Upeo wa Elimu waliyokuwa nayo Mitume




Mitume walikuwa na upeo wa fikra na hekima kuliko mtu 101
yeyote katika jamii zao. Hawakusoma kwa mtu bali walifunuliwa elimu kwa njia ya Wahay kutoka kwa Mola wao. Kwa mfano juu ya Nabii Daudi na Suleimani tunasoma katika Qur-an:“Na bila shaka tuliwapa Daudi na Suleimani elimu (kubwa kabisa na wakamshukuru Allah) wakasema, “Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu aliyetufadhilisha kuliko wengine katika waja wake waliomuamini” (27:15)