Hapa tunajadili sababu kuu zinazoifanya simu iwe rahisi kudukuliwa, mbinu zinazotumiwa na wadukuzi, na mambo ya kawaida ambayo watumiaji hufanya bila kujua na kujipeleka kwenye hatari.
Dukizi (hacking) ya simu imeongezeka kutokana na matumizi makubwa ya intaneti, mitandao ya kijamii, na programu zisizo salama. Wadukuzi hutumia udhaifu wa kifaa, tabia za mtumiaji, au programu hatarishi ili kupata taarifa au kudhibiti kabisa simu ya mtu.
Wi-Fi bila password ni rahisi kudukuliwa. Mara ukijiunga, mdukuzi anaweza:
Kuangalia unachotuma
Kunasa password zako
Kuingiza programu hatari kwenye simu
Hizi ni link zinazoonekana halali lakini zimeandaliwa kukuchukua:
Password
Kuweka malware
Kukudanganya utoe taarifa zako
Faili za APK zisizotoka Play Store au App Store mara nyingi huwa na spyware au keylogger zinazorekodi kila unachoandika.
Password kama:
123456
0000
jina lako
tarehe ya kuzaliwa
huifanya simu iwe rahisi kufunguliwa na mdukuzi.
Kila update hubeba “security patch”. Usipo-update, unakuwa na udhaifu ambao wadukuzi wanaujua tayari.
VPN nyingi za bure hushusha spyware au kukusanya data zako kwa siri.
Mdakuzi aliyeko karibu anaweza kuunganisha kifaa chake na chako bila wewe kujua.
Mfano app ya calculator ikitaka:
kamera
microphone
location
hiyo ni hatari. Wadukuzi hutumia njia hii kuingia.
Kutoset fingerprint, PIN ngumu, au screen lock hufanya simu iwe rahisi kufunguliwa.
Baadhi ya mafaili husambaa kama picha au video lakini yana malware ndani.
Je wajua kuwa zaidi ya 60% ya simu zinazodukuliwa hutokea kutokana na mtumiaji kubofya link moja tu ya ulaghai (phishing)?
Wi-Fi za bure, link za utapeli na apps za nje zipo katika hatari kubwa ya kudukuliwa.
Password dhaifu na kutoupdate simu kunatoa nafasi kwa wadukuzi.
Ruhusa nyingi kwa app na kutumia VPN zisizoaminika kunafungua “mlango” wa udukuzi.
Kuweka screen lock na kuwa makini unapopakua faili ni njia rahisi za kujilinda.
Umeionaje Makala hii.. ?
Tupo katika kipindi ambacho, tafiti nyingi zinahitajika kuhusu athari za AI kwenye ubunifu na taaluma.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu HDD (Hard Disk Drive) na SSD (Solid State Drive)
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza utaratibu unaotumiwa kuweka matoleo kwnye software.
Soma Zaidi...Ninutani lakini Kuna mafunzo, programmer wote hawatamsahau rafiki huyu
Soma Zaidi...Zani ilikuwa sehemu ya ku comment ni muhimu sana kwenye blog, ila Sasa sehemu hii imeondolewa kwenye blog nyingi. Ni Kwa nini hasa imeondolewa. Post hii itakujibu swali hilo
Soma Zaidi...Post hii utakwenda kujikitabzaidi kujibu swali, hata hivyo itambulike kuwa wengi wa wanasayansi waliohusika kwenye lugha hizi sio wamarekani.
Soma Zaidi...Leo tutajifunza sababu zinazoifanya simu kuwa rahisi kudukuliwa na hatua madhubuti za kuzuia udukuzi. Tutazungumza kuhusu matumizi salama ya intaneti, usimamizi wa apps, usalama wa akaunti, pamoja na tabia muhimu za kujikinga.
Soma Zaidi...Katika kompyuta, worm ni aina ya programu hasidi (malware) inayojinakili yenyewe na kusambaa kupitia mitandao bila kuhitaji kushikamana na faili au programu nyingine. Tofauti na virusi, worm husambaa haraka zaidi na mara nyingi hutumia mtandao kuenea.
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kujifunza kuhusu tofauti ya programmer na developer
Soma Zaidi...Virusi vya kompyuta ni programu hasidi (malware) inayojishikiza kwenye faili au programu halali na kujiendesha pale faili hiyo inapofunguliwa. Virusi vinaweza kuharibu data, kupunguza kasi ya kompyuta, au kusababisha upotevu wa taarifa.
Soma Zaidi...