Hizi ndio suna za swala kwa swala za faradhi na suna

Hizi ndio suna za swala kwa swala za faradhi na suna

Sunnah za Swala


Vipengele vya sunnah katika swala ni vile ambavyo mwenye kuswali akivitenda husaidia sana kukuza daraja ya swala yake na kuipa nguvu na msukumo mkubwa wa kuiwezesha kufikia lengo lililokusudiwa kwa urahisi zaidi. Ama mwenye kuswali akiacha kipengele chochote katika vipengele vya sunnah, swala yake itakamilika iwapo atatekeleza vipengele vyote vya nguzo. Katika Hadith tumeona kuwa Mtume (s.a.w) katika swala yake pana vipengele vya ziada ya nguzo kama ifuatavyo:


1.Kuinua viganja vya mikono mkabala na mabega, usawa wa vigingi vya masikio wakati wa kuhirimia swala, kwenda kwenye rukuu, baada ya rukuu na baada ya kutoka kwenye Tahiyyatu ya kwanza.
2.Kusoma dua baada ya takbira ya kuhirimia.
3.Kuanza na a 'udhubillaah (kumlaani Shetani) kabla ya kuanza kusoma suratul-Fatiha.
4.Kuitikia 'Aamin'baada ya kumaliza Suratul Fatiha.
5.Kusoma aya za Qur-an baada ya Suratul-Fatiha katika rakaa mbili za mwanzo.
6.Kuleta Tasbih, Tahmid na dua katika rukuu, itidali na s ijda.
7.Kutoa takbira katika kubadilisha kitendo kimoja kuendea kingine isipokuwa tu kutoka kwenye rukuu kwenda kwenye itidali ndipo tunaposema: 'Sami'Allahu liman hamidah - Rabbanaa lakal-hamdu'.
8.Kukaa na kusoma Tahiyyatu kila baada ya rakaa mbili, kwa swala zenye rakaa zaidi ya mbili.
9.Kusoma dua baada ya kumswalia Mtume na kabla ya kutoa S a la am.




                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 188

Post zifazofanana:-

Chemsha bongo namba 08
20. Soma Zaidi...

DARASA LA AFYA NA AFYA YA UZAZI
Jifunze mengi kuhusu Afya, kuwa nasi kwenye makala hii hadi mwisho. Soma Zaidi...

Hadithi ya Mshona nguo
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula ubuyu
Soma Zaidi...

DARASA LA VYAKULA, MBOGA, MATUNDA NA VIRUTUBISHO
Soma Zaidi...

Taqwa (Hofu ya kumuogopa Allah) ni popote ulipo
' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '... Soma Zaidi...

FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA BAMIA (OKRA)
Makala hii inakwenda kukuonyesha faida za kula bamia kwa afya afya Soma Zaidi...

swala ya witri na namna ya kuiswali
3. Soma Zaidi...

NINI CHANZO CHA UGONJWA WA MALARIA? NI YUPI MBU ANAYESAMBAZA MALARIA
Malaria husababishwa na vimelea (parasite) ambavyo husambazwa ama kubebwa na mbu aina ya anopheles. Soma Zaidi...

kwa nini riba ni haramu?
Soma Zaidi...

Vyakula vya fati na mafuta na kazi zake
Soma Zaidi...

Dalili (Alama) za Qiyama
Soma Zaidi...