Sheria Katika Uislamu

Sheria Katika Uislamu

4.

Sheria Katika Uislamu

4.2 Sheria Katika Uislamu

? Maana ya Sheria

Kilugha: njia ya Kufuata

Kimatumizi: ni taratibu, sharti, kanuni na amri zilizowekwa kuongoza jamii.



Kazi ya Sheria katika Jamii

i. Kulinda binaadamu binafsi dhidi ya madhara mbali mbali ya mwenendo wake mbaya.
ii. Kulinda na kuhifadhi maisha ya watu na mali au rasilimali zao kutokana na kuuliwa, kujeruhiwa, kuharibiwa, kuibiwa, n.k bila sababu ya msingi.
iii. Kuhifadhi na kulinda amani na usalama katika jamii kutokana na migongano, vurugu, n.k.
iv. Kuhifadhi na kulinda maadili ya jamii kama njia ya msingi ya kumbakisha mwanaadamu katika mwenendo mema.
v. Kuweka na kupanga utaratibu wa namna ya kuendesha shughuli na maisha ya kila siku kibinafsi na kijamii.
vi. Sheria ya Kiislamu ina kazi ya kulinda na kuhifadhi misingi mitano ya mwanaadamu ambao ni; imani, uhai, akili, heshima na hadhi na mali.




Chimbuko la Sheria za Kitwaghuti

- Zimetungwa na binaadamu kwa kutumia vipawa vya akili, elimu, mila, desturi, uzoefu, mazingira na matashi ya nafsi zao.

- Katiba ndio msingi (chombo) mkuu wa sheria za Kitwaghuti ambayo hugawanya utekelezaji wake katika vyombo vikuu vitatu;
1. Bunge (Legislature) – chombo kikuu cha kutunga sheria

2 Serikali (Executive) – chombo kikuu cha utendaji

3 Mahakama (Judiciary) – chombo kikuu cha kutafsiri sheria na kutoa haki.



Udhaifu wa Sheria za Kitwaghuti

- Pamoja na mwanaadamu kupewa na vipawa vya akili, ujuzi, elimu, n.k bado ana madhaifu mengi kama ifuatayo;
i. Mwanaadamu ana ujuzi wa mambo machache sana juu ya ulimwengu na yale yanayomzunguka.
Rejea Qur’an (17:85)

ii. Mwanaadamu anaathiriwa sana na matashi ya ubinafsi, uchoyo, upendeleo, chuki, n.k.
iii. Binaadamu wametofautiana mno katika fikra, uoni, vipawa, uzoefu

(mazoea).

iv. Mwanaadamu pia anaathiriwa sana na mabadiliko ya kimazingira na zama

(nyakati).



- Kutokana na mapungufu haya, usimamizi na utekelezaji wa sheria za kitwaghuti hufanywa na watu wachache (watawala) kwa ajili ya manufaa yao tu.



                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views: 4681

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 web hosting     πŸ‘‰2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     πŸ‘‰3 Simulizi za Hadithi Audio     πŸ‘‰4 Madrasa kiganjani     πŸ‘‰5 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰6 Kitabu cha Afya    

Post zinazofanana:

taratibu na namna ya kutaliki, na mambo ya kuzingatia

Taratibu za Kutaliki KiislamuKama palivyo na taratibu za kuoa Kiislamu ndivyo hivyo pia ilivyo katika kuvunja ndoa.

Soma Zaidi...
sunnah za swala

Sunnah za SwalaSunnah za Swala Vipengele vya sunnah katika swala ni vile ambavyo mwenye kuswali akivitenda husaidia sana kukuza daraja ya swala yake na kuipa nguvu na msukumo mkubwa wa kuiwezesha kufikia lengo lililokusudiwa kwa urahisi zaidi.

Soma Zaidi...
Faida za kuswali swala za sunnah

Hapa utajifunza faida za kuswali swala za sunnah.

Soma Zaidi...