DALILI KUU ZA MIMBA (UJAUZITO) Watu wengi sana wamekuwa wakilalamika kuwa mimba zao zinatoka, ama kupotea bila ya kujulikana tatizo wala bila ya kuugua.
DALILI KUU ZA MIMBA (UJAUZITO)
Watu wengi sana wamekuwa wakilalamika kuwa mimba zao zinatoka, ama kupotea bila ya kujulikana tatizo wala bila ya kuugua. Wapo wengine wanakujakujitambua ujauzito ukiwa na miezi kadhaa. Sasa ni zipi hasa dalili za ujauzito?. huenda swali hili kwa wanawake walio wengi lisiwe na manufaa kwao kwani tajari ni wajuzi wa swala hili. Halikadhalika wanaume wengi wanaujuzi pia. Kwani wengi wanaelewa kuwa dalili ya ujauzito ni kukosekana kwa siku za mwanamke yaani hedhi kwa vipindi zaidi ya kipoja. Lakini itambulike kuwa hii sio dalili pekee, kwani siku zinaweza kukosekana na isiwe mimba. Katika makala hii tutakwenda kuonesha kwa utani dalili kadhaa za ujauzito.
Kabla ya kiziona dalili hizo ningependa kutumia muda kidogo kueleza tatizo la kukosa kwa hedhi. Hedhi ni muhimu kwa kila mwanmke ambaye amefikia umri wa kupata ujauzito. Afya ya mwanmke huyu huwa salama kama hedhi yake ipo salama. Kwa kawaida hedhi huweza kukatika yaani kukata kutoka kabisa pindi umri wa mwanamke unapokuwa mkubwa yaani kuanzia miaka ya 45 na kuendelea. Katika kipindi hiki mwanamke huyu kupata tatizo la kutokupata siku zake ni la kawaida sana, ama siku zake kutokuwa na mpangilio maalumu.
Kwa wanawake walio wadogo kukata kwa hedhi kuna sababi nyingi sana. Watu wengi wamezoea kuwa lamda kupata ujauzito ndio sababu ya kutokupata siku zake. Hii sio swa kabisa. Kukata kwa siku za mwanamke kunaweza kusababishwa na maradhi kama kisukari na baadhi ya maradhi yanayoipata ovari ya mwanamke. Ovari ndio sehemu pekee ya mwanamke ambayo mayai huzaliwa. Hivyo sehemu hii ndio ambayo inatoa homoni ambazo huchochea upatikanaji wa hedhi ama huzuia hedhi isipatikane kutokana na kupata ujauzito. Pia matumizi ya njia za uzazi wa mpango huweza kusababisha tatizo hili la kutokuona siku zake mwanamke. Matumizi ya vyakula, hali ya hewa na madawa ni katika visababishi vikuu vya kutokupata hedhi kwa muda sahihi.
Baada ya kugusia kidogo kipengele hiko sasa tukaone baadhi ya dalili za ujauzito. Kwa hali ya kawaida dalili hizi huweza kuwa tofauti kwa mwanamke mmoja hadi mwingine. Ijapokuwa hali ni kama hii pia zipo dalili ambazo huwapata karibia wanawake wote:-
Kuonekana kwa damu iliyo chache. Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa asilimia 25% (yaani robo) ya wanawake wote wanaopata ujauzito hutokwa na damu kidogo, na rangi ya damu hii haikuiva kama ile ya hedhi. Damu hii hutokea siku 6 mpaka 12 baada ya kutungwa kwa mimba. Ila kwa wanawake walio wengi huiona damu hii kwenye wiki 12 za mwanzo za ujauzito.
Kujaa au kuuma kwa chuchu; mwanzoni mwa wiki ya 1 mpaka ya 2 ya ujauzito mwanamke anaweza kuona kuwa matiti yake yanajaa ama kuwa mazito tofauti na kawaida. Wanawake wengine chuchu za matiti yao zinakuwa ngumu na huwa zinajaa. Wanawake wengine wanaona chuchu ama maziwa yao huwa kama na maumivu wakiyaminya.
Uchovu usio wa kawaida; karibia wanawake wote wanaopata ujauzito huhisi uchovu usio wa kawaida. Mara nyingi dalili hii hutokea mwanzoni mwa wiki ya kwanza toka kupata kwa ujauzito. Na hii ni kutokana na kuwa mwili unazalisha homoni za kuweza kuufanya mwili uweze kulea ujauzito, upatikanaji nwa maziwa kwa ajili ya mtoto ajae. Pia kwa kuwa mwili wa mama unaongeza kuwango cha usukumaji wa damu, hivyo uchovu kutokea ni hali ya kawaida.
Mwanzoni mwa wiki ya kwanza ya ujaozito, mwanamke anaweza kupatwa na maumivu ya ghafla ya kichwa. Na hii ni kutokana kuwa mwili umeongeza kazi ya uzalishaji wa homoni, hivyo ongezeko hili linaweza kusababisha maumivu ya kishwa. Hali si kwa siku nyingi hali hii itapotea.
Kutapika; kwa kawaida hii hali huwapata wanawake wenye ujauzito kuanzia wiki ya pili mpaka wiki ya nane. Kitaalamu hali hii hutambulika kama โmorning sicknessโ. na huenda hali hii ikaendelea katika kipindi chote cha ujauzito.
Kukojoa mara kwa mara; hali hii hutokea kwa sababu mwili huzalisha homoni iitwayo human chorionic gonadotropin ambayo hii huongeza damu kupita maeneo ya chini yaani kuzunguka sehemu za siri, hivyo hali hii hupelekea mwanamke kwenda kukojoa mara kwa mara.
Kutokupenda baadhi ya vitu ama vyakula. Hii hutokea kwa ghafla mwanamke anachukia baadhi ya vitu ama hususani vyakula bila ya sababu yotyote.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa maziwa kwa akina Mama wakati wa ujauzito ni kawaida kwa sababu ya kuzaliwa kwa homoni ambayo usaidia kutoa maziwa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi ya mdalasini katika matibabu ya homoni kwa wanawake.
Soma Zaidi...Tafiti zinaonesha kuwa karibia asilimia 10% mpaka 25% ya wanawake wanaopata ujauzito, mimba zao hutoka.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi maelekezo muhimu kwa mama au mlezi wa mtoto mgonjwa. Ni maelekezo muhimu hasa wakati wa kutoa dawa kwa mtoto.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kutunza joto la mtoto mara tu anapozaliwa,tunajuwa wazi kuwa Mama anaweza kujifungulia sehemu yoyote ile kabla hajafika hospitalini kwa hiyo mtoto anapaswa kuwa na joto la mwili la kutosha i
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa mabonge ya damu wakati wa hedhi, tunajua kabisa wakati wa hedhi damu inapaswa kuwa nyepesi na ya kawaida ila kuna wakati mwingine inakuwa na mabonge zifuatazo ni sababu za kuwepo kwa mabonge ya damu wakati wa hedhi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu msaada kwa mwenye maumivu ya tumbo la hedhi, hizi ni huduma ambazo utolewa kwa wale wenye maumivu ya tumbo la hedhi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi siku za kubeba mimba na zisizo za kubeba mimba , tunapaswa kujua hivi Ili kuweza kupanga uzazi na kuepuka njia ambazo ni hatarishi kwa afya zetu.
Soma Zaidi...Mimba inaweza kutoka kutokana na maradhi, majeraha ama misukosuko mimgine. Kutoka kwa mimva haimaanishi ndio mwisho wa kizazi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuzuia Malaria kwa wajawazito na watoto wao wakiwa bado tumboni, tunajuwa wazi kuwa wajawazito wakipata Malaria inaweza kupelekea mimba kutoka kwa hiyo ili kuzuia tatizo hili zifuatazo ni njia zilizowekwa ili kuz
Soma Zaidi...