Madhara ya matusi katika jamii, na Kujiepusha na Matusi

15.

Madhara ya matusi katika jamii, na Kujiepusha na Matusi

15. Kujiepusha na Matusi


Mtu anayetukana ana lengo la kumdhalilisha mwingine. Waislamu tumekatazwa kutukanana na hata kuitana majina tusiyoyapenda kwa k ej eli.
'.... Wala msitukanane kwa kabila wala msiitane majina mabaya (ya kejeli). Jina baya kabisa kuitwa mtu ni 'Fasiqi' baada ya kuwa yeye ni Muislamu. Na wasiotubu basi hao ndio madhalimu '. (49:11)


Fasiq ni yule aliyebobea katika uasi. Yaani mtu anayejizatiti kumuasi Allah (s.w) kwa namna mbali mbali kama vile mwizi, mlevi,

mzinzi na kadhalika. Ni vibaya mno mbele ya Allah (s.w) kumsingizia au kumwita Muislamu 'mwizi' na huku si mwizi au kumwita 'mnafiki' au 'kafir' na huku ni Muislamu kamili. Tabia hii imekemewa vikali katika Qur-an:

'Kwa yakini wale wanaopenda uenee uovu kwa wale walioamini watapata adhabu iumizayo katika dunia na katika akhera, na Allah ndiye ajuaye, na nyinyi hamjui'. (24:19).
Kutokana na makemeo haya, Muumini wa kweli hana budi kujiepusha na tabia ya kuwaita watu kwa majina mabaya kwani kufanya hivyo mtu hujilaani mwenyewe kiasi kwamba hayo majina mabaya yatamgeukia, kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo:
Abu Dh-dhari(r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Hapana mtu atakayemsingizia mwingine uasi kwa Allah au akamwita 'kafiri', ila hayo yatamgeukia yeye mwenyewe iwapo huyo aliyemsingizia hayuko hivyo'. (Bukhari)



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 142

Post zifazofanana:-

Kuamini Mwenyezi Mungu sio suala la Kibubusa au Kufuata Mkumbo
Kuamini Mwenyezi Mungu sio suala la Kibubusa au Kufuata Mkumbo. Soma Zaidi...

Dua sehemu ya 04
Soma dua mbalimbali za kila siku ambazo unatakiwa uzijuwe. Dua 120 ambazo muislamu anatakiwa kuzijua Soma Zaidi...

MAFUNZO YA QURAN: QURAN NA SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Soma Zaidi...

VIRUSI VYA KORONA AU CORONA (CORONAVIRUS)
Virusi vya korona ni katika aina za virusi ambavyo asili yake ni kutoka kwa wanyama na kuja kwa binadamu. Soma Zaidi...

TEKNOLOJIA, HABARI NA MAWASILIANO
Soma Zaidi...

Hawa ndio waaasi wakwanza wa Dola ya kiislamu wakati wa makhalifa
Soma Zaidi...

Kibri cha Ibilis na Uadui Wake Dhidi ya Binadamu
Ibilis ni katika jamii ya majini aliyekuwa pamoja na Malaika wakati amri ya kumsujudia Adam inatolewa. Soma Zaidi...

Yusufu Aokotwa na Kuuzwa nchini Misri
Huko nyuma wapita njia walikisogelea kisima kwa lengo la kuteka maji. Soma Zaidi...

Ni zipi siku ambazo ni haramu kufunga? na ni kwa nini hairuhusiwi kufunga katika siku hizo
Soma Zaidi...

TAREKH, HISTORIA NA SIRA YA UISLAMU NA MTUME MUHAMMAD KUTOKA KUZALIWA MPAKA KUFARIKI NA HARAKATI ZAKE
1. Soma Zaidi...

umuhimu wa swala katika uislamu
Soma Zaidi...

HADITHI YA KAKA WA SITA WA KINYOZI
Soma Zaidi...