Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
SURA YATISA
HUKUMU ZA WAQFU AL-IBTIDAI
l-Waqfu Wal-Ibtidaai – Kisimamo Na Kianzio
Msomaji si kwamba muda wote atakuwa anasoma bali, wakati mwingine anapumzika, au anasimama kidogo kumeza mate au kupumua ana atakata kabisa kusoma. Hivyo hapa kuna kauli tatu ambazo inatupasa tuzijue kabla ya kuenddelea. Kauli hizo ni;-
1.Al-waqfu: maana yake ni kisimamo nako ni kukata kusoma kwa muda wa kawaida kwa ajili ya kuvuta pumzi huku msomaji akiwa na nia ya kuendelea kusoma.
2.Al-sakt:maana yake ni kipumziko nako ni kupumzika kwa muda kwa kiasi cha haraka mbili huku msomaji akiwa na nia ya kuendelea kusoma.
3.Al-qatw’u;maana yake ni ukataji nako ni kusimama kusoma kwa lengo la kumaliza kusoma. Hapa inabidi mtu amalize kusoma kwake mwishoni mwa aya au sura. Na inatakikana pindi anapotaka kuendelea kusoma aanze na isti’adha
ALAMA ZA WAQFU KATIKA QURAN:
1.aAlama hii(صلي) inamaanisha inajuzu kuunganisha.
Yaani pindi msomaji anapokuta alama hii anaweza kuunganisha maneno hayo, yaani neno la nyuma na maneno yanayofata. Hivyo hapa msomaji ana hiyari ima kuunganisha au kusimama (kufanya waqfu).
2.Alama hii (قلي) inamaanisha inajuzu kusimama.
Yaani pindi msomaji anapokuta alama hii atakuwa na hiyari ya kusimama.
3.Alama hii (ج) inamaanisha inajuzu kusimama ila kwa ufupi. Yaani msomaji anapokutana na alama hii ataweza kusimama hapa, ila usimamaji wake usiwe mrefu.
4.Alama hii (م) inamaanisha kusimama kwa lazima. Yaani msomaji anapokutana na alama hii kusimama kwake ni kwa lazima.
Alama hii (لا) inamaanisha hairuhusiwi kusimama sehemu hii. Hii inamaanisha msomaji hatakiwi kusimama pindi anapokutana na alama hii.
Umeionaje Makala hii.. ?
Aina za idgham ni idgham al mutamathilain, na idgham al mutajanisain
Soma Zaidi...Qur-an inavyogawa MirathiMgawanyo wa mirathi umebainishwa katika Qur-an kama ifuatavyo:Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu: Mwanamume apate sawa na sehemu ya wanawake wawili.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukuorodheshea aina saba za viraka vya usomaji wa Quran.
Soma Zaidi...Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Kuwa na tamaa huhitaji vitu vya watu si jambo jema. Ila kama tamaa hii itakuhamasisha na wewe kutafuta kitu hicho, kwa uwezo ambao Allah amekupa bila ha kuvuka mipaka yake, hili sio tatizo. Sura hii itakufundisha mengi
Soma Zaidi...Kama tulivyoona kuwa id-ghamu ipo katika aina kuu mbili ambazo ni id-ghamu bighunnah na id-ghamu bighair ghumnah. Sasa hapa tutajifunza makundi mengine ya idhgamu.
Soma Zaidi...(i)Mtume Muhammad (s.
Soma Zaidi...SURAT AL-MUAWIDHATAYN (SURAT AL-FALAQ NA SURATUN-NAS) Inaelezwa kuwa sura mbili hizi zilishuka pamoja, na maulamaa wanaelezea kuwa Mtume (s.
Soma Zaidi...