Darsa 5: Kujiepusha na tabia za unafiki na kutimiza ahadi
Katika Darsa hii tutajifnza kuhusu kujiepusha na tabia za unafiki na kitimiza ahadi.
Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu. Rehema na amani zimshukie Mtume Muhammad ﷺ, familia yake, maswahaba wake na wote wanaofuata mwongozo wake mpaka Siku ya Kiyama.
Ndugu zangu Waislamu, leo tutakumbushana kuhusu kujiepusha na tabia za unafiki. Muislamu wa kweli anatakiwa kuwa mkweli, mwaminifu na mtu wa kutimiza ahadi zake. Tabia hizi humfanya apendwe na Mwenyezi Mungu na kuheshimika mbele ya watu.
Abu Hurairah, Mwenyezi Mungu amridhie, amepokea kuwa Mtume Muhammad ﷺ alisema kuwa alama za mnafiki ni tatu. Anapozungumza husema uongo, anapoahidi havunji ahadi, na anapoaminiwa hufanya khiyana. Katika riwaya nyingine imeongezwa kuwa hata kama mtu huyo anafunga, anaswali na anajidai kuwa ni Muislamu, tabia hizo hubaki kuwa ni alama za unafiki. Hadithi hii imepokewa na Imam Bukhari na Imam Muslim, na imo katika Riyadh As-Swalihin, Hadithi namba 688.
Pia Abdullah bin Amr bin Al-Aas, Mwenyezi Mungu amridhie, amepokea kuwa Mtume Muhammad ﷺ alisema kuwa mwenye kuwa na sifa nne huwa ni mnafiki kamili. Sifa hizo ni kufanya khiyana anapoaminiwa, kusema uongo anapozungumza, kuvunja ahadi anapoahidi, na kutumia matusi au dhuluma anapogombana. Mwenye kuwa na sifa moja miongoni mwa hizo anakuwa na sehemu ya unafiki mpaka atakapoiacha. Hadithi hii imepokewa na Imam Bukhari na Imam Muslim, na imo katika Riyadh As-Swalihin, Hadithi namba 689.
Aidha, Jabir, Mwenyezi Mungu amridhie, ameeleza kuwa Mtume Muhammad ﷺ alimwahidi kumpa sehemu ya mali ya Bahrain itakapofika. Mtume alipofariki kabla mali hiyo haijafika, Abu Bakr, Mwenyezi Mungu amridhie, alitekeleza ahadi hiyo kwa ukamilifu. Hadithi hii imepokewa na Imam Bukhari na Imam Muslim, na imo katika Riyadh As-Swalihin, Hadithi namba 690.
Ndugu zangu, Uislamu unatufundisha kuwa ukweli, uaminifu na kutimiza ahadi ni maadili ya Waumini. Tujiepushe na uongo, tusivunje ahadi na tusifanye khiyana kwa amana tulizopewa. Hata tunapokuwa na tofauti na watu, tuendelee kuwa na heshima na kutumia maneno mazuri.
Mwenyezi Mungu atujalie tuwe miongoni mwa wenye ukweli, wenye kutimiza ahadi na wenye kuhifadhi amana, na atuepushe na tabia za unafiki.
Wassalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 web hosting 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Hadithi Muhimu Kuhusu Ndoa Katika Uislamu
Ndoa katika Uislamu ni mkataba mtakatifu (mithaqan ghaliza) unaounganisha watu wawili kwa lengo la kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu, utulivu wa nafsi, na kuendeleza kizazi. Makala hii inachambua Hadithi muhimu za Mtume Muhammad (S.A.W) zinazotoa mwongozo kuhusu vigezo vya kuchagua mwenzi, haki za wanandoa, na umuhimu wa kuhifadhi mahusiano haya kwa upendo na busara.
Soma Zaidi...Zijuwe nyakati ambazo ukiomba dua hujibiwa kwa urahisi
Post hii inakwenda kukugundisha ni nyakati zipi ambazo Allah hukubali dua kwa urahisi.
Soma Zaidi...Dua sehemu ya 04
Soma dua mbalimbali za kila siku ambazo unatakiwa uzijuwe. Dua 120 ambazo muislamu anatakiwa kuzijua
Soma Zaidi...