SURA YA 11
MADD (Al-Maddul-Far-’iy)

Al-Maddul-Far-’iy
الْمَدُّ الْفَرْعي - Al-Maddul-Far-’iy
Madd ambayo hutegemea sababu nyengine ima iwe hamzah au sukuwn ili iweze kurefushwa kuvutwa kwake kuishinda مَدُ الطَّبِيعي (maddutw-twabiy’iy) na hiyo sababu ya nje. Imeitwa ‘Al-Far-iy’ (tawi) kwa sababu madd hizi sio za asili bali zimechipuka kutoka katika مَدُ الطَّبِيعي (maddutw-twabiy’iy) . مَدُّ الْفَرْعِي Maddul-Far-‘iy Hugawanyika sehemu mbili kutokana na sababu inayopelekea kuwa madd:
• Madd kutokana na hamzah
مَدُّ الْواجِبِ الْمُتَّصِل . 1 Maddul-Waajib Al-Muttaswil
مَدُّ الجْائزِ المنُْفصِل . 2 Maddul-Jaaiz Al-Munfaswil
مَ دُّ الصِّل ةِ الْكُبْرَى . 3 Maddusw-Swillatil-Kubraa

• Madd kutokana na sukuwn
مَدّ الْعارِض لِلسُّكُون . 1 Maddul-‘aaridhwi lis-sukuwn
مَدّ ال لين . 2 Maddul-liyn
مَد الّلازِم . 3 Maddul-laazim

Madd kutokana na hamzah:
مَدُّ الْواجِبِ الْمُتَّصِل . 1 (Maddul-Waajib Al-Muttaswil) Na inaitwa ‘Waajib’ kwa kuwa Maqurraa wote wamekubaliana kuivuta zaidi kuliko مَدُ الطَّبِيعي (maddutw-twabiy’iy). Na inaitwa ‘Muttaswil’ kwa kuwepo hamzah na madd katika neno moja. Hukmu yake katika riwaayah ya Hafsw ‘an ‘Aaswim twariyq Ash-Shaatwibiyyah ni kuivuta ima kwa harakah nne au tano.
MADD


2 (Maddul-Jaaiz Al-Munfaswil) Ni kuwepo herufi ya madd mwisho wa neno, na kufuatiwa na hamzah katika mwanzo wa neno linaloifuatia. Huvutwa haraka nne mpaka tano.
MADD

Madd kutokana na sukuwn
مَدُّ الْعأرِض لِلسُّكُون .. 1 Maddul-‘aaridhw lis-sukuwn
Ni kuwepo baada ya herufi ya madd na baada yake sukuwn ’aaridhw kwa sababu ya kusimama. Hukmu yake kwa kila qiraa-ah inajuzu kuivuta katika hali tatu:
• Qaswr (kuifupisha) kama harakah mbili
• Tawasw-swutw (wastani) harakah nne
• Twuwl (kurefusha) harakah sita.
MADD


2 Maddul-Liyn
Hii ni madd ambayo ni tofauti na madd nyinginezo kwa sababu herufi zake ni tofauti kwani hizo zinajulikana ni ‘herufi za madd’ ( ا و ي ) zinazonasibiana na i’raab katika herufi ya kabla yake. Ama hii inajulikana kuwa ni ‘Harfulliyn’. Herufi za اللِّين (liyn) ni herufi za و au ي zinapokuwa saakin na kabla yake ni herufi iliyokuwa na fat-hah: ÏImeitwa اللِّين (liyn) kwa sababu ya kutamkwa kwake kwa usahali (ulaini) bila ya taklifu.
اللِّين (liyn)Ni kuwepo baada ya herufi ya اللِّين na baada yake sukuwn ’aaridhw kwa sababu ya kusimama. Hukmu yake ni kuvutwa harakah ima mbili au nne au sita kwa kila qiraaah

MADD
3 Maddul-Laazim
Ni kuwepo baada ya herufi ya madd herufi saakin yenye sukuwn ya asili ambayo inayothibiti wakati wa kusimama na kuunganisha. Maqurraa wamewafikiana katika kuivuta madd hii harakah sita. مَد الّلازِم (maddullaazim) na huvutwa haraka 6 inagawanyika sehemu mbili:
I. الْكَلِمِيّ Al-Kalimiyy (ya neno)
II. الحَْرْفِيّ Al-Harfiyy (ya herufi)

I. الْكَلِمِيّ Al-Kalimiyy (ya neno):
i. أل مَدّ الّلازِم الْكَلِمِيّ الْمُثَقَّل Al-Madd Al-Laazim Al-Kalimiyyi Al-Muthaqqal
Huitwa الْكَلِمِيّ (ya neno) kwa vile inatokana na neno. Huitwa الْمُثَقَّل (iliyo nzito) itakapokuja baada ya herufi ya madd herufi yenye shaddah. Itambulike kuwa herufi yenye shaddah asili yake ni herufi mbili zinazofanana; ya kwanza huwa ni saakin na ya pili ni yenye i’raab, hivyo ikatokea idghaam.
MADD


ii. الْمَدُّ اللاَّزِمِ الْكَلِمِيِّ الْمُخَفَّف Al-Madd Al-Laazim Al-Kalimiyyi Al-Mukhaffaf
Huitwa الْكَلِمِيِّ (ya neno) kwa vile inatokana na neno. Huitwa الْمُخَفَّف (khafifu) itakapokuja baada ya herufi ya madd herufi saakin isiyo na shaddah kwa maana, hapatoeki idghaam. Katika riwaayah ya Hafsw ‘an ‘Aaswim hakuna isipokuwa mara mbili pekee katika neno moja tu nalo ni tø9!#u katika Swurat
Yuwnus aya 51 na 91

II. الحَْرْفِيّ Al-Harfiyy: (ya neno)
الْمَد الّلازِمْ الحَْرْفِيّ Al-Madd Al-Laazim Al-Harfiyy ni madd inayopatikana katika herufi zilizokuja kwenye mwanzo wa Suwrah 29 za Qur-aan zinazoitwa:
الحُْرُوف الْمُقَطَّعة Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah (Herufi zilizokatika) kwa maana zinatamkwa kama herufi za hijaaiyyah. Jumla ya herufi hizo ni 14 ambazo zimeundwa katika ibara kadhaa mojawapo ni: طرق سمعك النصيحه
Baadhi ya hizi Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah zimekariri zaidi ya mara moja na kuzifanya jumla kuwa ni ishirini na tisa:
Herufi hizi zimegawika sehemu nne:
• Isiyo na madd nayo ni الف) ا ) Alif -haivutwi kabisa.
• Madd harakah mbili katika herufi za 1 حي طهر
• Madd haraka mbili au nne au sita katika herufi ya عين) ع ) kwa kuwa inatekelezwa kwa مَدُّ اللِّين (maddul-liyn)
• Madd harakah sita katika herufi za سنقص لكم (سين – نون – قاف – صاد – لام – كاف – ميم)
MADD

Imegawanyika katika sehemu mbili:
الْمَدُّ اللاَّزِمِ الحَْرْفِيّ المثَُقَّل -Al-Madd Al-Laazim Al-Harfiyy Al-Muthaqqal na الْمد الّلازِم الحَْرْفِيّ الْمُخَفَّف - Al-Madd Al-Laazim Al-Harfiyy Al-Mukhaffaf