Sifa za malaika

Sifa za malaika

Sifa za malaika

Sifa za malaika




Ni viumbe watiifu wasiomuasi Allah(SW)
Malaika ni viumbe watiifu kwa Allah(SW). Wakipewa amri ya kumuadhibu mtu muovu, hawagomi wala kumuonea huruma mtu huyo.Enyi mlioamini! Ziokoeni nafsi zenu na nafsi za watu wenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Juu yake kuna Malaika w akali wenye nguvu.Haw amuasi Allah(SW) katika yale anayowaamuru, na wanatekeleza vile walivyoamrishwa.(66:6)


Wana elimu ya kutosha kutekeleza majukumu yao
Malaika wana elimu inayowawezesha kutekeleza majukumu yao bila ya kubabaisha. Elimu waliyopewa malaika ni sehemu ndogo sana katika ujuzi wa Allah(SW). Na wenyewe walikiri mbele ya Allah(SW)Wakasema: Utukufu ni wako! Hatuna elimu ila ile uliyotufundisha, bila shaka wewe ndiye mjuzi na mwenye hekima(2:32)

Malaika hawana jinsia ya kike wala ya kiume. Qurโ€™an inawakosoa watu wanaodhani kuwa malaika ni wanawake. In a h oji:
Na wamewafanya malaika ambao ni waja wa Mwingi wa Rehma kuwa ni wanawake. Je wameshuhudia kuumbwa kwao(43:19).
Ni viumbe wenye mbawa



โ€œSifa zote njema ni za Allah, Muumba wa mbingu na ardhi. Aliyewafanya malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbili-mbili, na tatu tatu, na nne nne. Huzid is ha katika kuumba apendavyo. Bila shaka Allah ni mwenye uweza juu ya kila kituโ€. (35:1)
Huweza kujimithilisha umbile la mwanadamu
Malaika huweza kujimithilisha kuwa kama wanadamu. Hufanya hivyo pale wanapotumwa na Allah(SW)kuleta ujumbe kwa watu maalumu. Kwa mfano, Bibi Maryam, mama yake nabii Isa(a.s), alijiwa na malaika katika umbo mithili ya mwanaume.Na mtaje katika kitabu, Maryam, alipojitenga na watu wake katika upande wa mashariki.


Tukampelekea Muhuisha sharia Yetu(Jibril) akajimithilisha kwake kwa sura ya binaadamu aliye kamilifu. (19:16-1 7)
Lengo la kuumbwa malaika
Lengo la kuumbwa malaika ni kumtumikia Allah(SW). Katika kutekeleza lengo la kuumbwa kwao, malaika hawana hiyari katika kutekeleza amri za Allah(SW), hufanya mambo yote vile anavyotaka Allah(SW).


..Hawamuasi Allah(SW) katika yale anayowaamuru, na w anatekeleza vile w alivyoamrishw a.(66:6)




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Views: 5406

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Dua za Mitume na Manabii     ๐Ÿ‘‰2 ai web app     ๐Ÿ‘‰3 Kitau cha Fiqh     ๐Ÿ‘‰4 Bongolite - Game zone - Play free game     ๐Ÿ‘‰5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     ๐Ÿ‘‰6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zinazofanana:

Kwanini mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini?

Mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
UMBILE LA MBINGU NA ARDHI

โ€œKatika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana,ziko alama (hoja) za kuonyesha kuwepo Allah (s.

Soma Zaidi...
Kumuamini malaika wa mwenyezi Mungu...

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Udhaifu wa mtazamo wa makafiri juu ya dini dhidi ya mtazamo wa uislamu

Somo Hili linaeleza kuhusu mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Maana ya Elimu katika uislamu na nani aliye elimika?

Hili ni swali kutoka katika maarifa ya elimu ya dini ya kiislamu kidato cha kwanza (EDK FORM 1)

Soma Zaidi...
Mtazamo wa makafiri juu ya dini

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...