Kiungulia kwa wajawazito, dawa yake na njia za kukabilianannacho
Wajawazito wamekuwa wakisumbuliwa sana na kiungulia, makala hii itakujulisha njia za kukabiliana na kiungulia, dalili zake na dawa zake
Dawa ya kiungulia kwa wajawazito.
Kiungulia ni moka katika matatizo yanayotokea katika mfumo wa chakula. Kiungulia si katika mambo ya hatari, ila huwa ni hali sumbufu sana hasahasa kwa wajawazito. Kama na wewe unasumbuliwa sana na kiungulia makala hii ni kwa ajili yako. Hapa tutaoa sababu za kiungulia, matibabu yake na njia za kuepuka kiungulia.
Nini husababisha kiungulia cha mara kwa mara kwa wajawazito?
1.Ni kuwa wakati wa ujauzito kuna mabadiliko mengi ya homoni yanatokea kwa mwanamke. Mabadiliko haya yanapelekea misuli ya kooni inayounganisha tumbo na koo, kujiachia mara kwa mara na hivyo kusababisha tindikali iliyopo tumboni kupanda juu, na kusababisha kiungulia. Hali hii huweza ktokea sana pale unapolala baada ya kula chakula kingi.
2.Kadiri mtoto anavyoendelea kukuwa na mimba inavyosonga mbele ndivyo mtoto anaongeza mkandamizo kwenye tumbo. Hali hii inapelekea tindikali iliyopo tundoni kusukumwa kupanda juu na hatimaye kusababisha kiungulia.
Je ujauzito unasababisha kiungulia?
Hapana, ujauzito hausababishi kiungulia ila unaongeza uwezekano wa kupata kiungulia. Kivipi?, ni hivi mwanzoni mwa ujauzito koo lako linachukuwa chakula kidogokidogo, na kwa kuwa kuna mabadiliko mengi yanatokea husababisha mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi kidogokidogo hivyo kuchelewa kukimeng’enya chakula kwa haraka. Hali hii husaidia mwali kupata muda wa kutosha kufyonza chakula na kukipeleka kwa mtoto, ila kwa upande mwingine hali hii husababisha kiungulia.
Hata hivyo si kila mjamzito atakuwa anasumbuliwa na kiungulia, ni kwa sababu kuna mambo mengi yanafngamanna na kiungulia. Hali namna ambavyo mjamzito anaishi inaweza kuchangia kupata kiungulia. Namna mtu alivyo, vyakula anavyokula, namna anavyolala na hata mavazi pia yanaweza kuchangia kupata kiungulia.
Mjamzito afanye nini kuepuka kiungulia?
1.Kla kidogo kidogo mara kwa mara na hakikisha hunywi maji wakati wa kula
2.Kula kidogo na hakikisha unatafuna kila tonge kwa ufanisi zaidi
3.Wacha kula unapokaribia kulala
4.Punguza kula vyakula kama chokoleti, vyenye mafuta mengi, vyenye pilipili na vyenye uchachu
5.Usilale baada ya kula angalau unaweza kusimama ama kutembea.
6.Wacha kuvaa nguo za kubana sana
7.Unapolala hakikisha kichwa chako kinakuwa juu, unaweza kutumia mto ama mfano wake
8.Unapolala lalia ubavu wa kushoto
9.Tafuna bigji zisizo na sukari baada ya kula
10.Kunywa maziwa kama unayo unapohisi kiungulia
11.Kunywa asali kama unayo unapohisi kiungulia.
Dawa za kutibu kiungulia
Unaweza kutibu kiungulia kwa kutumia antacid kama vile Tums, Rolaids na Maalox.dawa ambazo zimetengenezwa kwa madini ya calcium carbonate au magnesium ni nzuri pia. Magnesium si nzuri kama ujauzito upo mwishoni.
Madaktari wengi wanakataza matumizi ya antacid ambazo zimechanganywa na sodium, ama zila lebo ya aluminium carbonate kwani zinawza kupelekea kukosa choo. Pia dawa hizi za kiungulia zinakatazwa kwa wajawazito Alka-Seltzer.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 web hosting 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 ai web app 👉5 Dua za Mitume na Manabii 👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Mambo ya kuzingatia kwa mama ili apate huduma endelevu.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na huduma kwa mama wajawazito na waliojifungua.
Soma Zaidi...Dali za udhaifu wa mbegu za kiume.
Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo zinaweza kujitokeza na zikaonesha kwamba mbegu za kiume ni dhaifu au ni chache.
Soma Zaidi...Dalili na sababu za Kukosa hedhi
Post hii inaongelea kuhusiana na Kukosa hedhi ambapo kitaalamu hujulikana Kama Amenorrhea ni kutokuwepo kwa hedhi - hedhi moja au zaidi ya kukosa. Wanawake ambao wamekosa angalau hedhi tatu mfululizo wana amenorrhea, kama vile wasichana ambao hawajaanz
Soma Zaidi...Mimba changa: Dalili za hatari unazotakiwa kuzijua.
Miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito (trimester ya kwanza) ni kipindi nyeti sana kwa ukuaji wa mtoto na mabadiliko ya mwili wa mama. Ingawa ni kawaida kuhisi uchovu au kichefuchefu kidogo, kuna baadhi ya dalili ambazo si za kawaida na zinaashiria dharura ya kitabibu. Makala hii inaangazia ishara za hatari unazopaswa kuzitilia maanani ili kulinda afya yako na ya kiumbe ulichobeba.
Soma Zaidi...Unakuta siku imefka ya hedhi kabla haijaanza kutoka hedhi yanatoka maji meupe clean kabisa hii Ina naamisha nini?
Kutoka na majimaji ka uchache kwa mwanamke sio jambo lakishangaa sana. Damu hii inawezapiabkikbatana damu na maumivu makali.
Soma Zaidi...Je? Naomba kuuliza mkewangu ali ingiya kwenye hezi siku tatu damu ikakata nikakutana nae siku ya nane je? Anaweza pata ujauzito
Idadi ya siku hatari za kupata mimba hutofautiana kutoka kwa mwanamke mmoja namwinhine. Kinda ambao idadivyavsikuvzao za hatari ni nyingi kuliko wengine.
Soma Zaidi...