye mzuri sana. Kasuku huyu pia alikuwa na uwezo wa kuzungumza habari zilizofanyika wakati bwana wake hayupo. Alimnun ua kasuku yule kwa gharama za juu na akamuweka kwenya kitundu chake. Alimpelekea mkewe na kumwambia “mtunze ndege wangu huyu, na umuweke ndandi na katu usimtowe”. Mke alitii ankumchukuwa kasuku yule na kumugifadhi ndani.


Mfanya biashara huye alitoka na kuenda mbali ya mji. Huku nyuma mkewe akafanya ya kuyafanya pale ndani. Ulipofika wakati mfanya biashara alirejea nyumbani. Alimchukuwa kasuku wake na kutoka naye nyumbani ili kutafute mahala pa faragha kisha akamuuliza kasuku kilichofanyaka pale ndani wakati hayupo. Kasuku aliyasema yote aliyoyaona na hayakumpendeza yule mfanya biashara. Aliporejea nyumbani aligombana saa na mkewe. Mke alishangaa ni nani alomwambia. Aliwapa adhabu watumishi wake akidhani ndio walovunja siri. Ila baada ya muda akagunduwa kuwa ni kasuku ndiye muongo.


Mfanyabiashara laipata safari nyingine ya kibiashara. Alipoondoka yule mkewe alipotaka mufanya anayoyafanyaga aliwaita wajakazi wake watatu. Mmoja akamwambia aweke beseni la maji chini ya tundu la kasuku, na mwengine akamwabia maji juu ya tundu la kasuku na mwinguni akamwambia achukuwe kioo na kwa kutumia mwanga wa mshumaa ammulike kasuku kwa mwanga uloakisiwa na kioo. Akamwambia afanya hivi kulia na kushoto. Wakati mambo yote haya yakifanyika yule mke nae alikuwa akifanya mambo yake anayoyafanyaga wakati mumewe akiondoka.


Siku ilofata mfanyabiashara akarudi nyumbani. Akamuuliza kasuku kilichotokea kasuku akamwambia “mmh bwana wangu mvua ilikuwa kubwa pamoja na radi nilishindwa kujuwa kinachotokea.” yule mfanyabiashara alijuwa kuwa hakuna mvua ilonyesha usiku ule. Akaona kuwa kasuku ni muongo hivyo akaamua amchinye. Baada ya siku akaja kugunduwa kuwa kasuku alikuwa mkweli ila alichezewa mchezo, alijilaumu sana lakini lawama zisingemrudisha kasuku.


Baada ya kumaliza kuzungumza hadithi hii (mvuvi akamwambia jini maneno aliyoyasema ) mfalme akamwambia waziri “sitakusikiliza kwa hili, nitamshughulikia tabibu na kama nisije nikajuta kama mfanya biashara alivyojuta baada ya kumuuwa kasuku asiye na hatia”. Waziri akajibu “mfalme tabibu anataka kukuuwa, siwezi kumuacha na kama itatokea nimefanya kosa nitakuwa tayari kuadhibiwa kama alivyoadhibia waziri wa mfalme flani” “alifanya nini huyo waziri” ni swali aliodakia mfalme. Waziri akasimulia hadithi ifuatayo;-


HADITHI YA WAZIRI ALIYEADHIBIWA.
Kulikuwa na mfalme aliyekuwa na mtoto wake mmoja wa kiume. Alimpenda sana mtoto huyu, huenda ni kwa sababu alikuwa ni mmoja na ni wakipekee. Mtoto huyu alipenda sana kuwinda na alikuwa ni hodari wa kupanda farasi, hasa alikuwa na uwezo wa kumdandia farasi kwa haraka sana. Zaidi haayo aliweza kuelewa lugha nyingi. Alikuwa anapokwenda kuwinda akienda na waziri ambaye alipewa kazi ya kumlinda mtoto huyu.


Walitoka sikumoja kwenda kuwinda, waliwinda kwa muda mrefu bila ya kupata kitu. Mtoto huyu akaona kibendera kimenyanyuliwa (isharaya kuonekana kiwindwa) alijuwa kuwa aliyonyanyuwa ni waziri. Basi akakifata kibendera na akakutana na swala mzuri mwenye afya. Alimfata na swala akikimbia, alichukuwa muda mwingi na hatimaye akaamuwa kurudi. Kwa bahati mabya alipotea nyia na asijuwe pa kurudia. Hakujuwa waziri yupo wapi, hivyo akazidi kutokomea mwituni.


Ilipofika karibia na jioni alikutana na bint mmoja msituni, akamkaribia na kumsalimia. “unafanya nini hapa na na ninnani wewe?” ni maswali aliyomuuliza binti yule. “mimi ni mtoto wa mfalme wa hindi na hapa nimepote” yalikuwa majibu ya bint. Basi akamchukuwa kwenye farasi wake na wakawa wanatafuta njia. Wakapita sehemu kuna jumba lililohamwa siku nyingi. Yule bint akashuka na kijana akashuka pia. Bint akawa anaelekea mule ndani. Alipoingia ndani yule kijana akiwa nje akasikia sauti ya yule bint ndani kwa lugha ya kihindi (yule binti alidhani yule kijana hatelewa lugha ile) “wanangu nimekuleteeni nyama kubwa yenye afya leo” akasikia sauti nyingine zikijibu “iko wapi mama tuile tuna njaa sana mama”. Kijana akagunduwa yule bint si mtu wa kawid,


Yule kijana kusikia vile kwa uhodari alio nao akaruka kweye farasi haraka na kuondoka. Baada ya mwendo wa dakika kadhaa akakutana na njia ya kuelekea kwao. Alipofika akamweleza baba yake kuhusu kilicho tokea. Mfalme alikasirika na akamwadhibu waziri kwa kutokuwa makini na kusababisha ajali kwa mwanae.


Baada ya kusimulia hadithi hii waziri akamwambia mfalme “angalia sana mfalme, unaonekana umemwamini sana tabibu, lakini usijejuta kwa kumuamini kwako kama alivyojuta huyu mfalme aliyemwadhibu waziri wake baada ya kumwamini”. Maneno haya yalimpenye sana mfalme, hivyo akaamuwa kumuamini waziri wake. Hivyo akaamuwa kumuuwa yule tabibu wake.


Siku iliyofuata akaamrisha askari wakamkamate tabibu na kumleta mbele yake. Tabibu akiwa hajui kinachoendelea, anashangaa kuambiwa amekamatwa kwa kosa la kupanga njama za kumuua mfalme. Tabibu akawa anajitetea “sasa kama ningetaka kumuuwa mfalme ina maana gani nikamponya?”. Ijapokuwa alizidi kujitetea lakini mfalme alishaamuwa ubaya hivyo hakusikiliza maelezo yake.Katika hali ngumu kama hii, yule tabibu akataka apewe ruhusa ya mwisho kuzungumza. “zungumza bila shaka, hata uzungumze vip leo utauliwa tu rafiki yangu tabibu.”. Ni maneno yaliyojaa kejeli kutoka kwa mfalme. Tabibu akazungumza “mimi sina kosa mfalme, ninaapa kwa jina la Allah, mimi sina kosa kabisa, lakini kama haina budi mimi kuuliwa, kuna kitabu changu kipo nyumbani, kitazungumza ukweli wote, juu yangu mimi. Kitabu hiki kitazungumza pindi utakapo niua”.


Baada ya mazungumzo haya mfalme akapatwa na mshangao na kuzungumza kimoyomoyo “yaani ili hicho kitabu kizungumze ukweli wa mambo mpaka wewe nikuuwe ndo kizungumze? Hii kweli ni khabarikubwa. Basi sina budu kukuuwa ili nione maajabu ya kitabu kinachozungumza”. Mfalme akamuuliza tabibu tukupe muda gani ukakilete hicho kitabu? “miachieni leo ili niweze kukiandaa kisha kesho nitakuja nacho hapa, na hukumu yangu itatekelezwa.” ni maneno ya tabibu kumwambia mfalme.


Basi mfalme akaamrisha askari wake wamlinde tabibu. Tabubu alipotoka pale akaenda nyumbani kwake na kuiaga familia yeke kwa uchungu na machozi ya hali ya juu. Baada ya pale akachukuwa hicho kitabu akakipaka dawa iliyo na rangi ya kijibu. Dawa hii ipo kama ungaunga, na haina harufu kali. Akakipaka kitabu kurasa zote. Ilipofika asubuhi akachukuwa beseni la maji lakini halikuwa na kitu ndani na akatoka kwake akiongozwa na askari wa mfalme. Alipofika sehemu ya hukumu akaanza kutoa maelekezo yake.


“nitakapokuwa nimeuliwa chukueni kichwa changu kisha kiwekeni juu ya kitabu kilichopo kwenye beseni hili. Pindi damu itakapoanza kutotesha gamba la nje la kitabu hiki mfalme atakichukuwa na kufungua mpaka ukurasa wa 6 wa kitabu hiki.” haya yalikuwa ni maelekezo ya tabibu kwa mfalme kuonesha maandalizi ya kitabu kitakachozubgumza. Basi haukupita muda dabibu akauawa kwa upanga.


Kwa shauku mfalme akafuata maelekezo kama alivyoambiwa. Damu ilipoanza kutotesha kitabu akakichukuwa kwa shauku kubwa. Akawa analamba kidole chake kutia mate ili afunguwe kurasa kwa urahisi, kichwa kikasema “funguwa mpaka ukurasa wa sita”. Akaanza kufunguwa huku anatia mate kidole na kisha nafungua, alifanya hivi mpaka akafika kurasa wa sita na hakukuta maandishi yoyote. Kichwa kikasema “fungua mpaka mwisho” akaendelea kufungua huku analamba kidole kutia mate, mpaka akafika mwisho na asione chochote.


Ghafla macho yake yakaanza kulegea na mwili ukaanza kupoteza nguvu, damu zikaanza kutoka puani, kisha kichwa kikaseme “na ukatili wako, haukujuwa kama ulikuwa ukilamba sumu iliyopo kwenye kurasa. Umebakiwa na muda mchache kufa. Hivi ndivyo watu waovu wanavyolipwa uovu.” baada ya maneno haya kichwa kikapoteza maisha na haukuchukuwa muda mfalme akafa huku anajuta kwa kumuua tabibu na kuamini maneno ya waziri wake.


Baada ya kumaliza kusimulia hadithi hii mvuvi akamwambia jini “kama mfalme angemwamini tabibu na kupotezea maneno ya waziri wake, haya yole yasingetokea. Hivi pia ndivyo itakavyokuwa kati ya mimi na wewe, nikikuamini nitajuta. Hivyo mimi nakutupa baharini sasa hivi na nitaweka alama na tangazo hapa ili kula mvuvi ajuwe kilichopo hapa nin nini. Na nitajenga na nyumba pia nitakaa hapa kuwaonya wavuvi.


Jini kusikia maneno haya akamwambia usinifanyie kama imma alivyomfanyia ateka. Mvuvi kwa shauku akauliza “kwani imma alinfanyia nini ateka?”. Jini likamjibu “unadhani nitakwambia wakati umenifungia humu?, nifungulie na nakuahidi nitakufanya tajiri maisha yako yote, nakuahidi”. Mvuvi kwa kupenda mali akakubali ahadi ya jini na akamfungulia, jini lilipotoka likapiga teke chupa ile na likacheka kwa sauti ya juu. Hali hii ilimuogopesha sana mvuvi. “usiogope rafiki yangu, nimefanya hivi kukutisha tuu, mimi naamini sana ahadi”. Ni maneno ya jini kumwambia mvuvi. Kisha akamwambia amfate na achuuwe na nyavu zake.


SAMAKI WA AJABU Walikwenda upane wa magharibu na mji wakauacha upande wa kusini. Walikwnda kwa muda usiopunguwa masaa saba. Kisha wakakutana na milima minne. Wakaipanda milima ile juu ya milima wakakuta kuna kijibwawa cha maji yaliyo meupe sana. Kisha jini akamwambia mvuvi atupe nyavu yake. Alipotupa akavuwa samaki wanne wa rangi tofauti. Mvuvi alishangaa hajawahi ona samaki wenye umbo na rangi kama hizi maishani kwakwe. Kisha jini likamwambia “chukuwa samaki hawa na ukawauze kwa mfalme, utapata utajiri bila shaka. Ila kumbuka utavua hapa kwa siku mara moja tu?” kisha jini likapiga miguu yake chini na kupotea.


Mvuvi akatoka na samaki wake wale na akakutana na mpishi wa mfalme, mpishi akawachukuwa samaki wale mpka kwa mfalme. Mfalme alishangaa uzuri ulioje wa samaki wale. Akawanunua kwa pesa nyingi sana iliyomfanya mvuvi asahau maisha ya kimasiki jitena. Mpishi akatoka kwendapika samaki wale. Akaanza kuwakaanga , pindi walipoanza kuiva, upande mmoja akawageuza ghafla akashangaa ukuta wa jiko umepasuka na kukatokea mwanamke mzuuri. Mwanamke yule akaaambia samaki “je mnafanye kazi niliyo watuma?” samaki wakamjibu “ndio tunafanya kaz” kisha mwanamke yule akapiga teke karai lile na samaki wakaanguka na kugeuka mkaa. Baada ya hapo akapoka na ukuta ukarudi ukawa kama vile ulivyokuwa.


Matukio yote haya yakifanyika mpishi aliyaona, na alikuwa akishangaa. Zaidi ni pale alipoona samaki wa mfalme wamegeuka mkaa, aliogopa sana na akatoka kumtafuta mvuvi ili amwambie amletee wengine. Kwa kuwa mvuvi aliwauza wawili akampatia wale wawili walobakia kwa pesa nyingi sana. Kisha mpishi akaenda jikoni. Tukio lielile likatokea tena na samaki wakageuka mkaa. Mara hii aliamua kumweleza mfalme mfalme alishangaa sana na kaamrisha aletwe mvuvi. Mvuvi alipofika akampewa amri ya kuleta samaki kama wale siku itakayofata.


Mambo yakawa kama hivi siku ilofata mvuvi akawaleta samaki wale na akapewa pesa kama ile ya jana mara mbili yake maana amempa wote wanne. Mfalme akaingia jikoni mwenyewe na akaanza kuwakaanga. Tukio kama la jana likatokea tena na samaki wakageuka mkaa. Sasa mfalme akaona hawa sio samaki wa kawaida. Akaagiza mvuvi aletwe. Alipokuja mvuvi akamweleza nataka unipeleke nikapaone hapo unapovua samaki hawa. Mvuvu akawaeleza ni bali lamda kwa kesho. Mvuvi alijitetea hivi akiogopa ahadi aliyoekeana na jini


Basi siku iliyofata mfalme akatoka na msafara wake kuelekea kule kwenye bwawa. Wakafika mida ya mchana, kwenye bwawa lililozungukwa na milima minne. Watu wote walistaajabu kuona bwawa likiwa milimani na lina maji masafi sana kiasi kile. Kila mmoja alitamani luyaonja maji yale. Ilipofika jioni mfalme akamwagiza mlinda mlango kuwa anatoka lakini asimwambie mtu yeyote. Na atakaemuuliza mwambie amesema hataki kusumbuliwa. Basi mambo yakawa kama hivi.


Usiku ule mfalme alitoka na upanga wake akiwa anazunguruka katika eneo lile, alikuwa akisaidiwa na mwanga wa mwezi ulioonekana unawaka sana. Katika kuzunguruka akaona kinjia kidogo kinaelekea upande wa ashariki kutokea kwenye ziwa. Akafata njia ile akakutana na bostani nzuri, yenye maua na matuta mazuri sana. Alistaajabishwa na bostani ile yenye vitu vizuri ambavyo kwenye ufalme wake havipo. Kwa sahuku aliendelea kuchunguza ndani mule kuona maajabu zaidi.


Kwa muda mrefu katika kuzunguka kwake alikutana na geti kubwa la rangi ya dhahabu, akaingia kupitia geti hili. Akakutana na njia iliyowekwa taizi za almasi. Alishangazwa na ururi ulioje wa njia hiyo. Mbele yake akakutana na kitu kizuri, kiti hiki kimenakshiwa dhahabu na fedha. Kuangalia vizuri akaona kwenye kiti kiel kuna mtu amekaa. Mtu huyu ni wa ajabu sana, alikuwa ni jiwe kwa chini mapaka kiunono. Kuanzia kiunini mpaka juu ni mtu aliye sawa.


Kwa shauku mfalme akataka kujuwa nini kunaendelea eneo lile. Akawa anamuuliza kuhusu yeye ni nani na anafanya nini pale. Na ni kipi kimetokea eneo lile. Maswali yote aliuliza bila ya kujibiwa. Kijana yule alikuwa anatokwa na machozi muda wote ule. Kisha kijana akaanza kuzungumza “hayo maji unayoyaona sio maji, na hao samaki unaowaona ni watu. Hiyo milima ni visiwa na mimi ndiye mfalme wa eneo hili” ni maneno ya kijana aliye jiwe nusu. Mfalme akauliza nini kilitokea sasa. Kijana akaanza kusimulia hadithi ya eneo hili kama ifuatavyo;-


HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE.
Baba yangu alikuwa ni mfalme wa eneo hili kwa muda usiopungua miaka hamsini. Alifariki akiwa na umri wa miaka 66, na baada ya kufariki kwake mimi nilichukuwa madaraka hayo. Nchi hii i;likuwa nzuri sana ilozungukwa na visiwa vinne ambavyo ndio milima unayoiona. Nilikuwa na mke wangu ambaye ni binamu yangu. Nilimpenda sana mke wangu na niliamini kuwa naye ananipenda kama ninavyompenda. Tuliishi hivyo kwa muda wa miaka kadhaa bila ya kuona mabadiliko yoyote katika mapenzi yetu.


Ilitokea siku moja nilipokuwa nipo kati ya kulala ama kusinzia (mang’amung’amu ya usingizi), vijakazi wawili wa mkewangu wakawa wananipepea. Nikawasikia wanazungumza “namuonea huruma mfalme, anampenda sana mkewe lakini mkewe hampendi, anampenda mtumwa wake.” ni maneno ya mmoja wa wale wajakazi. Mwingine akadakia “yaani anatamani hata amuuwe, na vile anajuwa ucha wipo siku atamuuwa tu”. Wajakazi hawa wakati wanazungumza walidhani nimelala, kumbe nimeyasikia vizuri maneno yao.


Siku ilofuata nikaanza kufanya uchunguzi wa maneno yale. Niligunduwa kuwa ni ya ukweli kama walivyosema wale wajakazi. Hivyo nikamchukuwa yule mtumwa na kuanza kumwadhibu. Kwa bahati mbaya wakati wa kumwadhibu alipigwa vibaya na akapoteza fahamu. Yule mke wangu alikasirika sana na akamtibu lakini bia ya mafanikio. Alifanikiwa kumueka hai, yaani anafahamu lakini haweza kufanya chochote. Mwanamke yule kwa hasira alizonzo wakati ule aliondoka kwa muda na nisijuwe wapi alipokwenda.


Baada ya muda akarudi, na akachukuwa kifuu cha nazi na akaweka maji, kisha akazungumza naneno ya ajabu akamwaga juu. Visiwa vilivyouzunguka mji huu vikawa milima hiyo unayoiona na mji yakiwemo maduka na vinginevyo ukawa bwawa la maji hayo unayoyaona na watu wakageuzwa kuwa samaki hao wa rangi nne unaowaona yaani hizo rangi za samaki ni aina za watu walokuwepo eneo hili. Baada ya kufanya hayo na mimi akanimwagia maji nikawa kama hivi unavyoniona. Haikuishia hapo kila siku anakuja kunitandika mijeledi ya ngozi ya kifaru. Hunitandia kadri anavyotaka kisha huondoka. Hii ndiyo historia yangu na mji huu.


Kijana alimaliza kusimulia hadithi ya nchi yake, mfalme alipatwa na uchungu sana wakati akisikiliza maneno yale. Chozi lilikuwa likimtoka kwa huruma na majonzi. Kish akauliza mahala alipo huyo mwanamke. Kijana akamjibu kwa kumwambia kuwa yeye hajui alipo isipokuwa kila siku jioni baada ya kuniadhibu huenda upande ule (akaelekeza kwa kidole upande wa kusini). Mfalme alikwenda kule alikoelekezwa na kumkuta mtumwa ambaye ni mgonjwa. Akarudi kwa kijana na wakapanga mbinu yako, kisha wakakubaliana watekeleze kesho mpango wao.


Basi mambo yakawa kama walivyokubaliana, siku ilofata mfalme akachukuwa upanga wake na akaunoa safi. Akaenda kwenye lile jumba lenye yule mtumwa mgonjwa. Alipofika akamkata upanga na kummalizia uhai wake, kisha akamuingiza kwenye kisima cha maji. Baada ya hapo akajilaza pale kwenye kitanda kama vile yeye ndiye mgonjwa. Yule mwanamke kama kawaida yake alipokuja siku ile akamuadhibu yule kijana kisha akaelekea kule kwenye mgonjwa wake. Alipofika akamwuliza “u hali gani wangu? Vip tafadhali naomba zungumza nami japo neno moja tuu”. Mfalme alojilaza pale kama yeye ndo mgonjwa akamjibu “sina raha kwakweli” “mmmh utamu ulioje leo kusikia sauti yako. Hebu niambie kipi kinachokukosesharaha jama”. Ni maneno ya yule mwanamke. Mfalme alojifanya ndo mgonjwa akajibu “hiyo sauti ya mumeo inanipa taabu, hebu mrudishe katika hali yake ya kawaida na aondoke hapa”. Basi kusikia hivyo yule mwanamke akatoka na kwenda kuchukuwa maji akayasemea maneno flani kisha akamwagia yule kijana na hapohapo akarudi katika umbo lake. Kisha akamwambia uondoke na nisikuone tena eneo hili, sihivyo nitakuuwa.


Yule kijana alijifanya anaondoka na akajificha ili ashuhudie kinachoendelea. Basi huku yule mwanamke akaelekea kule moyo wake ulipozama, alipofika akamuliza mtumwa wake “nimesha fanya utakavyo, vipi unajisikia amani sasa ?” yule mfalme alojifanya mgonjwa akamwambia hapana, hizo sauti za watu ulowageuza samaki zinanipa shida usiku. Hebu warudishe katika hali yao ya kawaida pamoja na mali zao”. Yule mwanamke akatii an kutoka akazungumza maneno yake ya kichwawi na mji ukabadilika kama ulivyo zamani. Wale watu wa mfalme walokuja kuchunguza samaki walishangaa kujikuta wapo katikati ya mji.


Yule mwanamke mchawi akaenda kwa mtumwa wake. Akamuuliza haya sasa bilashaka umeridhika. Yule mfalme alojifanya mgonjwa akamwambia “sogea hapa karibu” mwanamke akasogea zaidi yule mfalme akachukua upanga na kumkata vipande viwili. Hna huo ukawa ndo mwisho wa mchawi huyu. Mfalme akatoka na kukutana na kijana. Waliflai sana na kuzungunza mengi zaidi kuhusu eneo lile lenye mali mengi na utajiri wa kutosha.


Yule mfalme akamwambia kijana “nimeflai sana, na kwakuwa tupo majirani zaidi tutakuwa ndugu”. Kijana alicheka sana kwa fyraha na mshangao. Kisha akamwambia yule mafalme “kutoka hapa mpaka kufika kwenye utawala wako ni mwendo wa mwaka mmoja. Uliweza kutumia masaa machache kwa sababu eneo hili lilifanyiwa uchawi kama ulivyoona. Basi kijana akamwahidi atamsindikiza wakati wa kurudi mpaka kwake. Mfalme aliflai sana na akamwahidi kumfanya mrithi wa utawala wake kwani yeye hakuwa na mtoto wa kumrithisha.


Basi mambo yakawa hivyo, na safari ilikuwa ni nzuri ya ya furaha zaidi. Wafalme hawa walizungumza mengi na kucheka utadhani mtu na mwanae. Walibeba zawadi nyingi na mali nyingi kutoka ufalme ule tajiri. Walipofika walizigawa mali zile kwa viongozi kulingana na vyeo vyao. Mfalme aliitisha mkutano mkubwa sana siku ilofata na akatangaza nia yake ya kutaka kumrithisha ufalme kijana yule na kumfanya kuwa ni mtoto wake. Basi mambo yakawa kama hivyo,


Nchi ilikuwa katika hali ya furaha sana kwa muda mrefu. mfalme alikuwa katika furaha kubwa zaidi kwa kupata mtoto na mrithi wa utawala wake. Yule mvuvi ambae ndio chanzo cha yote haya alipewa mali nyingi sana za kuweza kutumia yeye na vizazi vyake vingi vijavyo na akamfanya katika watu wake wa karibu. Kufikia hapa Dinar-zade akamaliza hadithi ya mvuvi. Hadithi hii mpaka kwisha ilichukuwa siku nyingi kwa mfale mpaka akalowea na hadithi. Dinar-zade aliponyeka kuuliwa kama hivi ikawa ikiisha hadithi analeta nyingine. Hivyo akaendelea kusimulia hadithi iliyonzuri kuliko hii ya mvuvi nayo i hii;-



Pata kitabu Chetu Bofya hapa
  1. 1
  2. 2

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela1 Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 2848


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

SAFARI YA NNE YA SINBAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA NNE YA SINBAD Basi ikafikia siku ya kuanza safari yangu ya nne ya kibiashara. Soma Zaidi...

HADITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE
Download kitabu Hiki Bofya hapa HDITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE. Soma Zaidi...

HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE. Soma Zaidi...

Safari ya tano ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Alif lela u lela: utangulizi
Katika nchi za China, Hindi, Uarabuni na Uajemi alikuwepo mfalme aliyefahamika na kuheshimika sana kwa uhodari wake na utawala wake mzuru. Soma Zaidi...

SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI. Soma Zaidi...

Hadithi ya jini na mfanya biashara
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

HADITHI YA MZEE WA PILI NA MBWA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MZEE WA PILI NA MBWA WAWILI WEUSI. Soma Zaidi...

HADITHI YA MWEN YEKUTABIRIWA MTOTO WA TAJIRI
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITI YA MWENYE KUTABIRIWA MTOTO WA TAJIRI Kwanza tambua ewe ndugu yangu kuwa mimi ni mtoto wa tajiri mkubwa sana katika nchi yetu hii. Soma Zaidi...

HADITHI YA MKE NA KASUKU
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MKE NA KASUKU. Soma Zaidi...