image

Dalili za mwanzo za HIV/UKIMWI

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mwanzo za HIV/UKIMWI

DALILI ZA MWANZO ZA HIV AMA UKIMWDalili hizi huanza kuonekana kuanzia wiki mbili mpaka nne na wakati mwingine mpaka sita toka kuingia mwilini. Mara chache sana huweza kuonekana mwanzoni mwa wiki ya kwanza. Katika kipindi hiki mtu anaweza kuona dalili zifuatazo:1.kufimba kwa tezi za kwenye makwapa, mapaja na shingo2.Homa3.Uchovu4.Kuharisha5.Kupungua uzito6.Kikohozi7.Pumzi kutoka kidogodogo8.Mafua

Dalili hizi pia zinaweza kuhusiana na maradhi mengine, hivyo inaweza kuwa vigumu kujuwa nini chanzo zaidi. Wengi katika wanaopata HIV wametaja kuwa kuvimba kwa tezi ndio dalili pekee walioweza kuopata mwanzoni mwa kuathirika kwao. Wengine wanataja mafua kuwa ndio dalili yao ya kwanza.

 

Baada ya kipindi hiki kupita mgonjwa hatapata dalili yeyote ile. Hiki ni kipindi hatari sana kwani mtu hataweza kujijua kama ameathirika. Kipindi hiki kinaweza kudumi mpaka miaka 10. katika kipindi hiki virusi vinaendelea kuathiri seli za mwili. Baada ya mwili kuwa umeathirika sana na kudhoofu mtu ataanza kupata dalili za UKIMWI.

 

DALILI ZA UKIMWI1.kutokwa na jasho jingi wakati wa usiku2.Kupata homa za mara kwa mara na kuhisi baridi3.Kikohozi4.Kushinwa kupumua vyema5.Madoa madoa kwenye ulimi na mdomoni6.Maumivu ya kichwa7.Uchovu usiokuwa na sababu na usioisha8.Kutokuona vyema9.Kupungua uzito10.Mapele na ukurutu kwenye ngozi





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 840


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-