Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu tukio la Kupasuliwa kwa Kifua Mtume Wakati Akiwa Mtoto
Mtume alipokuwa mtoto, tukio hili la kupasuliwa kifua na kutolewa moyo wake na kusafishwa lilitokea. Yote haya yalitokea kipindi akiwa analelewa na Bi Halima katika kabila la Bani Sa'ad. Wanazuoni wa sirah wameeleza kwa urefu tukio hili jinsi lilivyotokea, na hapa tutaangalia kwa ufupi tu.
Ni kuwa siku moja Mtume (s.a.w) alikuwa anacheza na watoto wenzie. Ghafla akatokea mtu mmoja, naye ni Jibril, akamshika Muhammad na kumlaza chini kisha akamtoa moyo wake na kuuosha kwa maji ya zamzam na aliondoa uchafu wa shetani kisha akaurudisha kwenye kifua na kukifunika.
Watoto walokuwa wakicheza na Mtume (s.a.w) wakakimbia na kwenda kumueleza Bi Halima kuwa Muhammad kauliwa. Bi Halima akatoka kwa haraka kufika akamkuta Muhammad akiwa amebadilika rangi. Muhammad alikuwa mzima wa afya, hapa Bi Halima alipata mashaka makubwa mpaka akawa na hofu juu ya kuendelea kumlea kijana Muhammad.
Katika maelezo mengine, waandishi wa sirah wameeleza tukio hili kama kupasuliwa kwa tumbo. Kwani zimekuja nukuu kuwa siku moja watoto walipokuwa wakicheza pamoja nao alikuwepo Muhammad (s.a.w), basi ghafla wakaja wanaume wawili walovaa nguo nyeupe (malaika) wakaulizana, "Ni huyu?" Basi yule mwingine akajibu, "Ndiyo, ni huyu." Wakamlaza kisha wakampasua tumbo lake na kutoa uchafu wa shetani kisha wakafunika kama lilivyo. Basi watoto walokuwa wakicheza naye wakaenda mbio kusema kwa Bi Halima na alipokuja kuulizwa Muhammad (s.a.w), akasema kuwa watu wawili wamekuja na kunipasua tumbo langu. Utapata maelezo zaidi ya kisa hiki kwenye kitabu kiitwacho "Nurul-Yaqin."
Bi Halima aliendelea kumlea Mtume (s.a.w) kwa muda wa miaka miwili mingine hadi alipotimiza miaka minne. Alipoamua kumrudisha mtoto kwa mama yake. Alihofia kuendelea kumlea mtoto huyu huenda akapatwa na jambo. Miaka minne ilikuwa imemtosha mtoto huyu kuwa na mwili imara na kuweza kuzungumza lugha ya Kiarabu kwa ufasaha tofauti na watoto walolelewa maeneo mengine.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwend akujifunza mkakati uliohusu kuficha imani ya uislamu kimatendo na kimaneno kwa kuhofia mateso ya Makafiri dhidi ya Waumini wapya
Soma Zaidi...katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Mazazi ya Mtume MUhammad ﷺ na kupewa jina.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu historia ya Mkataba wa Aqaba wa kwanza
Soma Zaidi...Katikasomo hili utakwenda kujifunza stori maarufu ya Bahira kuhusu kukutana na Mtume Muhammad ﷺ na kumtambuwa utume wake.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza historia ya kuslimu kwa Hamzah bin Abdul-Muttalib.
Soma Zaidi...Katka somo hili utakwenda kujifunza kuhusu mateso ambayo wamepewa Waislamu ili kuachana na uislamu wao
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu mwanzoni mwa kuamrishwa ibada ya swala na vipi iliswaliwa.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu mmoja katika maadui wakubwa wa Mtume Muhammad wakati akilingania watu.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuusu historia ya mmoja katika maswahaba wa mwanzoni na mwenye mchango mkubwa sana katika uislamu ambaye ni Al-Arqam ibn Abi al-Arqam
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu miaka mitatu ya kulingania dini kwa siri na mambo yaliyojitokeza.
Soma Zaidi...