Chemsha bongo 10

imageimage
24.Mirathi
Kulikuwa na mzee mmoja na watoto wake watatu. Mzee huyu alikuwa na mali nyingi sana. Akatamani amrithishe mali zile mtoto wake ambaye atakuwa na busara zaidi. Basi akawaita wanawe na kuwapa chemshabongo, na kuwa atakayeshinda ndiye ambaye atarithishwa.

Aliwapa sarafu 2 za shilingi mia mbili na kuwataka wanunue kitu cha kujaza chumba kizima kwa pesa zile. Basi mtoto wa kwanza akaleta mikate ambayo haikujaa hata kwenye bakuli. Wa pili akaleta makaratasi ambayo hayakujaa chumbani. Mtoto wa tatu akaleta kitu . na mzee akamchaga huy wa tatu. Unadhani ni kitu gani mtoto huyu alileta?

Jibu
Alileta kibiriti, ulipofika usiku aliwasha njiti ya kibiriti na chummba kizima kikajaa mwanga.