WAJUE FANGASI NA AINA ZAO

Fangasi huweza kuishi na kuathiri maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Fangasi ni hatari sana, kwani wanaweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya na kiakili kama wasipitibiwa mapema. Kuna aina nyingi za fangasi ambao wanaweza kuathiri mwili wa binadamu.

 

Wapo fangasi ambao wanaonekana kwa macho na wengine hawawezi kuonekana. Kuna mamilioni ya aina hizi za fangasi, katika hawa kuna kuna mamia ya aina za fangasi ambazo huweza kumfanya mtu kuumwa. Miongoni mwa maradhi yanayoweza kusababishwa na fangasi ni pamoja nna:

  1. Aleji
  2. Mapele na maruturutu kwenye ngozi na vidole
  3. Maambukizi ya mapafu kama pneumonia ambayo hufanana na mafua au kifua kikuu
  4. Maambukizi kwenye mfumo wa damu
  5. Kupata ugonjwa wa meningitis huu ni ugonjwa unaoathiri ubongo pamoja na ugwe mgongo.

 

MAENEO AMBAYO FANGASI WANAISHI

Fangasi huweza kuishi kwenye maeneo mengi kama

  1. Kwenye udongo
  2. Hewa
  3. Kwenye mimea
  4. Kwenye ngozi za watu
  5. Na ndani ya miili ya watu

AINA ZA FANGASI

Fangasi wamegawanyika katika makundi mengi. Na wamekuwa wakisababisha maradhi mblimbali na katika sehemu mbalimbali za miili yetu. Hapa nitakutajia aina za fangasi hawa kama ifuatavyo:-