Navigation Menu



HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA MFANYABIASHARA NA JINI

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA MFANYABIASHARA NA JINI

mfanyabiashara na jini

By Rajabu Athuman

MFANYABIASHARA NA JINI

HADITHI YA JINI NA MFANYA BIASHARA.
Hapo zamani kulikuwa na mfanya biashara aliyejulukana kwa utajiri mkubwa sana wa mali na watoto. Alifahamika nchi nzima na aliishi maisha ya upendo na familia yake. Alitoka sikumoja katika safari zake za kibiashara. Alikuwa amepanda farasi akiwa na mfuko uiojaa tende na maji. Alifanya biashara kwa raha na amani na kuanza kurejea baada ya miezi miwili.


Siku ya nne baada ya kuanza safari ya kurudi alpita katika jangwa lililofahamika kwa jina la uwanja wa ujinini. Jina hili lilitumika miaka mingi iliyopita na huenda sasa limesahaulika. Mfanyabiashara huyu alipopita eneo hili akaona kuna mti wenye kivuli, hivyo akaamua kuketi ili apate kula chakula. Hivyo akawa anakula tende na kutupa punde pembeni. Alifanya hivi mpaka alipo maliza kula. Karibia na mti ule kulikiwa na kijieneo chenye maji hivyo alipomaliza kula tende zake akanawa mikono na akaswali swala zake.


Wakati yupo pale ghafla kulitokea upepo mkali sana na kimbunga, vumbi lilitanda eneo lile. Upepo uliambatana na moshi kisha kukatokea jini kubwa sana. “NITAKUUWA KAMA ULIVYOMUUWA MWANAGU” ni maneno ya jini yaliyosikika yakimwambia mfanya biashara. Nimefanya nini mpaka ninastahili kuuwawa?” mfanyabiashara akimwambia jini. Jini likaendelea “chagua nikuuwe namna gani.… Wakati ulipokuwa unakula tende zako ukawa unatupa punje na mwanangu alipita eneo lile ukampiga na punje yako akafa papo hapo. Hivyo lazima nikuuwe kama ulivyomuuwa mwanagu”


Mfanyabiashra akaendelea kumuomba jini msamaha “nisamehe mkuu, sikukusudia kumuuwa mwanao” jini kwa hasira likawa linajibu, “hakuna msamaha wala huruma hapa nitakuuwa kama ulivyomuuwa mwanangu”. Jini likatowa upanga wake kuuweka tajari kwa ajili ya kumuuwa mfanya biashara.


Mpaka kufika hapa Schehra-zade aligunduwa kuwa asubuhi imefika tayari na sultani anatakiwa akaswali na akahudhurie kikao cha baraza. “…. Mmmh ni hadithi nzuri sana dada nimeipenda kweli, hivi mwisho wake utakuweje?, mfanyabiashara atauliwa, au jini litamsamehe?” ni maswali aliyokuwa Dinar-zade akimuuliza dad yake Schehra-zade. “mmh ni nzuri kweli na bado huko mbele ni nzuri zaidi kama sultani ataniruhusu niishi ili kesho nikusimulie muendelezo wa hadithi hii” Schehra-zade alikuwa akimjibu mdogo wake. Sultani akamruhusu asiuliwe ali aje kuimalizia hadithi yake nzuri.


Siku ile sultani alitoka akiwa na tabashahsa na hata waziri wake alishangaa kuona sultani ametoka akiwa na tabasamu bla ya kutowa amri ya kumuuwa Schehra-zade kama ilivyo kawaida yake. Sultani alifanya kazi zake za kawaida huku akiwa na shauku la kutaka kujuwa mwendelezo wa kisa cha jini.


Usiku uliingia na ilipokaribia alfajiri, sultani hakusubiri akamwambia Schehra-zade “maliza mwendelezo wa hadithi yako, ninashauku la kuta kujuwa mwisho wake”. Basi Schehra-zade akaanza kusimulia kama ifuatavyo;-


Basi yule mfanya biashara alivyoona jini anakaribia kumkata upanga akapiga magoti na kumwambia jini “tafadhali mkuu nina neno naomba unisikilize, nina familia mkuu na nina madeni naomba unipe muda angalau nikaiage familia yangu na kulipa madeni yangu”. “Unataka nikuachie ili ukimbie?” ni jini akimjibu mfanya biashara. “hapana na ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa nitarejea hapa hapa, naweka ahadi mbele ya Mwenyezi Mungu” haya maneno aliyasema mfanya biashara.


Baada ya kufikiri jini likamuuliza “haya ni muda wa siku ngapi nikupe” naomba unipe mwaka mmoja” akamjibu. Basi jini lile likakubali kichukuwa ahadi ile na likamwacha mfanya biashara papepale na likotoweka. Mfanya biashara akaondoka akiwa na mjonzi makubwa. Alipofika kwake akaieleza familia yake yote yaliyompata.


Hakuwa na muda wa kupoteza akalipa madeni yake na kuweka akiba ya kuweza kutumiwa na familia yake pindi atakapo ondoka. Mwaka haukuwa mrefu hatimaye miezi 12 ikawadia. Mfanya biashara kwa majonzi na masikitiko akaaga familia na akaondoka kwenda kutekeleza ahadi yake. Alifika eneo la tukio na kumsubiri jini aje.


Katika hali kama hivyo akiwa amekaa kumsubiri jini katokea mzee mmoja akiwa na mbuzi wake. Alistaajabu mzee yule kuona mtu eneo lile hatari. Akmuuliza hasa yaliyomkuta kukaa eneo lile, akampa kisa kizima. Kiasha yule mzee kamwambia “nitakaa hapa hapa na mimi nishuhudie kitakacho tokea”. Punde akatokea mzee mwingine akiwa na mbwa wawili weusi. Naye akataka habari ya kilichowakuta wenzie wale mpaka wakakaa pale. Akasimuliwa kisa kizima, na yeye akabaki pale ili ashuhudie kitakacho endelea. Akaja mzee wa tatu akiwa na mbwa wake mwekundu na akapewa habari na akakaa ili aone kitakacho endelea.


Punde wakaona moshi uliofatana na upepo na likatokea jini kubwa lililoshika upanga mkononi mwake. Jini lile haliku msemesha yeyoye likamfuata mfanya biashara na kumwambia “simama ili nikuuwe kama ulivyo muuwa kijana wangu sasa hivi sina huruma leo”.


Pale yule mzee mwenye mbuzi akajitupa miguuni mwa jini kisha kwa hisia kubwa kamwambia “ewe mkuu wa majini wa eneo hili, naomba usikiklize hadithi yangu na huyu mbuzi nilyekuwa naye hapa. Kama utaiona inastaajabisha kuliko tukio hadithi ya mwanao na mfanya biashara huyu, iwe kama fidia ya kupunguzia adhabu:. Jini lifafikiri kwa muda na kisha likasema “vizuri sana ebu tuangalie hadithi yako”. Basi mzee yule akaanza kusimulia hadithi yake kama ifuatavyo;- HADITHI YA MZEE WA KWANZA NA MBUZI WAKE.
Mkuu sasa nakwenda nakwenda kukuhadithia habari ya ngu na huyu mbuzi niliye naye. Kwanza tambua huyu mbuzi unayemuona hapa ni mke wangu wa ndoa niliyeishi naye kwa muda wa miaka 30 bila ya kupata mtoto. Pale nyumbani kulikuwa na mtumwa hivyo nikamfanya mwanangu kwa maandishi.


Mke wangu kumbe kitendo hiki hakukipenda kitendo kile. Nilitoka kwa ajili ya shughuli za kibiashara huyu mke wangu alijifundisha uchawi na akambadili mtoto wangu na mama yake kuwa ng’ombe. Kisha akawapeleka kwa mfanya kazi wangu wa shambani ili awalishe na kkuwatunza.


Haikupita muda nikarudi kutoka safarini kwangu, na nikamuuliza kuhusu mtoto wangu na mama yake lakini akanijibukuwa mama wa mtoto wangu amefariki inapata miezi miwili sasa. Na kuhusu mtoto wangu ametoweka nyumbani na hafahamiki alipo. Jambo hili lilinishangaza sana lakini sikuwa na la kufanya zaidi ya kumtafuta bila ya mafanikio.


Ulipofika msimu wa sikukuu nilimwambia mfanyakazi wangu aniletee ng’ombe aliyenona ili nimchinje kwa ajili ya kusherehekea sikukuu. Nililetewa ng’ombe mmoja mzuri sana mwenye afya. Jambo lililonishangaza wakati nataka nimchinje ng’ombe huyu alikuwa akitoa machozi na akiniangalia kwa huruma. Kwakweli jambo hili halijawahi kutokea. Nikaagizwa arudishwe na niletewe mwengine.


Mkewangu alikasirika kuona ng’ombe anarudishwa, akanifata na kunisisitiza nimchinje. Nikamweleza mfanyakazi wangu amchinje yeye mii siwezi. Basi akamchinja ng’ombe yule. Jambo la ajabu ni kuwa ijapokuwa ng’ombe yule alikuwa amenenepa lakini hakuwa na nyamba ila ni mifupa mitupu. Nilishangazwa sana. Nikaagiza niletewe mwengine, na akaletwa ndama mmoja aliyenenepa vizuri. Huyu pia alifanya kama yule wa mwanzo alikuwa akitowa machozi na akajilaza miguuni mwangu kama anaomba aachiwe asiuliwe.


Huruma ilinijaa na nikaamua aondolewe aletwe mwingine. Mke wangu akanilazimisha ili nimchinge. Nikamuweka vizuri ili kuanza kumchinja, niliweka kisu kooni na nilipokaribia kumchinja aliniangalia kwa jinjo la unjonge na huku akitowa machozi. Kisu kilianguka na nikashindwa kumchinja. Nikaagiza arudishwe. Mke wangu alikasirika sana lakini mara hii sikubadili kauli yanngu


Siku ilofata mfanyakazi wangu alinifata kwa mazungumzo ya faragha akanieleza kuwa binti yake ana taaluma ya uchawi hivyo anataka kuzungumza na wewe faragha. Ilibidi nikutane nae, mazungumzo yake yaninistaajabisha sana. “mkuu ulipoondoka mkeo alijifunza uchawi na akambadili mtoto wako na yule mama yake kuwa ng’ombe. Yule ulomchinja jana ni mama yake na yule ng’ombe mdogo ulomrudisha ndiye mwanao. Nitaweza kumrudisha mwanao kawaida kwa masharti, kwanza uniwachie mkeo nimpe adhabu, na pili uniozeshe mwanao.” haya yalikuwa maneno ya binti wa mfanyakazi wangu. Nilikubaliana na masharti yale.


Yule binti akachukuwa maji na akatamka maneno nisiyoyajuwa kisha akammwagia yule ng’ombe, papo hapo akawa katik umbo labinadamu. Nilifulahi sana. Kama mashart tulokubaliana alimfata mke wangu na kutamka maneno flani na mke wangu akageuka kuwa mbuzi huyu ambaye unamuona.


Ni muda mrefu sasa hatujaonana na mwanangu hivyo nimetoka ili kama nitaweza kupata taarifa zake zozote. Hivyo nimeona ubaya kumuacha mke wangu huyu mbuzi chin ya uangalizi wa watu wengine. Nikaona bora nimchukuwe. Hii ndio stori yangu ewe mkubwa katika majini.


“naam nakubaliana na stori yako, kweli inasikitisha hivyo nitampunguzia adhabu huyu mtu” ni maneno ya jini akimwambia mzee wa kwanza. Baada ya huyu mzee wa kwanza kuzungumza, mzee wa pili akapiga magoti kwa lile jini akaliambia, “ewe mkuu katika majini naomba usikilize na mimi stori yangu na hawa mbwa wawili, kama utaona inasikitisha zaidi naomba umpunguzie adhabu huyu mtu”.


HADITHI YA MZEE WA PILI NA MBWA WAWILI WEUSI.
Mzee wa pili akapewa ruhusa ya kusimulia stori yake na mbwa wawili weusi. “kwanza utambue ewe mkuu wa majini kuwa hawa mbwa unaowaona ni ndugu zangu wa baba na mama mmoja, stori ilikuwa hivi”


Baba yety alikuwa ni tajiri mkubwa katika mji tuliokuwa tukiishi. Alipofariki alituachia mali kubwa na tukaigawa mafungu matatu kulingana na idadi yetu. Tuligawana sawa kwa sawa. Ndugu zangu hawa wakajikita kwenye biashara za nje na ndani ya mji. Wakawa wanasafirisha bdhaa kwenda miji mbali mbali, na hata kwenye visiwa.


Mimi niliamua kufungua duka hapa mjini na kwa neema za Allah biashara ikawa nzuri. Mali yangu ilifikia mara tatu ya ile niliopata kutoka kwenye urithi. Sikumoja ndugu zangu walitoka kibiashara, walikaa kwa muda wa miezi isiyopunguwa miwili. Baada ya hapo nikaona kuna watu wawili wamesimama mbele ya duka langu. Sikuwatambuwa watu hawa kutokana na mavazi yao. Walikuwa wamevaa mavazi yaliyochakaa ama yaliyookotwa jaani. Niliataajanu kuona wana nifahamu, baada ya kuzingatia zaidi nikagunduwa ni ndugu zangu.


Nikawapa mavazi na chakula kisha wakanihadithia mkasa wao. Walikuwa wamepata ajali na malizao zote zimetokomea majini. Nikachukuwa ile faida yangu na nikaigawa sasa kwa sawa kati yao. Wakaanza biashara tena na hawakukoma baada ya muda wakaamua kusafiri tena kibiashara. Hali ilikuwa mbaya zaidi wakati huu. Walipata ajali tena majini na wakktupiwa nchi kavu wakuiwa hata mavazi hawana.


Niwalipfika nyumbani sikuwatambuwa kwa kuwa walikuwa uchi na wakiwa wamechafuka ngozi zao. Wakajitambulisha na niliilia kwa huruma. Machozi yangu nhayakufaha kitu kwa kuwa tayari jambo lilisha tokea. Kama mara ya kwanza nikawapa mtaji na wakaanza upya biashara zaoi. Baada ya muda biashara zao zikakaa vizuri, na wakaamuwa kutoka tena kibiashara. Ila mara hii walitaka niende pamoja nao. Nilipinga zaidi safari hii lakini walinilazimisha na hata maandalizi pia wakanifanyia.


Sikuwa na jinsi nikajiandaa na mimi kwa safari. Nikachukuwa mali zangu nikazigawa sehemu mbili na sehemu moja nikachukuwa na nyingine nikaificha. Safari ilianza vizuri na tulifika miji mbalimbali tukifanya biashara. Nilipata faida kubwa na nikanunuwa baadhi ya bidhaa ambazo ningeziuza pindi nitakapo rejea.


Muda wa kurudi uliwadia tukawa tunaanda safari ya kurudi. Nilipokuwa matembezini nikitafuta bidhaa na zawadi za kwenda nazo nyumbani, nilipita ufukweni nikakutana na mwanamke aliyevaa mavazi yaliyo chakaa. Nilimsalimia na akarudisha salamu, nikamchukuwa na kumtafutia mavazi yaliyo mazuri. Kwa mavazi yale uzuri wake ulidhihiri mbele yangu. Kwakuwa sikuwa na mke ilibidi nifuate taratibi za kufunga nae ndoa na akakubali. Maandalizi yote yalipoisha nilimchukuwa mke wangu kurudi nae nyumbani.


Tukiwa kwenye jahazi zikugunduwa kumbe ndugu zangu walikuwa wananionea wivu. Wakawa wananipangia njama ya kuniuwa. Ulipofika usiku walinichukuwa na kunitumbukiza majini. Baada ya pale sikujuwa kilichoendelea nikajikuta nipo nchi kavu. Mke wangu akanieleza khabari za yote yaliyotokea na akanieleza kuwa yeye si mtu wakawaida. Akaniambia pia hatoweza kuwasamehe ndugu zangu kwa walichonifanyia. Nilimuomba asiwaue ila nipo radhi kwa adhabu yeyote ile.


Alinichukuwa mpaka nyumbani kwangu, kisha akalizamisha jahazi waliopanda ndugu zangu. Mali zangu zote akaziokoa. Siku iliyofata nikiwa nyumbani nikaona kuna mbwa wawili weusi wanakuja huku wakionesha majonzi na hali ya kuomba msamaha. Nilistaajabishwa na tukio hili. Haukupita muda mke wangu akatokea na akaniambia hawa ni nduguzangu amewapa adhabu hii. Watakuwa hivyo kwa muda wa miaka 10.


Miaka 10 sasa imefika, na kwakuwa alinielekeza sehemu ya kukutana, ndio nimetoka kuelekea hapo sehemu. Nikaona niwachukuwe ndugu zangu kwa kuhofia kuwaacha kwa mtu asie akawadhuru.


Hii ndio stori yangu na mbwa hawa ewe mkuu wa majini. “hii ya kwako inamakubwa zaidi” ni maneno ya jini. Baada ya hapo mzee wa tatu akazitupa miguuni kwa jini na kutaka ruhusa aruhusiwe kughadithia stori yake ili iwe ni kafara ya kuachiwa huru mfanya biashara. Lile jini likasema “hapana nimetosheka na hizi mbili, na nimekubali kumuacha huru mfanya biashara” jini lilizungumza maneno haya na kuondoka.


Mfanya biashara akawashukuru wazee wale. Basi wakati wazee wale wapokaribu na kuondoka yule mfanya biashara akamuuliza mzee yule wa tatu mwenye mbwa mwekundu kuhusu habari ya mbwa yule. Mzee akamwambia ni stori ndefu ila kwa ufupi huyu ni mke wangu. Akaanza kusimulia hadithi yake kwa ufupi huku akiwa na haraka ya kutaka kuondoka eneo lile


HADITHI YA MZEE WA TATU NA MBWA WAKE MWEKUNDU
Kama nilivyotangulia kusema , huyu ni mkewangu wa ndoa tulioishi pamoja kwa muda wa miaka zaidi ya kuni na tano sasa.mkewangu nilimpenda sana. Niliamini ananipenda sana pia. Bila ya kujua kinachoendelea kumbe alikuwa anajiiba na kuzini na moja ya watumwa wangu pale ndani. Ilichukuwa muda mrefu mpaka nilivyogundu tabia hii mabya ya mkewangu.


Basi siku moja nikaaga safari ya dharura lakini lengo langu nilitaka nimtegee ili nimkamate. Niliondoka nyumbani vizuri lakini nikarejea nyumbanni usiku ule na kumkuta mke wangua na yule mtumwa wakiwa wanafanya madhambi. Hali ile iliniumiza sana. Lakini mkewangu hata bila ya aibu akachukuwa maji na kuyasemea maneno ya kichawi na kunimwagia usoni. Hapo nikaanza kuunguwa mwili mzina na hatimaye nikabadilika kuwa mbwa.


Basi nilipojiona nimekuwa mbwa nikaondoka pale ndani na kuenda kwenye duka la mfanya biashara mmoja. Yule mfanya biashara akawa ananionea huruma kulikuwa na mbwa wengine wanataka kunipiga basi yule mfanya biashara akawa ananigombea. Ulipofika muda wa mchana binti yake mfanya bishara akaja kumletea chakula baba yake. Ghafla tu macho yangu na ya yule binti yalipo kutana nikahisi hali flani ya mabadiliko usoni kwa yule binti.


Baada ya mfanya biashara kual akanipatia mabaki yale ya chakua na kunipatia. Yule binti akamuuliza baba yake “baba umepata wapi mbwa mzuri huyu?”. “hapana amekuja mwenyewe hapa”. Basi binti akamwambia baba yake “baba uanjuwa huyu sio mbwa wa awaida, huyu ni binadamu aliyegeuzwa mbwa” niliposikia maneno yale nikawa natingisha kichwa isara ya kuyaunga mkono maneno yale. “sasa unaweza kumrudisha katika hali ya kawaida?” aliuliza mfanya bishara. “ndio baba naweza” ni majibu ya binti. Basi binti akachukuwa maji na akayasemea maneno yasiyo eelweka na kunimwagia usoni. Palel aple nikawa katika umbo la kawaida. Kisha akamwendea mke wangu na kumgeuza kuwa mbwa kama alivyonifanya mimi. Kisha akanielekeza sehemu ya kukutana nae itakapofika miaka 10. Hivyo miaka 10 sasa imefika ndio niko safarini kukutana nae ili amrudishie mke wangu umbo lake mwenyewe. Ndio nikakutana na nyinyi hapa. Basi waztu wote wanne wale wakaachana pale na kila mmoja akaenda na safari zake.


Baada ya kumaliza hadithi hii Schehra-zade akamwambia mdogo wake “vip unaionaje hadithi hii” “mmmmhmmh … Ni nzuri sana dada, ila ni ipi hadithi ya yule mzee wa tatu”? Ni maneno ya Dinar-zade. “hata mimi sijui ila naamini ni nzuri zaid, lakini haiwezi kushinda hadithi ya mvuvi na jini” alisikika Schehra-zade akimweleza mdogowake. Sultani akadakia “ooh, kama hii nzuri hivi vp hiyo ya mvuvi na jini, natamani kuisikiliza,” Schehra-zade akaongea “kama utanipa siku nyingine zaidi naamini utaflaiya hadithi hii”. Basi siku ile Schehra-zade hakuuliwa na siku ilofata mfalme akamuleza asimulie hadithi ya mvuvi na jini. Schehra-zade bila ya kuchelewa kaanza kusimulia kama ifuatavyo



Pata kitabu Chetu Bofya hapa
  1. 1
  2. 2

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela1 Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 3584


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA SAFARI SABA ZA BAHARIA SINBAD
SAFARI SABA ZA SINBADKatika nchi ya Baghdad kulikuwepo na kijana aliyejulikana kama Sinbad mbeba mizigo. Soma Zaidi...

Kisa Cha mfugaji na mkewe
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Kitabu Cha hadithi ya Chongo
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Hadithi ya chongo watatu wa mfalme na wanawake wa Baghdad
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

MFUGAJI NA MKEWE
Download kitabu Hiki Bofya hapa KISA CHA MFUGAJI NA MKEWE. Soma Zaidi...

Hadithi ya tabibu wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

HADITHI YA BINTI WA KWANZA NA MBWA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA BINTI WA KWANZA NA MBWA. Soma Zaidi...

NDOA YA SINBAD NA BINTI WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa NDOA YA SINBAD NA BINT MFALME. Soma Zaidi...

Safari ya saba ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

SAFARI YA SITA YA SINBAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA SITA YA SINBAD. Soma Zaidi...