picha

Kuepuka Maongezi yasiyo na Maana

12.

Kuepuka Maongezi yasiyo na Maana

12. Kuepuka Maongezi yasiyo na Maana


Maongezi au mazungumzo yasiyo na maana ni yale yasiyoleta manufaa au kheri yoyote ila hasara tu. Mazungumzo haya yapo katika kupiga soga, kupiga porojo, kupiga hadithi za pauka pakawa, kutaniana, kubishana, na mengine ya namna hiyo. Mara zote mazungumzo ya aina hii huwapelekea watu kusengenya, kusema uwongo, kufitinisha, kugombana na kupoteza muda. Aidha mazungumzo ya aina hii huwasahaulisha watu kumkumbuka Allah (s.w).
Muumini hana budi kujiepusha na tabia hii ya kujiingiza kwenye mazungumzo ya upuuzi. Miongoni mwa sifa za waumini ni pamoja na kujiepusha na mambo ya upuuzi kama tunavyojifunza katika Quran:


“Hakika wamefuzu Waumini. Ambao katika Sw ala zao ni wanyenyekevu. Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi”. (23:1-3).
Waja wema mbele ya Allah ni pamoja:

“Na wale ambao hawashuhudii uwongo na wanapopita penye upuuzi hupita kwa heshima (zao). (25:72).
Muislamu anashauriwa daima abaki kimya kama hana la maana la kuzungumza. Mtume (s.a.w) ametuusia:
“Kuwa kimya. Hii ni njia ya kumfukuza shetani na kuimarisha dini yako” (Ahm ad).

“Anayekuwa kimya (anayenyamaza wakati hana la maana la kuzungumza) atakuw a salama ”. (Ahmad, tirmidh).
“Ni jambo bora mno kwa Muumini kuacha yasiyomhusu” (Ma lik, Ahm ad, Tirm idh).
“Ni katika ubora wa Imani ya mtu kwa kuacha kujihusisha na mambo ya upuuzi”. (Tirm idh).



                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sunnah Main: Post File: Download PDF Views 1548

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Bongolite - Game zone - Play free game     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Dua za Mitume na Manabii     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zinazofanana:

NAMNA AMBAZO DUA HUJIBIWA

NAMNA AMBAYO ALLAH HUJIBU DUA.

Soma Zaidi...
Je! inajuzu wanawake kuzuru makaburi?

As salaam alaykum warahmatullah wabarakatuh, nauliza inajuzu wanawake kuzuru makaburi?

Soma Zaidi...
Wajbu wa wazazi kwa watoto wao

Wajibu wa Wazazi kwa Watoto Wazazi wanawajibu kwa watoto wao.

Soma Zaidi...
Hukumu ya kukusanyika kwenye dua na umuhimu wa dua ya watu wengi

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kukusanyika katika kuomba dua.

Soma Zaidi...
AINA ZA HADITHI

Aina za HadithKuna aina kuu mbili za Hadith- (a) Hadith Nabawiyyi.

Soma Zaidi...