Nafasi ya Elimu na wenye elimu katika Uislamu
Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika uislamu inaonkana katika maeneo yafuatayo: Kwanza, Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake.
Nafasi ya Elimu na wenye elimu katika Uislamu
Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika uislamu inaonkana katika maeneo yafuatayo:
Kwanza, Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake.Tunajifunza katika Qur-an kuwa jambo la kwanza alilotunukiwa Adam (a.s) mara tu baada ya kuumbwa kwake ni kupewa elimu.
“Na (Mwenyezi Mungu) akamfundisha Adam majina ya vitu vyote...” (2:3 1)
“Majina ya vitu vyote” katika aya hii inaashiria fani zote za elimu ambazo anahitajia mwanaadamu hapa duniani ili afikie kwa ufanisi lengo la kuumbwa kwake. Pia tunajifunza katika Quran kuwa mwenye elimu na hekima amepewa kheri nyingi.
(Mungu ) humpa hikma amtakaye, na aliyepewa hikma bila shaka amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili. (2.269).
Kutafuta elimu (kusoma) ni amri ya kwanza kwa mwanaadamu. Tunajifunza kutokana na historia ya kushushwa Qur-an kuwa Wahay wa kwanza kumshukia Mtume (s.a.w) ambao ndio ulimtawazisha rasmi kuwa mtume ni ule unaopatikana katika aya tano za mwanzo za Suratul-’Alaq:
“Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba.Ambaye amemuumba mwanaadamu kwa ‘Alaq (kitu chenye kuning’inia). Soma na Mola wako ni karimu sana. Ambaye amemfundisha mwanaadamu kwa kalamu. Amemfundisha mwanaadamu (chungu ya) mambo aliyokuwa hayajui”.(96:1-5)
Kutokana na aya hizi, kwa muhtasari, tunajifunza yafu atayo:
1. Kusoma kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni jambo la kwanza waliloamrishwa wanaadamu na Mola wao.
2. Kusoma kwa jina la Mola wako ni kusoma kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu au ili kuweza kumwabudu Allah(s.w) inavyostahiki na kusimamisha Uislamu katika jamii.
3. Radhi za Mwenyezi Mungu zitapatikana pale mwanaadamu atakapoweza kufikia lengo la maisha yake la kumuabudu Allah (s.w) kwa kuzingatia maamrisho na mipaka ya Mwenyezi Mungu katika kila kipengele cha maisha.
4. Amri hii ya kusoma hailengi fani maalum tu ya elimu; bali kila fani itakayomuwezesha mwanaadamu kufikia lengo la maisha yake kwaufanisi.
5. Chanzo au chimbuko la fani zote za elimu ni Allah (s.w). Hivyo kwa Muislam mlango wa kwanza wa elimu ni kusoma kwa mazingatio Qur-an na hadithi sahihi za Mtume (s.a.w) na kusoma maarifa ya Uislamu kwa ujumla kutokana na vyanzo hivi viwili.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 ai web app 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Dua za kuwaombea wazazi
Kwenye Quran kuna duaambazo Allah ametufundisha tuziombe kwa ajili ya wazazi, familia na kwa ajili yetu wenyewe.
Soma Zaidi...Dua za kuondoa wasiwasi, woga na kujikinga na uchawi, na mashetani
Post hii itakufundisha dua za kuomba wakati wa woga, wasiwasi na kujikinga na wachawi na mashetani
Soma Zaidi...Al-Arbauwn An-Nawawiyyah hadithi ya 6: ubainifu wa halali na haramu
Post hii inakwenda kukupa tahadhari juu ya mambo ya halali na mambo ya haramu.
Soma Zaidi...Ni zipi hadithi sahihi na hadithi Quds
Hapa tutajifunza maana ya hadithi sahihi na hadithi Quds na tofaiti zao.
Soma Zaidi...TANZU ZA HADITHI
Tanzu za Hadith(1) Tanzu ya UsahihiKulingana na kiwango cha usahihi wa Hadith, Hadith zimegawanywa katika makundi makuu manne:(a) Sahihi (b) Hasan/Nzuri.
Soma Zaidi...