Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kisukari Aina ya kwanza ambapo kwa kitaalamu huitwa Diabetes type 1, ni hali ambayo utokea ambapo mwili ushindwa kutengeneza insulini ambayo uweka sukari kwenye hali ya usawa.
Aina ya kwanza ya kisukari.
1.Ugonjwa huu wa kisukari utokea kwa Aina kuu mbili, Aina ya kwanza ni pale ambapo mwili inashindwa kabisa kuzalisha insulin kwa hiyo mgonjwa maisha yake yote anaishi kwa kuchomwa insulin, kwa hiyo mgonjwa anaishi kwa kutumia insulin maisha yake yote, hii Aina ya kisukari pengine mtu anazaliwa nayo na maisha yake yote anaishi kwa kutumia insulini Ili iweze kuweka kiwango Cha sukari katika usawa. Kwa hiyo mgonjwa anapaswa kujua hali yake kwa ujumla Ili kuweza kushika masharti yabayohitajika.
2. Ugonjwa huu wa kisukari Aina ya kwanza usababishwa na kuaribika kwa seli ambazo zimo kwenye kongosho seli hizi kwa kitaamu huitwa beta seli na Alfa seli ambazo kazi zake ni kuweka kiwango Cha sukari kwenye hali ya usawa, kwa hiyo hii Aina ya kisukari ni shida kuiweka sawa bila kutumia insulini, kwa hiyo tunapaswa kuwa waaminifu katika kutumia insulin mara nyingi hii Aina ya kisukari kama mtu hajazaliwa nayo ugundulika pale mtu akiwa na miaka chini ya thelathini.
3. Kuna sababu ambao upelekea kuwepo kwa ugonjwa huu kama vile , Kuna wakati mwingine mwili uzalisha antibodies ambazo uharibu beta seli zinazokuwepo kwenye kongosho kwahiyo antibodies hizi zinafanya seli ambazo zimo kwenye kongosho kushindwa kufanya kazi yake na baadae sukari kwenye mwili inashindwa kuwa sawa na hatimaye insulin utumika kila siku kwa mgonjwa na kusaidia kuweka sukari katika hali ya usawa. Na kufanya maisha ya mtu kuendelea kuwa kawaida.
4.pengine hali hii ya kuwepo kwa Aina hii ya kwanza ni kwa sababu za kuurithi kutoka kwenye familia kwa sababu Kuna familia ambapo Kuna Aina hii ya sukari Aina ya kwanza kwa sababu ya gene pengine Kuna shida katika kufanya kazi katika kongosho ambalo usababisha seli zinashindwa kufanya kazi yake kwa sababu ya kuridhi kutoka katika familia. Kwa hiyo tunapaswa kuwa macho na kuchunguza matatizo haya kama yako kwenye ukoo na kuyafanyia kazi.
5. Sababu nyingine ya chanzi Cha kuwepo kwa Aina ya kwanza ya sukari ni Ile hali ya kumpatia mtoto mapema kuanza kutumia maziwa ya ngombe na kutumia madini ya nitrate usababisha kuaribika kwa seli ambazo zimo kwenye kongosho kwa hiyo watoto wanapaswa kula kwa mda mwafaka na kuzuia kutumia maji yenye nitrate na mtoto kama hakufanikiwa kupata maziwa ya Mama kwa sababu mbalimbali anapaswa kuonana na wataalam wa afya Ili kumwonyesha maziwa anavyopaswa kutumia siyo kutumia maziwa ya ngombe kwa mda mrefu.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Je na wewe ni katika wanaosumbuka sana kujuwa dalili za kwanza za ukimwi toka siku ya kwanza, ama dalili za ukimwi kwenye ulimi, ama unatakakujuwa ni muda gani ukimwi huonekana, na je ukishiriki ngono zembe ndio utapata ukimwi? Basi makala hii ni kwa ajil
Soma Zaidi...posti hii inahusu dalili za Homa ya Manjano ni maambukizi ya virusi yanayoenezwa na aina fulani ya mbu. Maambukizi hayo ni ya kawaida zaidi na kuathiri wasafiri na wakazi wa maeneo hayo.
Soma Zaidi...Mvurugiko katika mfumo wa chakula mwilinivunaweza kusababisha maumivu ya tumbo, kuharisha, kutapika na kuchoka pia. Lakini zipo sababu nyingine kama kuwana ujauzito. Nini ufanye endapo unasumbuliwana hali hii
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa kisonono, ni ugonjwa unaosababishwa na mdudu ambaye kwa kitaalamu huitwa Neisseria gonococcal.
Soma Zaidi...Posti hii inaonyesha kiufupi kabisa madhara ya minyoo kwenye mwili wa binadamu. Yafuatayo Ni madhara ya minyoo;
Soma Zaidi...Magonjwa ya kuambukiza ni maradhi yanayosababishwa na vijidudu kama vile bakteria, virusi, fangasi au vimelea. Viumbe vingi vinaishi ndani na kwenye miili yetu. Kwa kawaida hazina madhara au hata kusaidia, lakini chini ya hali fulani, baadhi ya viumbe
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia au hatua tatu muhimu anazopitia Mgonjwa wa gauni, kuanzia kwa Maambukizi mpaka kwenye hatua ya mwisho hasa kama Ugonjwa huu haujatibiwa mapema.
Soma Zaidi...Karibia fangasi wote hawa wanatibika bila ya ugumu wowote maka mgonjwa atakamilisha dozi.
Soma Zaidi...