FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA TUNDA PERA

Pera ni tunda bora lakini pia ni dawa, tambua umuhimu wa tunda hili kiafya

FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA TUNDA PERA

FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA TUNDA PERA

Pera ni katika matunda yanayopatikana maeneo mengi duniani. Tunda hili ni katika matunda yenye kutia afya zaidi katika miili yetu hasa kwa wale wenye maradhi sugu. Tunda hili hutumika mapaka majani yeke na kuleta faida nyingi sana. Hata wazee wetu wa zamani walikuwa wakitumia mmea huu kwa ajili ya tiba asili. Sasa hebu tuanze kuziona faida hizo:-

 

  1. pera huweza kushusha kiwango cha sukari kwenye damu. Ijapokuwa tunda hili lina utamu lakini ni katika matunda ambayo ni mujarabu kwa kushusha kiwango cha sukari. Hii ni habari njema kwa wenye kisukari na wale wenye tatizo la homoni ya insulin. Hapa tunazungumzia majani ya mpera ni si tunda lenyewe.

 

Katika tafiti iliyofanyiwa watu 19 imethibitisha kuwa kunywa majimaji yatokanayo na majani ya mpera husaidia katika kushusha kiwango cha sukari na athari hii huweza kuendelea mpaka masaa mawili. Tafiti nyingine aliyofanyiwa watu 20 wenye aina ya kisukari type 2 diabetes waliligundulika kuwa kunywa majani ya mpera kumeshusha sukari kwa asilimia 10%.

 

  1. Pera husaidia katika kuimarisha na kulinda afya ya moyo. Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa pera lina mitamini vingi pamoja na antioxdant nyingi. Ambapo kwa pamoja vitu hivi husaidia katika kulinda moyo usiharibiwe na mionz na mambo mengine.

 

Pia kiwango cha madini ya potassium (chumvi) iliyomo kwenye pera pamoja na kambakamba zilizomo kwenye pera husaidia katika kuimarisha afya ya moyo. Pia ulaji wa mapera unaweza kuondoa cholesterol zilizo mbaya (LDL cholesterol) na kuongeza cholesterol nzuri). Hivyo hupunguza nafasi ya kupata maradhi ya shinikizo la damu la juu yaani presha ya kupanda na kupata kiharusi yaani kupalalaizi. (stroke).

 

  1. Husaidia kupunguza maumivu ya tumbo la chango kwa wanawake. Wanawake wengi wanapata maumivu makali wakati wa siku zao. Tafiti zinaonesha kuwa kunywa majani ya mpera husaidia katika kupunguza maumivu haya.

 

Tafiti iliyofanyiwa wanawake 197 ambao huwa wanapata maumivu wakati wa kupata sikuzao, tafiti imeonesha kuwa unywaji wa miligram 6 za maji ya majani ya mpera husaidia kupunguza maumivu haya. Pia utafiti zaidi umeonesha kuwa majani ya mpera husaidi kupunguza maumivu haya mara dufu tofauti na kutumia dawa za kupunguza maumivu. Pia tafiti zinaonesha kuwa majani ya mpera hupunguza maumivu wakati wa kukojoa kwa wale wanaopata maumivu haya.

 

  1. Husaidia katika mmeng’enyo wa chakula. Pera ni katika matunda yenye kambakamba kitaalamu hufahamika kama fiber. Hizi husaidia katika kuboresha mchakato wa kukimeng’enya chakula uende vyema. Hivyo husaidia kutokupata tatizo la kutokupata choo. Tafiti zinaonesha kuwa pera moja hukusanya asilimia 12% ya fiber zinazohitajika mwilini kwa siku.

 

Pia majani ya pera yakitengenezwa majimaji yake husaidia katika kuboresha afya ya mfumo mzima wa mmeng’enyo wa chakula. Kwa wale wenye tatizo la kuharisha majani ya mpera ni mujarabu sana katika kuondoa ama kupunguza tatizo. Pia kuna tafiti nyingi zinaonesha kuwa pera husaidia katika kuuwa vijidudu vibaya ndani ya matumbo yetu.

 

  1. Husaidia katika kupunguza uzito. Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa pera husaidia katika kupunguza uzito. Ni kuwa pera lina calory chache na lina fiber nyingi. Kwa pamoja hizi husaidia katika kumfanya mtu ahisi kushiba mapema na hivyo kumpunguzia kula sana. Hali hii husaidia katika kupunguza uzito mwili.

 

  1. Husaidia kulinda mwili dhidi ya maradhi ya saratani (cancer). Tafiti zinaonesha kuwa pera lina anticancer effect hizi hisaidi sana miili yetu kuzuia uwezekano wa kupata maradhi ya saratani au kansa, pia husaidia kuuwa seli za saratani ndani ya miili yetu.

 

  1. Huboresha mfumo wa kinga mwilini. Pera ni katika matunda yenye vitamini C vingi. Na ijulikane kuwa vitamin C ni katika vitamini ambavyo husaidia kuupa nguvu mwili kwa ajili ya kupambana na maradhi.

 

  1. Huboresha afya ya ngozi. Kwa afya njema ya ngozi, pera ni mujarabu katika kuhakikisha ngozi inabakia salama muda wote. Kuondoa mikunyomikunjo kwenye ngozi, na kuuwa baadhi ya bakteria kwenye ngozi na kuondoa chunjua.

 



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 585

Post zifazofanana:-

Wapinzani wa Ujumbe wa Nabii Salih(a.s)
Baada ya Nabii Salih(a. Soma Zaidi...

NI NINI CHAKULA CHA MINYOO?: maji, vyakula, nyama, udongo, kinyesi, mayai ya minyoo, uchafu wa mwili na mazingira
NI NINI CHAKULA CHA MINYOO? Soma Zaidi...

MAANA YA HADITHI SUNNAH
Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila. Soma Zaidi...

Mgogoro wa kuandama kwa mwezi, Je mwezi wa Kimataifa ama kila Mji na mwezi wake?
Mwezi ukionekana sehemu moja, Waislamu wote ulimwenguni watalazimika kufunga? Soma Zaidi...

Tofauti kat ya sura za Maka na Madina
Sura za Makka na Madina Kutokana na historia ya kushuka kwake sura za Qur-an zimegawanywa katika makundi mawili - sura za Makka na sura za Madina. Soma Zaidi...

ATHARI ZA KUTOKUTIBU MINYOO: maumivu ya tumbo, kichwa, kutapika damu, kichefuchefu, miwasho
ATHARI ZA KUTOKUTIBU MINYOO Kukaa na minyoo na kutoitibu kwa muda mrefu kunaweza kusababisha madhara mengi hususani kwenye ini na maeneo mengine ya mfumo wa kumeng'enya chakula. Soma Zaidi...

UTAMBUE UGNJWA WA UTI DALILI ZAKE, CHANZO NA TAHADHARI DHIDI YAKE
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Sababu za kushuka kwa Surat At-Takaathur
Wanazuoni wengi zaidi wanakubaliana ya kuwa sura hii surat At-Takaathur ilishuka Makka, na hizi ndio sababu za kushuka kwa sura hii Soma Zaidi...

magonjwa na lishe
3. Soma Zaidi...

Faida za kula Embe
Embe ni katika matunda atamu na yenye faida kubwa kiafya, soma makala hii hadi mwisho Soma Zaidi...

Dua ya kuzuru makaburi, na utaratibu wa kuzuru makaburi
Kuzuru makaburi ni katika matendo ya sunah yaani unapata thawabu kwa kwenda klizuru kaburi. Soma Zaidi...

walioruhusiwa kufungua (kula) mwezi wa ramadhani
Soma Zaidi...