Vitamini A ni katika vitamini fat soluble vitamin akama vile retinol, retinal, retinoic acid na beta-carotene.
Vitamini A ni katika vitamini fat soluble vitamin akama vile retinol, retinal, retinoic acid na beta-carotene. Vitamini A ni moja kati ya vitamini vingi. Vitamini vingine ni viamini b, C, D, E, K. unaweza kupata vitamini A sana kwenye mboga za majani za kijani, maini, mayai, maziwa, karoti na spinach. Katika makala hii tutakwenda kuona mengi kuhusu vitamini A, kazi zake, vyakula vya vitamini A pamoja na athari za upungufu wake mwilini:
Yaliyomo:
1.Maana ya vitamini A
2.Kazi za vitamini A
3.Vyakula vya vitamini A
4.Upungufu wa vitamini A
5.Athari za kuzidi kwa vitamini A
Maana ya vitamini A
Vitamini ni aina ya fat soluble vitamini ambayo ni kampaind ogania (organic compound) inayopatikana katika makundi kama retinol, retinal, retinoic acid na provitamin ambazo ni beta-carotene. Vitamini A ni muhimu katika ukuaji, uboreshwaji wa mfumo wa kinga na kuboresha afya ya macho.
Ugunduzi wa vitamini A umeanza toka miaya ya 1816 na Mwanasayansi aliyejulikana kwa jina la Francois Magendie alipokuwa akimfanyia uchunguzi mbwa mgonjwa. Baada ya hapo tafiti mbalimbali zikafata mwaka 1912, 1913, 1918, 1920 na 1939 na 1947. vitamini A vimepewa jina hili katika tafiti za mwaka 1920.
Kazi za vitamini A
1.Husaidia katika afya ya macho yaani kuona
2.Husaidia katika ukuaji
3.Husaidia katika kuboresha mfumo wa kinga mwilini
4.Husaiia katika ukuaji wa mimba na mtoto aliye tumboni
5.Husaidia katika afya ya mifupa
6.Husaidia katika afya ya ngozi
7.Husaidia katika afya ya meno
8.Husaidia katika utengenezwaji wa uteute mwilini.
Vyakula vya vitamini A
1.Maini
2.Karoti
3.Viazi vitamu
4.Spinachi
5.Maboga
6.Pilipili
7.Maembe
8.Njegere
9.Maziwa
10.Mayai
11.Mboga za majani za rangi ya kijani
Upungufu wa vitamini A
Tafiti zinaonyesha kuwa upungufu wa vitamini A huathiri watoto wanaokadiriwa kufikia 670,000 waliochini ya umri wa miaka mitano kila mwaka. Pia inakadiriwa kuwa watoto katika ya 250,000 na 500,000 wanakuwa vipofu katika nchi zinazoendelea kila mwaka. Tafiti zinathibitisha kuwa chanzo kikuu cha upofu kwa watoto ni upungufu wa vitamini A.
Athari za vitamini A kupitiliza
Endapo mtu atakuwa na vitamini A vingi ndani ya mwili hata vikapitiliza kiwango ambacho mwili unaweza kudhibiti, athari zifuatazo zinaweza kutokea:-
1.Mkusanyiko wa sumu mwilini
2.Kichefuchefu
3.Kuwshwa
4.Kukosa hamu ya kula
5.Kutapika
6.Kuona maluelue
7.Maumivu ya kichwa
8.Kupotea kwa nywele na misuli
9.Maumivu ya tumbo na uchovu
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula fenesi
Soma Zaidi...Umetaja faida za matunda , mimi ninataka kujuwa Je miwa ina madhara yoyote?
Soma Zaidi...Papai ni moja kati ya matunda yenye vitamini C na virutubisho vinginevyo. Lakini papai pia ni moja kati ya vyakula ambavyo mjamzito anatakiwa awe makini navyo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea kazi za virutubisho vya protini mwilini
Soma Zaidi...hapa Tutakwenda kuona Vyakula Vya vitamini B, kazi za Vitamini B na dalili za Upungufu wa Vitamini B mwilini
Soma Zaidi...Kuna aina nyingi za vyakula kama mafuta, wanga, fati, protini na vitamini. Je! unajuwa faida zake na hasara zake?
Soma Zaidi...Okoa afya yako kwa kula tunda papai, kwa hakika hutajuta, papai lina virutubisho vingi
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula fyulisi/ peach
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kufundisha vyakuna na vinjwaji salama anavyopaswa kutumia mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Pia utajifunza vyakula na vinywaji hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.
Soma Zaidi...