Swala za tahajud na namna ya kuziswali

4.

Swala za tahajud na namna ya kuziswali

4. Swala ya Tahajjud



Swala ya Tahajjud ni miongoni mwa swala zilizokokotezwa sana katika Qur-an na Hadithi. Neno 'Tahajud' lina maana ya kuamka kutoka usingizini. Swala hii huswaliwa usiku wa manane, hasa katika theluthi ya mwisho wa usiku karibu na al-Fajiri.



Swala hii vile vile hujulikana kwa jina la 'Qiyaamul-layl'. Yaani kisimamo cha usiku kwa sababu inakuwa na visimamo virefu ambapo Qur-an husomwa kwa urefu. Mkokotezo wa swala ya Tahajjud unadhihirika katika aya za Qur-an zifuatazo:


Na katika usiku jiondoshee usingizi (kid ogo) kwa (kusoma) hiyo (Qur-an ndani ya Swala).Hiyo ni (Ibada) zaidi kwako. Huwenda Mola wako akakuinua cheo kinachosifika. (17:79).



Miongoni mwa sifa za waja wema wa Allah (s.w) ni pamoja:


'Na wale wanaopitisha baadhi ya saa za usiku kwa ajili ya Mola wao kwa kusujudu na kusimama '. (25:64).
J e , afanyaye ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama na kuogopa Akhera na kutarajia rehema ya Mola wake (ni sawa na asiyefanya hayo)? Sema: 'Je, wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?' Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu. (39:9)


Pia Mtume (s.a.w) amekokoteza Swala za Usiku kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo.



Abu Umamah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Jizoesheni kusimama Usiku (kwa swala) kwa sababu ilikuwa ndio tabia ya Wacha-Mungu w aliokutangulieni na ni njia ya kukukurubisheni karibu na Mola wenu na ni njia ya kufutiwa dhambi na ni kizuizi cha kutenda maovu (dhambi)'. (Tirmidh).



Idadi ya rakaa alizoswali Mtume (s.a.w) katika hii swala ya Tahajjudi ni nane (8) na kisha akamalizia na rakaa tatu za Witri. Katika hizi rakaa nane alitoa salam kila baada ya rakaa mbili. Mtume (s.a.w) alikuwa akisoma Qur-an kwa kitambo kirefu kwa kila rakaa kiasi kwamba miguu yake ilikuwa inavimba kama tunavyojifunza katika Hadithi ifuatayo:-



'Mughirah (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) alikuwa akisimama katika (sw ala ya usiku) kwa kitambo kirefu kiasi kw amba miguu yake ilivimba, akaulizwa: Kwanini unafanya hivi ambapo umesamehewa dhambi zako zilizotangulia na zitakazokuja? Akauliza: 'Nisiwe mja mwenye Shukrani?' (Bukhari na Muslim).




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1966


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Dhamana ya Kuchunga Ahadi Katika Uislamu
Kuchunga'au kutekeleza'ahadi'ni miongoni mwa vipengele muhimu vya tabia ya muumini wa kweli. Soma Zaidi...

DARSA ZA QURAN
DARSA ZA QURAN 1. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII IBRAHIIM(A.S) NA KUANDALIWA KWAKE:
Nabii Ibrahiim(a. Soma Zaidi...

UANDISHI WA HADITHI WAKATI WA TABI'INA
Wakati wa Wafuasi wa masahaba (Tabi'ina)101-200 A. Soma Zaidi...

Nabii Yunus(a.s) Amuomba Allah(s.w) Msamaha
Ndani ya tumbo la samaki, Nabii Yunus(a. Soma Zaidi...

Hukumu na taratibu za ndoa katika uislamu
Soma Zaidi...

HUKUMU ZA KUSOMA QURAN, HUKUMU ZA TAJWID, HUKUMU ZA NUN SAKINA, MIM SAKINA, QLQALA NA IQLAB, TANWIN NA MADA
Soma Zaidi...

Hukumu ya Mtu asiyefunga kwa makusudi mwezi wa ramadhani
Soma Zaidi...

HUKUMU ZA MADD YAANI KUVUTA HERUFI KWENYE USOMAJI WA QURAN
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

kuwa mwenye huruma na faida zake
25. Soma Zaidi...

maana ya swala kilugha na kisheria
Soma Zaidi...

Namna ya Kutayamam hatua kwa hatua, suna zake nguzo za kutayamam na masharti ya kutayamam
Soma Zaidi...