image

Kuingia kwa wageni

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

KUINGIA KWA WAGENI

Amina na Sadie walimuonea huruma wakamuomba Zubeid amruhusu abakie. Basi Zubeida akamwambia “naongeza sharti lingine kuwa usiulize chochote kwa utakayoyaona yanafanyika hapa ndani”. Kijana kwa mara nyingine anakubaliana na sharti hili. Basi pale ndani furaha iliendelea mpaka waliposikia mlango unagongwa. Sadie akaenda kufungua akakuta kuna watu watatu kwa mavazi yao wanaonekaa ni wageni katika mji ule. Walikuwa wote wanachogo jicho la kulia, na wamenyoa nyusi zao na vichwa vyao ni kipara. Wageni hawa wa kushangaza walikuwa wanamuomba Sadie hifadhi ya kuwaruhusu walale pale kwa leo.

 

Sadie akarudi kwa dada zake kuwaambia kilichopo mlangoni, Zubeida alionekana kutokukubaliana na ugeni huo Sadie akadakia “dada waruhusu walale bila shaka mtawafurahia, maana wanapendeza kweli” kwa shauku Amaina alitaka kujuwa wakoje wageni hao, “wote ni vipara na hawana nyusi upande wa kulia na waote ni chongo jicho la kulia, na wanaonekana ni wageni wa huu mji, bila shaka ni wasafiri” alisema Sadie. Basi Zubeida alijubali kuwaruhusu ila akamsisitiza Sadie awape shari la kukubaliana na kilichoandikwa mlangoni.

 

Wageni wakaingia ndani na bila kusahau Sadie akawaashiria wasome maandishi yaliyopo malangoni “USIULIZE CHOCHOTE KATIKA MAMBO UTAKAYOYAONA HUMU NDANI” wageni walionesha ishara ya kukubaliana na sharti hili. Basi nyumba iliendelea kufurahia, mmoja ya wale wageni akaomba apewe filimbi, na akaanza kupiga na mwenzake mwengine akawa anaimba na mwenzao mwengine akawa anacheza. Wimbi uluwafurahisha sana wakina Amina na Sadie. Zubeida alionekana kupenda zaidi namna ya yule aliyekuwa akicheza.

 

Basi mabo yakawa kama hivyo, furaha ilienea sana ndani mule. Siku hiyo mfalme wa nchi hiyo alikuwa anafanya uchunguzi wake akiwa amefaa nguo za kiraia zinazofanana na wafanyabiashara. Basi walipofika jirani na nyumba ya wakina dada hawa walisikia vifijo na furaha iliyoenea nyumbani pale. Basi kwa shauku kubwa mfalme alitaka kujuwa ni wakinanani hao. Na kwakuwa alifaa mavazi ya wafanya biashara haikuwa rahisi kumtambua. Basi akamuamuru waziri wake akagonge mlango. Waziri akafanya kama alivyoambiwa, na akagonga mlango akatoka Sadie kuja kufungua mlango. Akakuta wafanya biashara watatu waliovaa mavazi mazuri ya kupendeza.

 

Sadie akaingia kwenda kutoa taarifa ndani kwa dada zake, “dada ni wageni watatu wanataka hifadhi, wamekuja nchi hii hawana wanaemfahamu hivyo wanaomba hifadhi ya kulala kwa leo tu” ni maneno ya Sadie akiwaeleza dada zake. Baada ya mashauriano Zubeida akaruhusu wapate hifadhi lakini kwa shart lilelile liloandikwa kwenye mlango wao. Basi Sadie akawakaribisha na kuwapa sharti lile waliopewa wale wageni kwa kwanza. Basi furaha ikarejea pale ndani na vinywaji na vyakula vililiwa na wachezaji na waimbaji wakaendelea. Waziri alikuwa muda wote anadukuduku la kutaka kujuwa kwa nini pale kuna chongo watatu, wote upande wa kulia wamenyoa nyusi na ni vipara. Wakati anataka kuuliza Sadie akadakia “jua mambo yako usiulize kitu usije ukajuta”.

 

Haliiliendelea hivyo mapa Zubeida aliposimama na kuwaambia ndugu zake “HAYA MUDA UMEFIKA TUANZA SASA”. Basi pale Sadie akaanza kusafisha pale ndani na kupangilia kila kitu kwenye sehemu yake. Kisha akawataka wageni wote wakae kwenye viti na pale ndani pabakie pakiwa safi. Kisha sadie akamuomba kijana mbeba mizigo aje amsaidie. Wakaingia ndani na kuja na mbwa wawili wakiwa wamefungwa nyororo katika shingo zao. Zubeida akiwa amekaa kwenye kiti kile kirefu akaagiza aletewe moja kati ya wale mbwa. Basi Sadie bila kuchelewa akampelekea mbwa yule. Zubeida akambusu mbwa yule kisha akasema “je tuanze?”. Hakuhitaji kujibiwa swali lile.

Basi akachukuwa mjeledi akaanza kumchapa mbwa yule kwa muda mrefu mpaka akachoka. Akapunzika kidogo na kuendelea. Alipomaliza akamshika yule mbwa miguu ya mbele na kuanza kumfuta machozi. Akajifuta na yeye pia kisha akambusu kwa mara nyingine. Kisha akaagiza aletewe mbwa mwingine na yule arudishwa, Sadie akatii maagizo. Mbwa wa pili alifanyiwa kama alivyofanyiwa yule wa kwanza.

 

Wakati mambo yote haya yanafanyika, wageni walikuwa wakigusana gusana kwa shauku ya kutaka kujua hasa ni nini kinaendelea. Mfalme aliyejifanya mfanyabiashara akawa anampa maagizo waziri wake kuuliza lakii waziri akajifanya hakusikia. Wakati mambo yanaendelea pale ndaubaida akamuita Amina na kumwambia “njoo Amina ufanye kazi yako”. Muda uleule Amina akaja na vifaa vyake vikaletwa pale na Sadie.kukaletwa filimbi, nguo, kioo na vitu vingine.

 

Basi Amina akawa anaimba mashairi kwa filimbi ile mpaka akapoteza fahamu. Walati huo watu wote wakawa wanashangaa kinachoendelea pale ndani. Basi Sadie akaja na kumpepea dada yake na kumpunguzia mavazi, basi mfalme na wenzie wakaona akovu mengi ya kutisha yaliyopo kwenye mwili wa Amini. Mara hii mfalme alishindwa kujizuia kwa shauku akataka kujuwa ni vitu gani vinafanywa pale ndani, kwa nini mbwa wamepigwa vile na ni kwa nini huyu dada ana makovu makubwa na ya kutisha kwenye mwili wake?. Basi waziri kumridhisha mfalme akamuuliza moja kati ya chongo “hebu tuambieni nyinyi wenzetu mlikuwa hapa ni mambo gani haya tunayo yashuhudia?”. Chongo akawajibu “mmh hata sisi hatuna ujuzi wa kujua mabo haya, sisi pia tumekuja muda si mrefu kabla ya kuja kwenu, lamda tumuulize kijana mbeba mizigo huyu maana tumemkuta. Huenda akawa na habari ya mabo haya”. Majibu ya kijana yakawa yaleyale hatambui kinachofanyika hapa.

 

Basi wakiwa katika hali ya kunong’ona pale ndani ghafla Zubeida akanyanyuka na kuwaambia “mnanini hapo? au mmesahau sharti tuliowapa kabla ya kuingia ndani hapa?”. Kijana akajibu “heti wananiuliza wanataka kujuwa maana ya mabo haya mmnayoyafany ahapa.”. Watu wote pale walikuwa tayari hata kufa lakini wajue maana ya mambo yale. Zubeida akauliza tena “ni kweli anayosema mwenzenu?”. Wote wakaitikia “naam, hasa ni kweli kabisa”. Zubeida akaoka pale kwenye kiti chake akiwa maekasirika sana na kuanza kusema “tumewafadhili hapa na tukawapa sharti moja tu lakini limewashinda. Sasa mnataka kujuwa mabo msiyopasa kuyajuwa.”. Kisha akaita “njooni”

 

Muda uleule wakaja walinzi wa ndani pale na kuwaekea kisu shingoni kwa kila mmoja pale ndani.

 

“sasa wote mtakufa kwenye mikono ya walinzi wangu hawa au kula mmoja anieleze habari yake hata bila ya kudanganya” kusikia maneno haya mfalme akafurahi kwa sababu wakisikia kuwa yeye ni mfalme wasinge muua. Basi Zubeida akamwenea kijana mmemba mizigo na kumwambia “tueleze habari yako bila ya kudanganya na umefika vipi hapa?” kwa sauti ya woga kijana akaanza kuzungumza kuanzi apale asubuhi alipokutana na Sadie maka alipofika pale ndani.

 

Baada ya kwisha kutaja hadithi yake kijana akaruhusiwa aondoe ke muda uleule. Akapiga magoti mbele ya Zubeida na kumwambia “dada naomba ufanye haki kati yetu, wao wamesikiliza hadithi yangu na mimi nataka Kimoyoni alikuwa akiwaza kusikiliza hadithi za hawa vichongo watatu. Basi Zubeida akamwendea moja ya chongo wale na kumwambia ahadithie hadithi yake. Kichonho yule akanza kusema “kwanza jua ewe dada mkubwa wa nyumba hii kuwa sisi unaotuona ni chongo wote ni watoto wa wafalme katika tawala mbalimbali. Kila mmoja anastori yake ya kustaajabisha kuhusu chongo yake. Basi wakaanza kuhadithi stori zao kama ifuatavyo;-





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1037


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

MWANZO WA USALITI
Download kitabu Hiki Bofya hapa USALITI UNANZA HAPA Baada ya kukaa pale siku moja nahodha akaamrisha chombo kiondoke pale na kurudi nyumbani. Soma Zaidi...

HADITHI YA MZEE WA PILI NA MBWA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MZEE WA PILI NA MBWA WAWILI WEUSI. Soma Zaidi...

Hadithi ya mke na kasuku
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

HADITHI YA BINTI MWENYE KUFICHWA MTOTO WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA BINTI MWENYEKUFICHWA, MTOTO WA MFALME. Soma Zaidi...

Safari ya pili ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Kisiwa cha uokozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Hadithi ya mji uliogeuzwa mawe
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI. Soma Zaidi...

ALIF LELA U LELA: UTANGULIZI
ALIF LELA U LELA. Soma Zaidi...

KISIWA CHA UOKOZE CHA PILI
Download kitabu Hiki Bofya hapa KISIWA CHA UOKOZI Nilikwenda mpaka nikakuta misitu minene na nisijuwe pa kuenda. Soma Zaidi...

Safari ya saba ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Alif lela u lela 1
Alif lela u lela ni hadithi zilizosheheni utamu na machungu pamoja na visa vya wachawi na majinim soma sasa. Soma Zaidi...