SAFARI YA KWANZA YA SINBAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA KWANZA YA SINBAD Tambua kuwa baba yangu alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana katika nchi ya baghdad wakati wa utawala wa sultan harun Rashid.
![]()
Download kitabu Hiki Bofya hapa
SAFARI YA KWANZA YA SINBAD
Tambua kuwa baba yangu alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana katika nchi ya baghdad wakati wa utawala wa sultan harun Rashid. Baba yangu alifariki miaka 21 iliyopita nilipokuwa kijana kama wewe. Wakati huo nilikuwa na marafiki wengi sana. Na nilianza kutumia mali aloniachia baba na hatimaye akakaribia kuisha na marafiki wakanikimbia. Na hapo ndipo nilipoamua kuanza biashara za majini, yaani kuuza bidhaa sehemu mbalimbali za visiwa.
Nilijiandaa vizuri kwa ajili ya safari yangu ya kwanza. Na maandaliizi yalipokuwa tayari tulianza safari ya kubiashara. Safari ilikuwa salama kabisa kwa muda wa masiku. Tulipita visiwa kadhaa tukiuza na kununua. Kwa upande wangu biashara haikuwa mbaya ijapokuwa ugeni ulinisumbuwa sana. Kwa ujumla nilifurahia safari ile. Baada ya kutembea visiwa kadhaa tuliamua kumalizia katika viziwa vingine ili tuweze kurudi nyumbani. Ilitikea sikumoja ghafla upepo ulianza kubadilika na jahazi likashindika na kudhibitiwa na manahodha.
Upepo ulizidi mpaka nahodha akaamua kukiachia chombo kiende kokote, hali iliendelea kuwa mbaya mpaka bidhaa zikaanza kutumbukizwa majini ilikuokoa ualama wa maisha. Haliiliendelea kuwa mbaya hata chombo kikaanza kunywa maji. Watu wakaanza kuania rohozao, na kuanza kushika mbao zilizovunjika kutoka kwenye jahazi. Mimi nilipata mbao moja na ilinipeleka mbali zaidi ambapo sikuweza kuona hali za wenzangu kilicho endelea.
Kwa upande wangu mawimbi ya maji yalinipeleka mbali sana, nikiwa nimeshikilia tawi lile hata sikusubutu kuliachilia. Nilipofika hali ambapo sijielewi kwa kuchoka ghafla nikaona kunaweupe mbele yangu, kuangalia vizuri kilikuwa ni kijisiwa kidogo. Basi nikajitahidi kujizuia huku nikawa naiba maji ili yanipeleke kule. Kwa bahati njema kaupepo kakanipeleka kwenye kisiwa kile. Kwa msaada wa mizizi ya miti niliweza kutoka kwenye maji yale.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 ai web app 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
HADITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE
Download kitabu Hiki Bofya hapa HDITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE.
Soma Zaidi...Hadithi ya binti mwenye kufichwa mtoto wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela
Soma Zaidi...KUTOKA NYANI MPAKA KUWA CHONGO
Download kitabu Hiki Bofya hapa KUTOKA NYANI MPAKA KUWA CHONGO.
Soma Zaidi...Safari ya nne ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad
Soma Zaidi...