Haki na Hadhi za Mwanamke katika jamii za mashariki: China, India na Japani hapo zamani

2.

Haki na Hadhi za Mwanamke katika jamii za mashariki: China, India na Japani hapo zamani

2. JAMII ZA MASHARIKI



Kila jamii utakayoichunguza utakuta kunyanyaswa na kudhalilishwa kwa mwanamke kuko pale pale. Ukichunguza hata zile nchi zilizohesabika katika historia kuwa mbele katika maendeleo ya mwanaadamu kama vile China, India, Iraq na Iran, utasikitishwa na vitimbwi alivyokuwa akifanyiwa mwanamke. Hebu tuanglie baadhi ya jamii chache za nchi za Mashariki.



Uchina
Mwanamke wa Uchina alikuwa hana haki yoyote katika jamii. Hata watoto wake aliowazaa mwenyewe hakuwa na haki nao. Mume wake aliweza kuuza mwili wake kwa mume mwingine. Baada ya mumewe kufariki alirithiwa kama mali na ndugu wa mumewe na haikuwezekana kwake kuolewa tena. Juu ya yote hayo, wanawake waliuzwa na kufanywa watumwa. Mpaka kufikia 1937, Uchina ilikuwa na wasichana watumwa milioni mbili.



Katika kitabu chao kiitwacho, Marriage East and West (New York, 1960) David na Mace wanasema hadhi ya mwanamke huko Uchina ilikuwa duni sana. Mshairi mashuhuri wa China aliyeitwa Xuan,(100B.C) aliandika katika shairi moja:



Ni huzuni ilioje kuwa mwanamke Duniani hakuna kilicho duni Duniani hakuna kilicho duni kuliko mwanamke.
Mwana falsafa wao mkubwa, Bwana Confusious ambaye alikuwa pia kiongozi wa kidini aliwafundisha watu kuwa wajibu mkuu wa mwanamke ni utii. Akiwa mototo amtii baba yake, akiolewa amtii mumewe na akifiwa na mumewe basi amtii mwanawe wa kiume. Na atii kila kitu bila kuhoji. Wachina pia waliamini kuwa mtu akipata mtoto wa kiume amepata hidaya kutoka kwa Mwenyezi Mungu lakini akipata binti, basi ni nuksi.



India
Katika jamii ya India mwanamke hakuthaminiwa kabisa. Mwanamke alihesabiwa kama mashine ya uzazi. Iwapo mwanamke hakujaaliwa kupata mtoto wa kiume kwa mume aliyemuoa, alilazimishwa azini na mume asiyemjua iii apate mtoto wa kiume.



Budha, kiongozi wa kidini huko India aliwafundisha wafuasi wake kuwa mwanamke ni kiumbe duni aliyejawa na dhambi. Hakuna kiumbe anayefaa kuhofiwa na kuepukwa kama mwanamke. Na kwa mujibu wa sheria ya Manu wa huko huko India, wanawake ni lazima wabanwe na kudhibitiwa vikali kwani wao ndio chanzo cha madhambi yote na ufisadi.



Mwanamke hakuna na haki ya urithi bali urithi ulikuwa ni haki ya watoto wa kiume tu. Mke alitakiwa amwite mume wake ama Bwana wangu au Mungu wangu kwani mume alihesabiwa kuwa ni mungu wake hapa duniani. Ilikuwa marufuku mke kula pamoja na mumewe. Jimai hata kati ya mtu na mkewe ilihesabika kuwa ni kitu kiovu na kichafu. Mke mwema alikuwa yule ambaye akili zake, kauli yake na mwili wake si huru. Mke hakuruhusiwa kuolewa tena pindi mumewe akifariki. Ilibidi afanye moja katika mawili, ama ajichome moto ili afe na kumfuata mumewe au awe mtumishi wa shemeji zake hadi atakapo fariki. Mwenendo huu wa kujichoma moto au kuchomwa moto na mashemeji zake bado unaendelea hadi leo. Gazeti liitwalo "The Economist" 27 August - 2 September 1983 liliandika hivi:



The grisly practice of wife burning in India shows no sign of succumbing on its own to modern ideas about the value of a womans ' life. Many women are donsed with kerosene and set aflame by in-laws greedy for more dowries... The official figures shows 610 burnings in 1982.



Tafsiri:
Mwenendo wa kutisha wa kuwachoma moto wanawake huko India hauonyeshi dalili za kukoma kutokana na fikra za kisasa juu ya thamani ya uhai wa mwanamke. Wanawake wengi humwagiwa mafuta ya taa na kuchomwa moto na mashemeji kwa uroho wa kutafuta mahari nyingine. Taarifa rasmi ya serikali yaonyesha kuwa wanawake 610 walichomwa moto mwaka 1982. Hali ilikuwa hivyo hivyo huko Japan.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 119


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

HISTORIA YA NABII DAUD
Soma Zaidi...

HISTORIA YA KUPASULIWA KWA KIFUA AU TUMBO CHA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) AKIWA MTOTO KWA BI HALIMA
KUPASULIWA KWA KIFUA MTUMEWAKATI AKIWA MTOTO. Soma Zaidi...

Nafsi ya mwanaadamu
Soma Zaidi...

DUA ZENYE MANENO HAYA HUJIBIWA
SIFA ZA (MANENO NA MATAMSHI YA) DUA YENYE KUJIBIWA. Soma Zaidi...

Kitabu Cha Dua 120
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KULELEWA NA BABA YAKE MDOGO MTUME (ABU TALIB)
KULELEWA NA BABA YAKE MDOGOBaada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake. Soma Zaidi...

Hadhi na haki za Mwanamke Ulaya Wakati wa mapinduzi ya viwnda
Soma Zaidi...

hizi ndio nguzo za swala, swala za faradhi na suna
Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat al-Falaq na surat an-Nas na fadhila za kusoma sura hizi
SURAT AL-MUAWIDHATAYN (SURAT AL-FALAQ NA SURATUN-NAS) Inaelezwa kuwa sura mbili hizi zilishuka pamoja, na maulamaa wanaelezea kuwa Mtume (s. Soma Zaidi...

Ghasia na chokochoko za Makhawariji na kuuliwa kwa Ally
Soma Zaidi...

Faida za Kuwa mwenye Subira na Uvumilivu
29. Soma Zaidi...

Hii ndio namna ya kuswali kama alivyoswali Mtume s.a.w
Mtume (s. Soma Zaidi...