Navigation Menu



HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MLEVI MBELE YA SULTANI

HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MLEVI MBELE YA SULTANI

Hadithi aliyosimuliwa Sultani na Mlevi

bongoclass-burudani

HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MLEVI MBELE YA SULTANI

HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MLEVI MBELE YA SULTANI
Tambua ewe Sultani muadilifu wa Baghdad mwa na wa Rashidi utambulikae kwa Harun, tambua kuwa mimi ni mzaliwa wa Misri na huku nimefika tu kwa sababu za utafutaji wa riziki. Baba yangu alikuwa ni mfanyabishara mzkubwa sana huko misri. Alijulikana sana katika miji na hata viji na nchi za majirani ya misri. Nilikuwa nikishiriki biashara na baba yangu toka nilipokuwa mdogo.


Hatimaye Mwenyezi Mungu akamchukuwa baba yangu na hapo mimi nikarithi kazi ya baba. Katika familia nipo peke yangu na mama yangu alishafariki zamani sana nikiwa mdogo. Nilifanyabiashara misri. Biashara yangu kuu ilikuwa ni kuuza kanzu. Nilikuwa nikizipaka manukato mazuri hata zikawa zikinukia sana na kumvutia mpita njia.


Watu walipenda sana biashara yangu na jina langu lilikuwa hata kumzidi baba yangu. Ila katu sikuweza kusafiri kibiashara kama alivyokuwa akifanya baba yangu. Niliweza kutengeneza chaneli za kibiashara wakawa wafanyabiashara wadogowadogo wanachukuwa mzugo kutoka kwangu. Kwa hakika biashara ya kanzu ilikuwa ikinilipa vyema. Kipindi chote hiki sikuwa mwenye kuoa.


Ilitokea siku moja akaja mtu mmoja na kuulizia bei ya kanzu. Badala ya kumtajia akanipatia kiasi kikubwa cha fedha na kunieleza nimpelekee mzigo wake sehemu ambayo alinitajia. Haikuwa ni kazi nzito kwani ni katika majukumu ya kazi yangu. Nilipomaliza maandalizi nikampelekea mzigo wake. Alipouona akanieleza kuwa nimuuzie mzigo ule pale kwake na faida yeyote nitakayoipata tutagawana.


Kwa uchu wangu wa pesa nikakubali. Yule bwana akaniaga safari ila akanieleza nimtunzie pesa yake mpaka atakapo rejea. Mambo yakawa hivyo nilimaliza kuuza mzigo na nilipata faida kubwa sana. Yule bwana baada ya mwezi akaja na kuniulizia pesa yake. Nikamueleza kuwa ipo salama. Basi akanieleza nimtunzie hadi atakaporudi tena.


Baada ya mwezi akarejea, na kuniambia kuwa ana shughuli nyingi, baada ya kumaliza atakuja kuchuuwa pesa yake. Alipoondoka akakaa kiasi cha mwezi. Hata aliporudi alikuwa mapendeza sana. Alifaa nguo nadhifu na za kupendeza.. alipokuja akanieleza ataondoka tena ila akirudi atachukuwa pesa yake. Mimi nikajiapiza kuwa pindi akija nitamkirimu kama mgeni wa heshma.


Safari hii alikaa kama mwaka hivi na aliporudi akaulizia pesa yake nikamueleza kuwa ipo salama. Basi nikamuomba awe mgeni wangu kwa siku ile na akakubali kwa sharti kuwa matumizi nitakayotumia yasiwe katika ile pesa yake. Nikakubali, baada ya muda kikaletwa chakula safi sana. Nikamnawisha kisha akanawa mgono wa kushoto. Nilistaajabu sana. Apilpoanza kula akala kwa mkono wa kushoto.


Nilistaajabu sana kwa mtu mtanashati na msafi kama huyu alafua anakula kwa shoto. Tulipomaliza kula akanywa maji kw ashoto. Basi baada ya chakula tukaanza kuzimulia za hapa na pale. Ndipo nikamuulza anitoe mashaka kuhusu kula kwake kwa shoto. Huenda ana ugonjwa ama ameumia ama anafanya masifa. Ndipo akatoa mkono wake. Looo! Mkoni wake ni kugupu aani ni kiwete ana mkono lakini kiganja kimekatwa.


Baada ya hapo akanieleza kuwa si kama ametaka kula na kushoto ila kuna sababu ilopelekea hali hiyo. Basi kwa udadisi niauiza kuhusu chanzo bila kusita ndipo akaanza kuzimulia hadithi yake na kukatwa kwa mkono wae:-



HADITHI YA KILEMA, MTANASHATI ASIYE NA MKONO
Basi tambu kuwa mimi ni Mtu wa Baghadad na ni mtoto wa aliyekuwa mfanyabishara mkubwa sana. Nilipokuwa mdogo nilisikia wafanyabiashara wakitoa sifa kemkem kuhusu miji ya misri na uzuri wake. Walikuwa wakisifia jinsi mto Nile unavyokwenda kwa kasi na kupendezesha macho. Majumba makubwa ya wafalme na mafarao wa Misri. Hawakuacha kusifia uzuri wa masoko na mabinti wa Misri.


Basi wakati alipofariki baba yangu mimi nikawa ndiye msimamizi wa mali zake. Katika familia yetu nilikuwa peke yangu yaani sikuwa na mama wa la baba na nilizaliwa peke yangu. Basi niliendelea kukuza biashara aliyoiacha baba yangu. Na ilikuwa ni kuuza kanzu pamoja na nguo za kike. Nilikuwa nikiuza vitamaa vya kujifunika kwa wanawake ambavyo vimechovywa na dhahabu pamoja na kuwekewa haririri.


Watu walipenda sana aina za mavazi nilizokuwa nikiuza.nilibahatika kupata wateja wa jumala na rejareja. Sifa za nguo zangu zilienea bara la arabu hata zikafika Misri. Niliweza kupata wateja wa kike na kiume. Niliongeza ujuzi wa kuchovya nguo zangu na marashi pamoja na mafuta ya miski. Kwa hakika hazikuisha kunukia katu.


Sikumoja walipata kunijia wafanyabiashara wa kutokea misri. Walikuwa wakitoa sifa nyingi sana. Hata nikavutiwa na mimi kwenda Misri. Nikaanza kuwauliza maswali kuhusu bidhaa na naman aya soo lilivyo. Nikaandaa bidhaa zangu na kujiandaa kwa safari kuelekea Misri. Baada ya maandalizi kukamilika nikatoka na Ngamia wangu tulipia maeneo mbalimbali yakiyo ya kuvutia. Tulivuka bahari ya na kuingia Misri. Nikatafuta nyumba ya wageni na kulala nikiwa mimi na wafanyakazi wangu.


Ilipoofika asubuhi nikaanza kuchunguza mjini vyema na kutafuta eneo salama kwa biashara. Katika pirika nikakutana na meya wa Mji na kumuelezea shida yangu. Hapo akanielekeza kwa wafanyabishara wadogo. Basi nikaingia mkataba na wafanyabishara wadogo kwa makubaliano kuwa watauza bishaa zangu kisha nitakuwa ninkikusanya mapato kila siku ya alhamisi. Pia nitakuwa nikiwalipa kulingana na faida kwa kiasi maalumu. Wafanya bishara wengi wa Misri huwa wanatumia njia hii.


Basi nikawa kila alhamisi nakwenda kufuatailia mapato yangu na kisha ninawapatia ujira wao. Nikawa naagiza bidhaa kwa jumla kutokea maeneo mbalimbali kisha ninawapatia wauzaji. Kwa hakika Misri kulikuwa kukinipatia faida kuliko Baghadad. Nilifanya hivi kwa muda wa miezi 2 na nusu.


Sikumoja nilikaa dukani kwa wauzaji wangu nikiwa ninakunywa tangawizi iliyotokea china. Akaja msichana mmoja wa makamo kati ya miaka 21 mpaka 25. alikuwa amefunika sura yake, kama ilivyo tamaduni kwa waislamu. Kwa muonekana anaonekana ni msichana kutoka familia ya kitajiri. Basi alisogea mpaka pale nilipokaa na akakaa pembeni yangu. Hapo ndipo nilipopata kusikia sauti yake na harufu ya manukato yake. Hakika sijapatapo kupata harufu nzuri kama ile. Kwa muda huo aliweza kuteka fikra zangu na moyo wangu hata nisiweze kuhisi ladha ya tangawizi niliokuwa nikinywa.


Nilibakia mdomo waki nikiwa na maswali mengi, huyu ni nani, anataka nini hapa, ni mafuta gani amepaka, ni kwa nini amekuja kukaa karibu na mimi. Mmmmhhh sikutaka kumuuliza kwa kuhofia kuondoka kwake. Baada ya muda akaanza kuulizia bei za vitambaa vya ushungi, ambao una michirizi ya dhahabu nyekundu na mapambo ya hariri. Aliagizia vitu vya thamani sana hata nikafikiri atakuwa ni mtoto wa Mfalme.


Baada ya kuagiza akataka aruhusiwe achukuwe bidhaa kisha pesa atamuagiza mtu ailete. Yule muuzaji akakataa na kumueleza kuwa hawezi kufanya hivyo maana leo mmiliki wa bishara yupo. Nilipata kuyasikia vyema mazungumzo hayo. Yule binti alikasirika na kurudisha bidhaa zile na akasema “kwa hakika biashara yako haijali hadhi za watu”. maneno yale yalinichoma sana.


Basi kwa sauti ya upole nikamuita na kumwambia chukuwa hiyo bidhaa uliyoitaka kwani mimi ndiye mmiliki. Ukipenda utarudisha pesa usipopenda pia itakuwa ni sadaka yangu kwako. Maneno haya niliyasema bila ya kufikiri gharama ya bidhaa zile. Yule bint alinisogelea na kunieleza “Mungu akubariki kwa hisani yako, Naomba akupe afya njema ujekuwa mume wangu”. maneno haya yalikuwa ni kama msumari wa mshangao uliokita kwenye moyo wangu.


Nikamsogelea zaidi ni kumwambia ningepata japo kuona sura yako. Basi akasogea zaidi na kufunua kidogo kitambaa kilichoziba sura yake. Nilibaki kukodoa mimacho, hakika sijapatapo kuona uzuri huo kwa mwanadamu. Macho ya kuvutia yaliyozungukwa na nyusi nzuri zilizo nyeusi sana. Ngozi iliyo laini iliyokaa vyema kwenye shavu la binti huyo. Kwa haraka binti alishusha kitambaa na kupotelea njiani.


Sikumuuliza jina lake na hata wapi anakaa. Nilijuta sana maana nilitamani niwe ninamuona kila muda, kila saa, kila wakati. Nikamuuliza muuzaji wangu kuhusu taarifa za binti yule, naye hakuwa akifahamu jambo lolote. Siku hiyo sikupata hata lepe la usingizi, maana sura ya binti ilikuwa ikinijia usiku kucha. Nilitambua kuwa moyo wangu amekwenda nao wote.


BINTI HUYU NI NANI?
Siku iliyofuata nilioga mapema, kisha nikavaa ngu zangu safi na kuelekea pale dukani. Loo! Yule binti akaja tena, alipokuja moja kwa moja akakaa karibu nami na kutoa kitambaa kilichofungwa bundu. Kisha akaniambia “ Chukuwa hii malipo yako kwa bidhaa yako siku ya jana”. nikachukuwa na kumpatia muuzaji wangu ahifadhi. Sikuwa na haja ya kuhakiki kama pesa imetimia ama laa.


Basi nikaendelea kuzungumza naye maneno ya hapa na pale. Kisha nikaanza kuchomekea maneno ya ishara. Bila shaka alizifahamu vyema ishara zangu. Kwa ghafla alionyesha kukasirika na ndipo alisimama na kuondoka zake. Nilijijutia nafsi yangu kwa nini nimeongea naye kwa ishara za mapenzi. Aliondoka tena bila hata kuniambia anaitwa nani na wapi anakaa. Aluondoka hata sijazungumza hasa nini kipo moyoni kwangu.


Hakika siku hiyo niliiona ndefu sana na sikuweza kula chochote. Nilipata pia kujiwazia huenda binti yule sio mtu wa kawaida, huenda ni jini ama malaika ametumwa kuja kunijaribu. Siku ya tatu yake nikaamua kutembea mjini nkiamini huenda nikakutana naye kwa bahati mbaya. Loo! Sikuiliisha bila hata kukutana na sura yake.


Siku ya nne nilikaa kenye duka lile na ghafla akanijia bibi mmoja. Akanieleza kuwa ameagizwa na bosi wake aje anichukuwe ana mazungumzo. Bibi alikuwa ni mjakazi katika jumba la kitajiri. Nilifahamu hilo baada ya kuona mavazi yake. Nilikubali wito kwa kuamini atakuwa ni yule mrembo aliyeteka hsia zangu, aliyechukuwa moyo wangu, aliyenikosesha hamu ya kula wala kulala.


Niliongozana na bibi yule hata tukafika kwenye nyumba ya wageni. Hap akanieleza niingie kwani bosi wake yumbo ndani. Nilipoingia tu nikakaribishwa na manukato yanayonukia kwa uzuri sana, Loo! Alikuwa ni yule mrembo, alikuwa amependeza sana siku hii. Alvaa mavazi marefu yenye rangi za kuvitia kama tausi. Akanikaribisha kwnye busati lililotandika katikati ya chumba.


Hapo wakaja mabinti wengine wawili vigori, wakaleta vinywaji na kukaa pembeni. Akanieleza kuwa hawa pia ni wafanya kazi wake. Hawezi kukaa peke yake kwani faragha ya mwanaume na mwanamke wasio oana hairuhusiwi kwenye dini. Basi tulianza kuzungumza hapa na pale wakati huo mabinti wale wapo. Mwisho niamueleza uhalizi wa moyo wangu juu yake, ni kiasi gani ninampenda, ni taabu gani nimeipata kwa siku tatu hizi toka niutane naye.


Nilimueleza vyeote kuhusu kuwa sikuwa na usingizi wala sikuona tamu ya chakual. Wakati wote niliokuwa nachungumza yeye alikuwa akitokwa na machozi tuu. Moja wa mabinti wale akachukuwa kitambaa cha hariri kilicho zungushiwa na dhahabu nyekundu, na kutiwa manukato yanayonukia kama miski nyekundu ya kutoka india. Alimfuta machozi kisha akasema “ kwa hakika unayoyasema ndiyo yaliyomkuta bosi wetu, toka majuzi anakazi ya kukuwaza, kukutaja, kukufikiria, hali, halali, hanywi kwa upendo alionao kwako”.


Nilitamani kumfuta machozi ila nikaogopa kumvunjia heshima mbele ya wafanyakazi wake. Ndipo akasema kuwa “ kwa hakika walioyasema ndugu zangu ni sahihi, wewe ni mtu wa kwanza kukupenda, na amini nakupenda kweli, naomba tuoane. Kwani siwezi kukukosa tena, siwezi kuonja tena adhabu ya kuwa mbali nawe, uso wako kama lulu kwangu, katu sichoki kukutazama, tabasamu lako…… mmmhmmh nakupenda sana.”


Basi aliendelea kuzungumza kisha tukakubaliana kuwa tuoane ila ndoa iwe kwa siri kwa sababu, mimi ni mtu ambaye bado ni mgeni hivyo haitakuwa vyema kutangaza harusi yetu, na mimi ninatambulikamkwa utajiri nilio nao, hivyo wanaweza kukufanyia fitina, na hata kukuumiza. Siku ilofata ilikuwa ni ijumaa. Basi akanielekeza kwake ili niende baada ya kuswali ijumaa ili ndoa ikafanyike. Basi tukaagana pale na mimi nikaondoka na wao wakaelekea zao.


Sikuwa na haja tena ya kulijuwa jina lake maana niliamini kuwa nitalijuwa siku ya harusi. Nilijuwa kuwa yeye ni tajiri na ni mtoto wa tajiri. Niliamini ili niweze kuishi naye ni lazima nitumie pesa vyema. Basi siku hiyo sikuweza tena kulala kwa kuisubiri asubuhi ifike, ili nikamuoe kipenzi maridhawa.


NDOA YA SIRI YAFANYIKA
Hatimaye siku ya ijumaa ikafika na mimi nikaoga nyema na kuchukuwa kanzu iliyo nadhifu zaidi. Nikaifaa na kujipaka manukato maridadi na kuwa mtanashati ka kuelekea kwenda sala ya ijumaa. Mapema nilifika msikitini na kuanza kumuomba Mungu. Kwa furaha nia shauku nilioa nayo hata sikuweza kulala msikitini. Baada ya sala kuisha nilitoka masikitini na tayari kuelekea kwa kipenzi changu mtarajiwa.


Nilichukuw amashahidi wawili kwa siri, na hawa walikuwa ni wafanyabiashra wenzangu wa kutokea Baghadad. Tulipanda magari ya kuburuzwa na farasi. Tukafika katika nyumba niliyoelekezwa na tayari kugonga mlango. Mabinti wawili wengine walio wazuri sana wakafungua malango na sisi watu watatu tukaingia. Tulikutanan na ukumbi mzuri wenye malumalu za almasi. Ukuta uluojengwa vyema na kutiwa mapambo ya madini ya fedha a almasi.


Nikaangalia vyema nikaona mapambo yenye kuchorwa kwa lugha ya kiarabu kilicho pendeza. Tuliweza kusogea kila chumba kikiwa kina mapazia marefu yenye rangi za kupeneza sana. Mapazia yalikuwa na michirizi ya madini ya silva pamoja na mapambo ya nayoning’inia mithili ya lulu zilizohifadhiwa vyema. Niliweza kustaajabishwa na manukato ya vyumba hivi ni mazuri sana sijapatapo kuyaona. Tuliendelea hata yukafika kwenye kumbi moja kubwa sana. Hapo tukakuta kuna watu kadha aa wanaume.


Niliweza kuchunguza vyema ukumbi huu nikagundua umepambwa mapambo mazuri sana. Umechorwa michoro ya vippeo michoro iliweza kutiwa rangi za kijani, manjano na bluu. Hakiak niliweza kumpa sifa sana mchoraji. Katikati ya chumba kulukuwa na kiti kikubwa sana cha miguu sita. Miguu iliyopamba kwa vishikizo vya madini ya shaba, magodoro ya hariri yalikaa byema kwenye kiti hiko kikubwa.


Juu ya kiti mzee mkubwa alikuwa amekaa hapo. Nilimtambuwa umri wake ni kati ya 60 mpaka 70. alikuwa na ndevu nyingi na nyeupe zilizomkaa vyema. Alikuwa na sharubu nyupi na mashrafa yaliyo lala vyema. Ndevu zenye afya njema zilizotiwa hina na kufanana vyema. Mzee alivaa kanzi nadhifu yenye manukato zaidi ya watu wote tulio hudhuria. Basi tukakaribishwa vyema nikaka mimi na wenzangu. Jumla tulikuwa wtatu 9.
Bila ya kupoteza muda yule mzee akanitaja kwajina “Je wewe kijana ndiye Ibrahimu Khalidi wa Baghadad?” nilisita kidogo kujibu huku nikiwaza amelijuaje jina langu, na amejuaje kama natokea Baghadad. “ndiye mimi mzee” basi akaniambia nisogee karibu na ndipo akaniuliza maswali kadhaa na nikamjibu vyema. Basi akaniuliza “ Kijana Ibrahimu khalid umekubali kumuoa mwanangu Nurat khan”? “ hapo ndipo nilipopata kujuwa jina halisi la binti yule na kumjuwa Baba yake. “Ndio nimekubali kumuoa Nurat Khan…”


Baada ya hapo mbele ya mashahidi ndoa ikafungwa. Mashahidi waliweza kupatiwa dhahabu pishi tano kila mmoja na wakaruhudiwa kuondoka. Mimi nikapelekwa kwa mke wangu. Kwa hakika nilipatapo kuona mambo mengi na mazuri na ya kustaajabisha. Naomba nisielezee hasa kipengelehiki. Basi tukaelekea nyumba nyingine ambapo ndipo binti anaishi. Huko ni mbali na alipo baba yake. Na tukaendelea kumaliza taratibu za usikuwa harusi mimi na mkewangu (……taa ikazimwa…….).


KUKATWA MKONO NA KURITHI UTAJIRI
Basi niliweza kulala kwa mke wangu siku ile na asubuhi nilimuashia kipande 1000 vya dhahabu na kuondoka kuelekea dukani. Jioni niaenda tena kwa mkewangu nikalala na asubuhi jikamuachia vipande 1000 vya dhahabu na kuondoka. Niliweza kufanya hivi kwa muda hata nikafiisika mali yangu yote ikiisha. Nikiwa sina kitu, huku nikiamini kama nitaenda mikono mikavu nitaingia aibu katika familia ya kitajiri.


Nikiwa na mawazo kama hayo mara nikaona sehemumoja kuna msongamano wa watu. Nikasogea karibu nakukuta kuna watu wanapigana. Katika kusogea zaidi mara bikaona mama mmoja ameweka vipande vingi vya dhahabu kwenye kikapu chake kisha amefunika kwa kanga kuukuu. Basi nikasema leo ninaiba nipate kumliwaza mke wangu. Nilisogea karibu na kuingiza fumba la kwanz ana kutoa vipande kama kumi.


Nikaingiza tena mkono na kupata vipande 5 nikajisemea hivi vinatosha. Wakati nataka kuondoka yule mama akashibuka na kuniona. Hapo akaniitia kuwa ni mwizi na haikupita muda nikawekwa mbaroni. Nilijitetea na ndipo nikapelekwa kwa kadhi. Nikasachiwa na kukutwa na vipande vya dhahabu. Basi kadhi akahukumu nikatwe kiganja cha mkono kwa mujibu wa sheria za kiislamu.


Nilikatwa mkono na kupoteza fahamu. Kuja kushituka nipo sehemu ya mbali nimetupwa. Niliweza kujikongoja hata nikafika kwa mke wangu. Nikaufunga mkono wangu ili asiuone. Niliishia kulala na kumueleza kuwa ninaumwa. Kilipokuja chakula nilikulwa kwa moko wa kushoto. Kitebdo hiki kilimuuuma sana ndipo akataka kuona nini kipi kwenye mkono wangu wa kulia. Nilimueleza kuwa nina jipu ila hakutaka kuniamini.


Alinifungua na ndipo akaanza kuli sana. Basi nikamueleze akila kilichotokea bila hata kuficha kuwa kwa ajili yake nilikusudia kuiba na nikaiba ila nikakamatwa na kukatwa kiganja cha kulia. Basi alilia sana kisha akasema “ kwa ajili yangu umekatwa mkono, ulidhani nimekupenea pesa” basi akaagiza aletewe mashahidi wawili ndipo walipokuwa akawaambia washuhudiie kuwa mali za ke zote ni za kwangu, alioroshesha mali nyingi sana, mashamba na majumba mengi yaliyopo mjini. Alipo maliza kuoroshesha akaweza muhuri wake na hati ile ya makubalian ikapelekwa kwa baba mkwe naye akaikubali.


Kila kitu kilivyokuwa sawa aliwalipa mashaihidi na kisha akanichukuwa mpaka kwenye stoo. Huko nikakuta kuna mamia ya masanduku yaliyojaa dhahabu na fedha nyingi. Sanduku moja lilifumikwa kitambaa cha kijani na kuandikiwa kwa lugha ya kiarabu cha asili. Sikuweza kutambua maana yake. Ndip akanieleza kuwa kumeandikwa “kwa kipenzi changu” akanieleza fungua. Loo! Nilipofungua nilikuta vipande vyote vya dhahavu nilivyompa vipo pale kama vilivyo.


Akanieleza kuwa Mwenyezi Mungu amekurudishia mali yako na kukupa ziada, na kukupa mke mwema. Hapo nilimkumbatia mke wangu na kumbusu katikati ya paji lake. Mmhmmmh….(rahaaa). basi nilianza kuendeleza mali za mkewangu tukiwa pamoja. Tuliweza kuishi mika 10 na kubahatika mtoto mmoja wa kike. Miaka mitatu iliyopita mkewang aliumwa na kufariki.


Hivyo kwa ubize niliyokuwa nao ndipo hata nikashindwa kuchukuwa pesa yangu iliyo kwako. Na hii ndio hadithi yangu ya kukatwa mkono. Usidhani nilikula kwa mkono wa shoto kwa kupenda ama majigambo. Baada ya kijana mtanashati kumaliza kuzimulia kisha chake akanieleza kuwa, je ungependa yuende wote Baghadad kibiashara?. nami nikakubali.


Wiki ilofata ndipo tuakaanza safari ya kuja Baghadad. Tulifanya bishara na muda wa kurudi ulipofika mwenzangu alirudi ila mimi nikamueleza kuwa nitaendelea kuishi hapa. Akanieleza nitakaporudi Misri nimpe taarifa maana binti yake atakuwa amefikia kuolewa, hivyo angependa niwe mkwe wake.


Basi niliweza kuishi hapa Baghadad ni mpaka leo


  1. 1
  2. 2

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela1 Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 970


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Hadithi ya mzee wa tatu na mbwa wake mwekundu
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Ndani ya pango la makaburi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Alif lela u lela 1
Alif lela u lela ni hadithi zilizosheheni utamu na machungu pamoja na visa vya wachawi na majinim soma sasa. Soma Zaidi...

HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE. Soma Zaidi...

HADITHI YA BINT WA PILI MWIMBA MASHAIRI MWENYE MAKOVU
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA BINTI WA PILI MWIMBA MASHAIRI MWENYE MAKOVU. Soma Zaidi...

JINI NA MFANYABIASHARA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA JINI NA MFANYA BIASHARA. Soma Zaidi...

Kitabu Cha hadithi ya wanawake watatu
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: KIFO CHA DAMU
Soma Zaidi...

Hadithi ya chongo wa tatu mtoto wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

NDOTO YA MGONJWA MTOTO WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa NDOTO YA MGONJWA BINTI WA MFALME. Soma Zaidi...